Kikao cha kuunda TANU nyumbani kwa Hamza Kibwana Mwapachu - Nansio, Ukerewe 1953

Hahaha, nimefurahi kujua jina jingine la Rumaliza, kumbe alikuwa anaitwa bw Muhammad! Ila mi nafahamu Rumaliza alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa utumwa, alitesa sana ndugu zetu kuanzia kongo mashariki hadi Bwagamoyo, sawa kwamba alikuwa rafiki wa mkwawa inashangaza!

Mi najua rafiki yake Rumaliza ni Tip Tipp, mtu mmoja katilikatili hivi sijui aliishia wapi, nimewahi kusoma ka kitabu nafikiri kalikuwa ka 'diary" ameandika mwenyewe kwa kiswahili cha wakati huo, library ya mkoa Tabora, kinafurahisha sana japo mwenyewe anaudhi!!
 
Nabii...
Hizi ndizo changamoto za historia.

Hakika Rumaliza, Tip Tippu wote wamehusika katika biashara ya utumwa na ya pembe za ndovu.

Lakini hawakuwa peke yao biashara ya utumwa imefanywa na mataifa mengi makubwa.

Rumaliza alkuwa pia na misuguano na Wamishionari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…