Kikao cha kuunda TANU nyumbani kwa Hamza Kibwana Mwapachu - Nansio, Ukerewe 1953

Kikao cha kuunda TANU nyumbani kwa Hamza Kibwana Mwapachu - Nansio, Ukerewe 1953

Vesuvius...
Nimekueleza kuwa Abdul Sykes alianza mazungumzo na Chief David Kidaha Makwaia kuchukua nafasi ya TAA President waunde TANU.

Nadhani hili halikukupendeza na pengine hukupata kulijua.

Wengi wenu hampendezewi na ukweli kuwa harakati za kuunda TANU zilianza hata Nyerere hajafahamika Dar es Salaam.

Ndiyo mnakuja na "wazee" wa Nyerere na ambao hata majina yao hamyajui kueleza "karama" zake.

Kama kulikuwa na wazee katika kumuunga mkono Nyerere mbona mchango wa Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika hauelezwi au wa Mshume Kiyate?

Kama kweli ziko karama TANU isingesubiri iundwe nyumbani kwa Hamza Mwapachu katika kikao cha watu watatu - Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Hii mipango ikaendelea katika mikutano ya siri nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu nyumba ambayo Nyerere alikwenda kuishi baada ya kuacha kazi ya ualimu?

Nyerere inaelekea hakuipenda historia hii na ndiyo maana ikafutwa.

Wengi historia ya kweli ya TANU inakutaabisheni.

Aliyekwepa ukweli wa historia ya TANU kwa nguvu si mimi.

Mimi nimekuja hapa na historia ambayo wewe kwa mara yako ya kwanza umeisikia kwangu.

Historia hii ni historia ya wazee wangu na nina haki ya kuieleza na kuilinda isivurugwe.
Ikawaje Kidaha akakosa akapata wakuja Nyerere? Maelezo yako ni mengi ila hayajibu swali hili. Nyerere alipata kwa uwezo wake ama hao waanzilishi walighairi kumpa Kidaha ama mwingine yeyote na kuamua kumpa Nyerere? Kwa sababu zipi? Unampata mtu kama Nyerere mara moja tu kwa kizazi..huo ukweli uchukue
 
TANU wasingeweza kuandika kuhusu Mufti Hassan Ameir, aliefukuzwa Tanganyika kwa sababu za kueneza chuki za kidini na kuwagawa wananchi.....Utaandikaje historia ya mtu kama huyo? Hata historia ya Oscar Kambona imefutwa kwa makosa yake ya UHAINI....
Vito...
Unapata wapi taarifa hizi za uongo?
Kwa nini mathalan huniulizi nikakueleza kilichotokea?

Hamza Aziz alikataa kumkamata Sheikh Hassan bin Ameir alipoambiwa kuwa akamatwe kwa kuwa alikuwa anapanga kupindua serikali.

Alikataa kutii amri akisema huo ni uongo.
Haya kanieleza Hamza Aziz mwenyewe.

Ikiwa Kambona kafutwa katika historia kwa uhaini Abdul Sykes na yeye kafutwa kwa sababu ipi?
Nina paper, ''Islam and Politics,'' nimeeleza kisa chote cha Sheikh Hassan bin Ameir East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na kupigwa kwake marufuku ili kuzuia ujenzi wa Chuo Kikuu na mipango mingine ya elimu kwa Waislam.
  1. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  2. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

1652246985786.png
 
Ikawaje Kidaha akakosa akapata wakuja Nyerere? Maelezo yako ni mengi ila hayajibu swali hili. Nyerere alipata kwa uwezo wake ama hao waanzilishi walighairi kumpa Kidaha ama mwingine yeyote na kuamua kumpa Nyerere? Kwa sababu zipi? Unampata mtu kama Nyerere mara moja tu kwa kizazi..huo ukweli uchukue
Vesus...
Unataabika kwa kuwa unadhani mimi nia yangu ni kumdogosha Nyerere ndiyo maana unakuja na fikra ya kujaribu kunieleza umuhimu wa Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika na unakuja na lugha ambazo si za kiungwana za ''mtu wa kuja.''

Hakika dunia nzima haiwezi kuzaliwa Dar es Salaam.
Nyerere kuzaliwa kijijini haikupata kuwa jambo muhimu kwa wazee wetu.

Huko nyuma nimeeleza kuwa katika kikao cha Nansio Hamza Mwapachu alimwambia Abdul kuwa yeye anaona Nyerere anafaa zaidi kuongoza harakti za uhuru kushinda yeye.

Lakini kubwa alimwambia, ''Abdul wewe Muislam hatutaki ionekane kuwa harakati hizi za kudai uhuru ni harakati za Waislam peke yao.''

