Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kikosi cha Walinda Amani cha Tanzania kinachohudumu chini ya mwamvuli wa FIB-MONUSCO kimehitimisha rasmi jukumu lake la ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupitia gwaride maalumu la makabidhiano kati ya TanzQRF ya 4 na TanzQRF ya 5. Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya kituo cha kikosi hicho kilichopo Beni-Mavivi, jimboni Kivu Kaskazini.
Akizungumza mara baada ya gwaride hilo, Kamanda wa Kikosi cha 5, Luteni Kanali David Nkungu, amesema kuwa jukumu lao ni kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufasaha na weledi, huku wakizingatia mamlaka waliyopewa na Umoja wa Mataifa ya kulinda raia na mali zao chini ya MONUSCO, ili kuhakikisha amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hususan katika jimbo la Kivu Kaskazini, inaendelea kudumishwa.
Kwa upande wake, Meja Rafael Ngombale, akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa TanzQRF Kikosi cha 4, Luteni Kanali Omary Yahya aliyemaliza muda wake, amesema kuwa baadhi ya mafanikio ya kikosi hicho ni pamoja na kurejesha hali ya amani na utulivu, hatua iliyowawezesha raia kurejea katika shughuli zao za kila siku tofauti na hali ilivyokuwa awali.
Kwa makabidhiano haya, safari ya ulinzi wa amani iliyokuwa ikitekelezwa na Kikosi cha 4 cha TanzQRF katika jimbo la Kivu Kaskazini imekamilika rasmi, na jukumu hilo sasa limekabidhiwa kwa Kikosi cha 5 cha TanzQRF kutoka Tanzania.