Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #61
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha, nimefurahi kujua jina jingine la Rumaliza, kumbe alikuwa anaitwa bw Muhammad! Ila mi nafahamu Rumaliza alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa utumwa, alitesa sana ndugu zetu kuanzia kongo mashariki hadi Bwagamoyo, sawa kwamba alikuwa rafiki wa mkwawa inashangaza!Nabii...
Uzuri ni kuwa nami nina haki ya kueleza historia niijuayo ya TANU ambayo haikatai ukweli.
Kweli Nyerere ni Rais wa TANU kadi yake no. 1.
Lakini ukiishia hapo utakuwa umejipunja.
Muhimu ueleze pia kuwa kadi hiyo aliandikiwa na Ally Sykes ambae kadi yake ni no. 2 na Abdul Sykes kadi yake no. 3.
Hawa wote ni washindi.
Umemtaja Mkwawa.
Niliwashtua wengi nilieleza hapa kuwa Mkwawa jina lake ni Abdallah alikuwa na nduguye akiitwa Yusuf na alikuwa mmoja katika majemadari wake.
Mkwawa alikuwa na rafiki yake ambae ndiye aliyekuwa akimpatia silaha jina lake Muhammad bin Khalfan Al Barwani lakini akifahamika zaidi kwa jina la Rumaliza.
Ndani ya jeshi lililokwenda kupigana na Mkwawa Kalenga walikuwapo Sykes Mbuwane na Chief Mohosh (Affande Plantan) kutoka Kwa Likunyi Imhambane, Mozambique.
Huyu Mbuwane ni babu yake Abdul Sykes yaani baba yake Kleist Sykes.
Nabii...Hahaha, nimefurahi kujua jina jingine la Rumaliza, kumbe alikuwa anaitwa bw Muhammad! Ila mi nafahamu Rumaliza alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa utumwa, alitesa sana ndugu zetu kuanzia kongo mashariki hadi Bwagamoyo, sawa kwamba alikuwa rafiki wa mkwawa inashangaza!
Mi najua rafiki yake Rumaliza ni Tip Tipp, mtu mmoja katilikatili hivi sijui aliishia wapi, nimewahi kusoma ka kitabu nafikiri kalikuwa ka 'diary" ameandika mwenyewe kwa kiswahili cha wakati huo, library ya mkoa Tabora, kinafurahisha sana japo mwenyewe anaudhi!!