Hamza Mwapachu alikuwa mkubwa kwa Abdul Sykes kwa miaka 11.
Yapo mengi.

Ila unanishangaza sana kuwa mpaka sasa hujashtuka kwa nini Nyerere miaka yote alikuwa kimya katika historia hii?

Abdul Sykes hayuko katika historia ya TANU wala katika historia yake miaka kwa miaka na yeye yuko kimya tuli kabisa.

Chief Kidaha yeye alikuwa akitawala machifu karibu 50 chini yake Usukumani na pia alikuwa katika Baraza la Kutunga Sheria.

Majukumu haya yalimzuia kuingia TAA kupigania uhuru wa Tanganyika.

1652248218724.png

Abdul Sykes na Hamza Mwapachu
 
Hii historia ni nzuri lakini swali langu ni je kuna maslahi yoyote labda watu hawa walistahili hawakupata au ushindani ni wa nini labda?

Au Nyerere hakustahili sifa zote anazopewa kama Baba wa Taifa?
Balotel,
Kilichonifanya mimi kuandika historia ya TANU ni kuwa walioandika historia ya TANU walikuwa hawaijui.

Sikuandika kwa lingine lolote lile ila kueleza ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika.
 
Vesuvius...
Nimekueleza kuwa Abdul Sykes alianza mazungumzo na Chief David Kidaha Makwaia kuchukua nafasi ya TAA President waunde TANU.

Nadhani hili halikukupendeza na pengine hukupata kulijua.

Wengi wenu hampendezewi na ukweli kuwa harakati za kuunda TANU zilianza hata Nyerere hajafahamika Dar es Salaam.

Ndiyo mnakuja na "wazee" wa Nyerere na ambao hata majina yao hamyajui kueleza "karama" zake.

Kama kulikuwa na wazee katika kumuunga mkono Nyerere mbona mchango wa Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika hauelezwi au wa Mshume Kiyate?

Kama kweli ziko karama TANU isingesubiri iundwe nyumbani kwa Hamza Mwapachu katika kikao cha watu watatu - Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Hii mipango ikaendelea katika mikutano ya siri nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu nyumba ambayo Nyerere alikwenda kuishi baada ya kuacha kazi ya ualimu?

Nyerere inaelekea hakuipenda historia hii na ndiyo maana ikafutwa.

Wengi historia ya kweli ya TANU inakutaabisheni.

Aliyekwepa ukweli wa historia ya TANU kwa nguvu si mimi.

Mimi nimekuja hapa na historia ambayo wewe kwa mara yako ya kwanza umeisikia kwangu.

Historia hii ni historia ya wazee wangu na nina haki ya kuieleza na kuilinda isivurugwe.

Mi nafikiri defend agenda yako wewe mwenyewe na si kwamba sababu ni historia ya wazee wako basi haiwezi kupingwa? Kwahiyo Makongoro nae aje hapa a defend historia ya TANU sababu tu nia mzee wake?
 
Mi nafikiri defend agenda yako wewe mwenyewe na si kwamba sababu ni historia ya wazee wako basi haiwezi kupingwa? Kwahiyo Makongoro nae aje hapa a defend historia ya TANU sababu tu nia mzee wake?
Nduka...
Mimi sina tatizo na mtu yoyote awaye yule.

TANU ingekuwa ya Nyerere Abdul na Ally Sykes wasingekuwa na kadi za TANU No. 2 na 3 wala mimi nisingeandika historia ya TANU kwa kusoma Nyaraka za Sykes.

Ikutoshe tu kuwa kadi no. 1 ya Julius Nyerere kaandikiwa na Ally Sykes.

Sina shida wala simlazimishi mtu kukubali yote niliyoandika kuhusu historia ya TANU.

Kwa miaka mingi sana watu waliishi wakiwa hawajui historia hii na wala haikuwa shida kwa yoyote.
 
History of Tanzania kuna lecture mmoja yupo nondo mno anitwa DANIEL SEMBURI
 
Nimekuelewa, TAA haikuwa chama cha siasa, bali ulikuwa ni muungano wa wafanyakazi, na waafrika kutetea haki zao kwa serikali,...Nyerere alipoingia madarakani, aliibadili TAA kutoka chama cha wanaharakati wa kiafrika ,mpaka kuwa chama cha siasa cha kupigania Uhuru. Historia ya TANU inaanzia pale Nyerere alipoingia madarakani...Nyerere ndio aliekuwa mpangaji wa mipango yote ya chama.....Wengine walikuwa wasindikizaji tu
Umemaliza
 
Umemaliza
Ed...
Tatizo kubwa ninaloliona kwenu ni kule kuwa mna fikra imejengeka vichwani kwenu kuwa mnajua historia ya TANU na Nyerere ilhali hamjui chochote.

