Kikosi Kazi kimeundwa na Msajili sio Rais, na wajumbe wake hawajaapa mbele ya Rais

Kikosi Kazi kimeundwa na Msajili sio Rais, na wajumbe wake hawajaapa mbele ya Rais

Nadhani ungesoma tena kilichoandikwa kwenye ile taarifa ujiridhishe kama kuna popote mle kunapozungumziwa sheria ya kuanzisha hiyo tume au kunazungumziwa tu sheria 40 ambazo tume hiyo ya Nyalali iliona kuna umuhimu wa kuzifuta ili kujenga mazingira ya siasa za haki nchini!.
Jisomee zaid hapa ili uwe na uelewa mpana jinsi sheria na Tume za rais zinavyofanya kazi, hazianzishwi kiholela.

Kazi ya KUPITIA sheria ZOTE za TZ na kutoa MAPENDEKEZO ya kufanyika marekebisho ni kazi ya TUME YA KUREKEBISHA SHERIA ambayo ilitokana baada ya taarifa ya Tume ya Mapitio ya Mfumo wa Mahakama (Tume ya Msekwa) ya 1977. Tume hii ilianzishwa na sheria "The Law Reform Commission Act" sheria SURA 171 ya 1980 ambapo Tume ilianza kazi RASMI mwaka 1983.

Baadhi ya MAJUKUMU ya Tume hii ni pamoja na KUBORESHA sheria, na KUPENDEKEZA kutungwa kwa sheria MPYA pale inapoonekana kuna uhitaji. Hii kazi ndiyo inayofanywa na "KIKOSI KAZI CHA RAIS" kwa sasa – kazi isiyo yake.

Tume hii ina Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe wengine wasiopungua WANNE na wasiozidi SITA. Wajumbe hawa uteuliwa na Rais na wanatakiwa kuwa na SIFA, pamoja na kuwa na degree ya sheria, sifa ya kuteuliwa kuwa Jaji, na sifa nyingine kadhaa zilizotajwa na sheria hiyo.

Hata Jaji Damian Lubuva, aliyekuwa Mwenyekiti wa NEC, alikuwa Mwenyekiti wa Tume hii inayojulikana kwa kifupi "LRCT" kati ya 1984 - 1985. Nchi nyingi zina Sheria za kuunda hizi Tume za MAREKEBISHO ya sheri, huitwa "Law Reform Commission". Hakuna kitu kinaitwa "KIKOSI KAZI".

Hii ndiyo Tume inayotambulika kisheria kusimamia marekebisho ya sheria ZOTE nchini. Sasa, ni sheria ipi inampa MAMLAKA Msajili wa Vyama vya Siasa kuunda Tume ya kushughulika na masuala ya kisheria! Nini maana ya "KIKOSI KAZI CHA RAIS" endapo wajumbe wake HAWAKUTEULIWA na Rais?

Credit to Baba Mwita from Twitter.
 
Back
Top Bottom