Pre GE2025 Kikwete: 2025 hakuna wa kuchukua fomu ya Urais ya kumpinga Samia Suluhu Hassan labda mambo yaharibike sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
nguvu na ushawishi wa Kikwete kwenye chama na serikali ipo active,chawa wa CCM wa njaa njaa hawa hii kauli ya"labda mambo yaharibike saana"angeundiwa zengwe na hata kuonywa au kuitwa kujieleza nini maana ya"labda mambo yaharibike saana".

chawa wakisifu na kuabudu huwa wanafunga kufuli,"mama atagombea tena",,,,au mama hana mpinzani',,lakini mzee Kikwete kaona uwenda mambo yakaharibika wakachagua mwingine.
 
Waseme ukweli tuu"

Hii ni awamu ya tano na raisi wa sita ama ni awamu ya sita na raisi ni awamu ya Tano?
 
Mpango gani wa JPM ambao ulikuwa na nafuu ya maisha kwa wananchi lakini serikali hii imeupa kisogo?
 
Umetumwa? Mwambie alie kutuma yupo Mungu wa wa Tanzania.
 
Sisi walala hoi tunajua na tunafurahi mvua imenyesha, sababu njaa na maisha magumu ni vitu viwili hatari Sana.Tunashukuru Mungu mvua imenyesha,angalau unga utanunulika
 
Acha uzushi wa kipuuzi Rais Samia Suluhu tuko nae mpaka 20230 hili halina mpinzani
 
Hakuna kitu kama hicho hizi ni propaganda tu Rais Samia Suluhu lazima atagombea kama katiba ya nchi inavyosema na atapita kwa kishindo acheni kuamini hizo propaganda
Maendeleo ni makubwa na yanaonekana hasa katika suala la uchumi siku izi pesa inaonekana mtaani sio kama zamani
 
Hivi watu huwa mnaongea mkiwa mnamaanisha au chuki zimewajaa kiasi akili hujitenga na macho na masikio? Ni mipango ipi unsyodai imeanzishwa na Magufuli Samia amekataa kwenda nayo kama unavyodai? Baada ya Nyerere, Samia ndiye Rais atakayeacha legacy kubwa sana kwa nchi yetu. Muheshimu Sana kiongozi anayeheshimu elimu na kuweka nguvu kwenye elimu. Tatizo la msingi la nchi hii ni elimu, jitihada za Samia kwenye elimu hazina mfanowe. Kujenga shule, madarasa mengi ya standard nzuri kabisa na vyuo vya Kati ndiyo muarobaini wa nchi hii.

Kwa upande mwingine, ulisikia Rais gani aliyeanzisha program ya block farms na kuwachukua vijana kuwapa mafunzo na kuwagawia mashamba katika maeneo yenye miundombinu ya kilimo?

Je unaona taarifa za habari siku hizi kuhusu miradi ya maji na afya inavyofunguliwa kila siku vijijini? Kuna kilio cha bei ya mbolea sasa hivi? Umeona wakulima wa korosho walilakamika dawa ya kupulizia mwaka huu? Samia anagusa kipa sekta kwa umakini mkubwa. Samia akifika 2030, ataiacha Tanzania kwenye hali nzuri Sana tena kila sekta.
 
Take a breath for a second, umelipwa sh ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…