Kulikuwa kuanzia mwaka wa 1950 ndani ya TAA kamati ndogo ya siasa TAA Political Subcommittee wajumbe wakiwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Huu ndiyo ulikuwa wakati Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes walipochukua uongozi wa TAA kwa madhumuni sasa ya kuunda chama kamili cha siasa.

Huu ndiyo wakati hata ukisoma Tanganyika Intelligence Summary taarifa za Special Branch utaona zinasema Abdul alihuisha matawi mengi majimboni na akafanya mkutano wa siri na Jomo Kenyatta Nairobi.

Kuanzia 1950 hadi 1953 serikali ya kikoloni ilitoa Government Circular 5 ikionya TAA kutojihusisha na siasa.

Nashangaa kuwa wewe uwe na fikra mwaka wa 1929 Kleist Sykes na wenzake wangekwenda kusajili African Association kama chama cha siasa.

Unadhani Waingereza wangewapa tasjila?

Mtafiti makini atapenda kujua hali ya siasa ya Tanganyika kabla TANU haijaundwa.

Hii ni historia ya miaka 25 na Kleist Sykes kaandika mswada wa kitabu kuhusu historia hii.

Kaeleza kila kitu hadi kuwa Kanisa likiwakataza waumini wake kujihusisha na siasa.

Msome Aisha Daisy Sykes Seminar Paper, "The Life of Kleist Sykes," (1968) iko Dar es Salaam University Library, East Africana.

Hivi kwa nini mnakimbilia kuandika mambo msiyoyajua badala ya kuuliza?
 
Yaani huyu Mohamed Said anaulizwa kingine, anajibu kingine, tena kwa maelezo marefuu. Napoteza tu muda wangu kusoma majibu yake, heri nikale zangu kitimoto (nguruwe) mie.
 
Yaani huyu Mohamed Said anaulizwa kingine, anajibu kingine, tena kwa maelezo marefuu. Napoteza tu muda wangu kusoma majibu yake, heri nikale zangu kitimoto (nguruwe) mie.
Love...
Wewe unalo jibu ambalo unalitaka.

Kwa kuwa hulipati unachopata ni historia zaidi usiyoipenda unataabika.
Kwa jinsi ulivyomaliza kifedhuli nimekuelewa vyema.
 
Mzee muhammed kuna mengi tukiyasoma na kuchambua akili zinaanza kurudi.

nikianza kufatilia historia naona walio taka uhuru ilikuwa umoja wa waislamu na ikuanza leo na baada waingereza kupuuzia sana.

wamesababisha mengi hata zanzibar hawa waingereza sema ndio hivo
 
Hamna mtu alitawaliwa Afrika au kuchukuliwa utumwani kisa dini fulani kuja kusema waliogombania uhuru sijui dini fulani huo ni wazimu mkuu
 
fikraHamna mtu alitawaliwa Afrika au kuchukuliwa utumwani kisa dini fulani kuja kusema waliogombania uhuru sijui dini fulani huo ni wazimu mkuu
Ed...
Hizo ni fikra zako siwezi kukulaumu hapa tuko katika mjadala na ni ustaarabu kusikiliza hoja za wenzako nami nimekusoma na naheshimu hoja yako.

Lakini katika historia ya jinsi TANU ilivyoingia Southern Province matatizo ni kuwa Kanisa lilikuwa likiwaasa waumini wake wasijiingize katika siasa za TANU kwani hicho ni chama cha Waislam kinataka kuleta Vita Vya Maji Maji.

Halikadhali wakati African Association (AA) inaasisiwa Dar es Salaam hali ilikuwa kama hiyo pia na ndiyo maana utaona harakati za AA hadi TANU zilitawaliwa zaidi na Waislam.

Hiyo picha hapo chini naomba uiwekee ''caption,'' ni safarii ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.

Hao akina mama wanamsindikiza Mwalimu uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na dhifa ya kumuaga ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Najua unapata shida na historia hii lakini ndivyo ilivyokuwa.

Historia hii ilifutwa lakini sisi watoto wa hao akina mama wazalendo kwenye hiyo picha hapo juu tumeiandika kwa mikono yetu na sasa inasomwa kama sehemu ya historia ya TANU na historia ya kupigania uhuru.

