RWANDES
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,788
- 4,401
Kauli ya Rais wa Awamu ya 4 Dk. Jakaya Mrisho Kikwete haikuwa ya kubahatisha, huenda kwa jinsi chombo kinavyozidi kuzama mabadiliko makubwa yakafanyika ya kiuongozi mwaka 2025.
Hata hivyo kauli hiyo aliitoa hadharani, lakini ukweli ni kwamba mama mwenyewe kashawaambia baadhi ya watu wake wa karibu kuwa hatagombea kiti cha Urais, akisema kwamba kama ni kutumikia nchi ametumikia vya kutosha, anahitaji apumzike.
Chawa wa CCM ambao wamezoea kulamba asali hawataki mama apumzike, kutwa nzima ni kusema mama hadi 2030 kitu ambacho hataki kukisikia. Pamoja na yote mama amepima upepo kwa sasa, waliomzunguka ni watu hatari, walafi wa madaraka na mafisadi na hapendi kuleta uhasama nao. Yeye ameona astaafu kwa heshima, wengine waongoze chombo hiki ambacho kinayumbayumba wakati huu.
Kwa sasa uchumi umesinyaa na tunapoelekea huenda hata mishahara ya wafanyakazi baadhi ya taasisi hawatapewa kwa wakati na hili linasemwa na watu wa juu kabisa ndani ya serikali. Watu wanasema kuongoza nchi siyo lelemama, inahitaji roho ngumu na jasiri kuamua baadhi ya mambo.
Shukrani sana kwa mama Samia kuliona hilo, maana hao watu wanamtesa katika uongozi wake si kwamba anashindwa kupambana nao, bali ameona mbali kwa kuwa yeye ni hataki makuu na wale wanaojiita wenye nchi. Mama ana vyombo vyote vya dola lakini ameona isiwe tabu, 2025 astaafu aanze kuwa mtazamaji.