Kwa hakika hii ni historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

1652303082262.png
 
Mzee muhammed kuna mengi tukiyasoma na kuchambua akili zinaanza kurudi.

nikianza kufatilia historia naona walio taka uhuru ilikuwa umoja wa waislamu na ikuanza leo na baada waingereza kupuuzia sana.

wamesababisha mengi hata zanzibar hawa waingereza sema ndio hivo
Chiz...
WALIFIKAJE TAREHE 7 JULAI 1954 NA KUUNDA TANU NA TUNAWAADHIMISHAJE WAZALENDO HAWA?

Kuna mtaa Dar es Salaam sisi tulimezaliwa tumeukuta ukiitwa Stanley Street.

Baada ya kupatikana uhuru mtaa huu ukabadilishwa jina ukaitwa Aggrey Street kisha baadae wakati marehemu Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ukabadilishwa tena jina ukaitwa Mtaa wa Max Mbwana.

Mtaa huu umepewa majina ya watu maarufu watatu ambao wote wamekuwa na uhusiano wa kihistoria kuanzia Tanganyika hadi kufika Tanzania.

Henry Morton Stanley ndiye aliyetumwa kuja Tanganyika kumtafuta David Livingstone na akamkuta Ujiji.

Dr. Aggrey alikuwa Mwafrika kutoka Ghana.

Umaarufu wake unatokana na kuwa yeye alikuja Tanganyika mwaka wa 1924 akiwa mmoja wa wajumbe wa kamisheni iliyokuja Tanganyika kuja kuchunguza elimu ya Waafrika.

Wajumbe wengine wote waliobakia katika kamisheni hii walikuwa Wazungu.

Kleist Sykes anaeleza katika mswada wa maisha yake alioandika kabala ya kifo chake mwaka wa 1949 kuwa alikuwa Dr. Aggrey ndiye aliyemtia hima aunde African Association.

Dr. Aggrey alimpa Kleist ushauri huu baada ya kutambua kuwa Waafrika wa Tanganyika hawakuwa na umoja wao, wakati Wazungu, Waasia na Waarabu wote tayari walikuwa na jumuia zao.

Katika mswada wake ule Kleist anasema kuwa Waafrika waliwakiishwa na Father Gibbons kutoka Misheni ya Minaki ambae yeye anastaajabu kwa kuwa hakuwa na uhusiano wala muiingiliano wowote na Waafrika wa Tanganyika.

Father Gibbons ni huyo wa kwanza waliosimama kushoto kwenye picha.

Kwa sifa hii ya Aggrey kuja Tanganyika akiwa Mwafrika msomi Jiji la Dar es Salaam wakabadili jina la Stanley na kuliweka jina la Dr. Aggrey.

Kitwana Kondo akiwa Meya wa Dar es Salaam akabadili tena jina la mtaa kutoka Aggrey ukaitwa Mtaa wa Max Mbwana.

Mzee Max Mbwana alikuwa mmoja wa wazee maarufu wa Dar es Salaam waliounga mkono harakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baraza la Wazee wa TANU 1955 katika picha hapo chini:

1. Abdallah Shomari (Tandamti Street No. 3)
2. Nassoro Kalumbanya (Simba str.)
3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo Street)
4. Mtoro Ally (Muhonda Street.)
5. John Rupia (Misheni Kota)
6. Julius Nyerere( Pugu Sekondari)
7. Said Chaurembo (Congo/Mkunguni Street.)
8. Jumbe Tambaza( Upanga)
9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili)
10. Dossa Aziz ( Mbaruku /Somali Kipande Street )
11. Mshume Kiyate (Tandamti Street)
12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo )
13. Maalim Shubeti (Masasi/Likoma Street)
14. Rajab Simba (Kiungani Street)
15. Waziri Mtonga (Kilosa no. 18, Ilala)
16. Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
17. Maxi Mbwana ( Aggrey /Kongo Street)
18. Usia Omari (Sungwi ,Kisarawe)
19. Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo)

Kulia wa pili waliokaa Sheikh Suleilan Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU 1954 - 1958) (Swahili/Kariakoo Street).

Muhimu kufahamika ni kuwa Jiji la Dar es Salaam lilipotoa jina la mtaa wa huu kwa Dr. Aggrey hawakutoa kwa kuenzi ile fikra yake ya kuwataka Waafrika waunde African Association.

La hasha, jina la mtaa lilitolewa kwa ile sifa yake ya yeye kuwa Mwafrika msomi aliyefika Tanganyika wakati ule wa ukoloni.

Max Mbwana alipewa mtaa kwa mchango wake katika kuunga mkono TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia ya TANU inaanza hapa alipofika Dr. Aggrey Tanganyika na kumshauri Kleist na wenzake kuanzisha umoja wa Waafrika wa Tanganyika.

Hata hivyo ilimchukua Kleist miaka mitano hadi 1929 kuasisi African Association akiwa katibu muasisi na rais muasisi akiwa Cecil Matola.

Mkutano wa kuunda African Association ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola Mtaa wa Ndanda na Masasi.

Nyumba hii baadae ikaja kununuliwa na John Rupia na ipo hadi leo.

Waliokusanyika pale kuasisi African Association walikuwa Kleist Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Hili lilikuwa kundi la wazalendo tisa walioanza kufunga safari ngumu ya kuelekea New Street kuja kuunda TANU tarehe 7 Julai 1954.

Bahati mbaya sana ni kuwa wazalendo hawa hawafahamiki katika historia ya Tanganyika na kwa hakika historia hii isingelijulikana kama Kleist asingeandika historia ya maisha yake.

Mswada wake huu ulichukua miaka 24 hadi 1973 kufikia kuchapwa na kama si juhudi za John Iliffe mswada ungebaki kama ulivyoandikwa na mwishowe kutoweka kama zilivyotoweka nyaraka nyingi katika historia ya Waafrika wa Tanganyika.

Mswada huu ulichapwa katika kitabu alichohariri Iliffe, ‘’Modern Tanzanians,’’ kilichopigwa chapa na Tanzania Publishing House.

Nyaraka hizi za Sykes zimesaidia sana katika kuhifadhi si historia hii ya African Association bali hata historia ya TANU.

Abdul Sykes alimpa mswada huu pamoja na nyaraka nyingine binti yake Daisy, wakati ule mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kupitia nyaraka hizi mwalimu wake wa historia, John Ilife aliweza kujua mengi ambayo yalimsaidia katika kuiandika kwa uhakika historia ya African Association.

Nyaraka hizi ndizo nyaraka pekee zilizoweza kuhifadhiwa kutoka kwa waasisi wa African Association waliokuwapo kati ya mwaka wa 1929 hadi 1954 ilipokuja kuasisiwa TANU.

Kushoto: Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana Julius Nyerere na Mshume Kiyate, 1962.
Ukitaka kusoma makala kamili ingia:

http://mohamedsaidsalum.blogspot.com/search...

Screenshot_20220512-002822_Facebook.jpg

Screenshot_20220512-003112_Facebook.jpg
 
Kumbe ukifanya kosa yoyote inapelekea historia yako inafutwa? Hii nadhani ipo Tanzania pekee... Maajabu sana.
TANU wasingeweza kuandika kuhusu Mufti Hassan Ameir, aliefukuzwa Tanganyika kwa sababu za kueneza chuki za kidini na kuwagawa wananchi.....Utaandikaje historia ya mtu kama huyo? Hata historia ya Oscar Kambona imefutwa kwa makosa yake ya UHAINI....
 
Kwa kawaida historia ni kwa washindi tu, ndio maana tunamsoma mkwawa, mirambo n.k Kama vile walipanga au kuongoza mapambano peke yao, ukweli ni tofauti kidogo, lakini hao ndio waliotengeneza historia na itabaki hivyo.

Kwamba nyerere ndio alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU, CCM na Rais wa kwanza wa Tanganyika/ Tanzania huyo ndio mwamba wa Historia, hata tungeandika historia mpya huku tunatembea uchi, haibadili chochote, ni kupoteza muda bure
 
Nabii...
Uzuri ni kuwa nami nina haki ya kueleza historia niijuayo ya TANU ambayo haikatai ukweli.

Kweli Nyerere ni Rais wa TANU kadi yake no. 1.

Lakini ukiishia hapo utakuwa umejipunja.
Muhimu ueleze pia kuwa kadi hiyo aliandikiwa na Ally Sykes ambae kadi yake ni no. 2 na Abdul Sykes kadi yake no. 3.

Hawa wote ni washindi.
Umemtaja Mkwawa.

Niliwashtua wengi nilieleza hapa kuwa Mkwawa jina lake ni Abdallah alikuwa na nduguye akiitwa Yusuf na alikuwa mmoja katika majemadari wake.

Mkwawa alikuwa na rafiki yake ambae ndiye aliyekuwa akimpatia silaha jina lake Muhammad bin Khalfan Al Barwani lakini akifahamika zaidi kwa jina la Rumaliza.

Ndani ya jeshi lililokwenda kupigana na Mkwawa Kalenga walikuwapo Sykes Mbuwane na Chief Mohosh (Affande Plantan) kutoka Kwa Likunyi Imhambane, Mozambique.

Huyu Mbuwane ni babu yake Abdul Sykes yaani baba yake Kleist Sykes.
 
Nipo nachukua notes
 
Back
Top Bottom