mashikolomageni
JF-Expert Member
- Jan 5, 2010
- 1,570
- 193
Kama unakubali walishindwa kuzikarabati utasemaje tena "hata kama nyumba zilikuwa hoi serikali ingeweza kujenga nyumba mpya..." Ni sawa na mtu yuko broke anakwambia nimeshindwa ku maintain gari langu zee zee naliuza, unamwambia basi pole, nunua jipya! Kama dai lao ni kwamba hawawezi kuzi manage financially hiyo ina include hawawezi kuzibomoa na kuzijenga upya!
Kama tatizo ni ufisadi wa watumishi wa serikali na makandarasi sasa hizo nyumba mpya zingejengwa na nani na kusimamiwa na watumishi wa wapi, serikali ya Zambia?
Mbona hamueleweki? Ushasema mfumo wa kuzi maintain ulikuwa una matatizo halafu solution yake ni kujenga nyingine, this is really absurd, I am sorry to say that, but I just can't comprehend this fuzzy stuff you are saying here.
Nyumba za serikali ziliuzwa kwa sababu ya shinikizo la IMF na wahisani (tena sio shinikizo, simple agizo, maana wao ndio mabwana zetu wanaotulisha). Walisema serikali haiwezi kuwa kwenye real estate service, hasa ukizingatia kwao waziri hapewi nyumba ya bure, gari, sijui posho ya mafuta, dereva etc. Kitu ambacho nakikubali 100%. Ok, so they sat down and haggled over how do you dispose of this litany of assets that you have? Wazo la kupigwa mnada halikupita, ikaonekana watakaonunua ni Rostam Aziz na Manji na waarabu wa Dowans, au type za Mengi na Chenge na Lowassa, wale wale.One example, Tanzania Breweries iliuza nyumba zake zilizoko prime areas and not surprisingly walionunua si raia, achilia mbali si wazawa. Hatuna robust immigration enforcement ya kujua nani raia nani kanunua passport. Ndo wakauziwa watumishi kwa sharti kwamba wasiziuze tena kwa miaka 100.
Another important dimension about the sale that is always overlooked relates to the scope of the exercise, the issue of "prime areas... expensive plots." It wasn't only the properties in Masaki na Oysterbay which were involved here. Rank and file government employees and the public at large have been buying NHC houses uswahilini zile za corridor katikati chumba huku na huku way before and after agizo la Mkapa, mtawanyang'anya hawa pia, na za msajili zilizouzwa? Watu wa hali ya chini na ya kawaida nao waliuziwa nyumba, mbona hizi haziongelewi? Tena za Nationa Housing za uswahilini, unlike za Masaki, hazikuuzwa na masharti, ndo maana wanunuzi wanaziuza upya, matajiri wanazibomolea mbali wanaendeleza business plans zao, residential areas za wazawa get gentrified, wazawa misplaced. Haya hayasemwi haya. Hata kidogo.
In any event, one problem plaguing this nation is lack of information due to decrepit media. Ndo maana mchakato mzima wa kuuza nyumba haujulikani. Nyumba ziliuzwa kwa mlolongo na maagizoya kimaandishi, lakini hakuna hata kiumbe kimoja kwenye press outlet za Tanzania mwenye balls za kwenda Ujenzi au kuwabana Ikulu kudai decision making records zina details gani, ilikuaje, hakuna.
Hii ilikuwa danganya toto kula kunde mbichi.
Wengi walionunua nyumba bado wapo bungeni na serikalini sasa sijui huu mpango utapitia wapi.
Wengine walinunua kwa sh mil 20 wakauza milioni 800.
Hii yote ilikuwa danganya toto kula kunde mbichi kurudi nyumba zilizouzwa ni uongo wa hali ya juu...
Magufuli aoneshe mfano kwa kurudisha za kwake na rafiki zake...
Serikali ikitaka Nyumba inauwezo kuzichukua,kwa kuwa ndani ya mkataba kuna clause [kifungu] ambacho kinawabana waliowauzia nyumba hizo kuwa ndani ya miaka 25 hawapaswi kufanya lolote lile zaidi ya marekebisho ya kawaida.Hivyo basi kama Serikali ikapata kiongozi akafunga macho kuwa anaziitaji ITAKULA KWAO WANUNUZi,manake kitakachofanyika ni compensation.Wajanja wa ununuzi ambao wanajiita watoto wa mujini na mabilioni yao ya PESA ndio watakaoteketea kwa kuwa iliitaji uangalifu sana kwenye ununuizi wa nyumba zile.Ila kwa kuwa wamilki wa nyumba hizo kwa hapa Dar ni watu wasio zidi wanne basi itakuwa kazi nyepesi na AFRICAN EMPOWERMENT itakuwa imefanikisha kazi kwao waliokuwa mabingwa wa kubadilisha, matumizi ya viwanja.
japo serikari zetu kwa siku za karibuni zimekuwa na sifa ya kuwa dhaifu (ref. Kafulila katika kikao cha Bunge) lani suala la hizi nyumba sidhani kama litapita hivihivi. Utabiri unaonyesha muda sio mrefu zitarudiSerikali ikitaka Nyumba inauwezo kuzichukua,kwa kuwa ndani ya mkataba kuna clause [kifungu] ambacho kinawabana waliowauzia nyumba hizo kuwa ndani ya miaka 25 hawapaswi kufanya lolote lile zaidi ya marekebisho ya kawaida.Hivyo basi kama Serikali ikapata kiongozi akafunga macho kuwa anaziitaji ITAKULA KWAO WANUNUZi,manake kitakachofanyika ni compensation.Wajanja wa ununuzi ambao wanajiita watoto wa mujini na mabilioni yao ya PESA ndio watakaoteketea kwa kuwa iliitaji uangalifu sana kwenye ununuizi wa nyumba zile.Ila kwa kuwa wamilki wa nyumba hizo kwa hapa Dar ni watu wasio zidi wanne basi itakuwa kazi nyepesi na AFRICAN EMPOWERMENT itakuwa imefanikisha kazi kwao waliokuwa mabingwa wa kubadilisha, matumizi ya viwanja.
Hatimaye Kikwete Afanya Kweli
- Aagiza Nyumba za Serikali Zilizouzwa Zirejeshwe
Na Mwandishi Wetu
Rais Jakaya Kikwete ameanza mchakato wa kuhakikisha nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wake wakati wa uongozi wa Awamu ya Tatu, zirejeshwa serikalini.
Habari za uhakika kutoka baadhi ya maofisa waandamizi serikalini zinasema Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo katika mikono ya serikali kwa kuzinunua upya kutoka kwa watumishi waliokwisha kuzinunua.
Kwa mujibu wa habari hizo Rais Kikwete ameiamuru Wizara ya Miundombinu kufanya tathmini ya kina ya ununuzi wa nyumba hizo kubaini ni kiasi gani kinastahili kurejeshwa kwa wote walionunua nyumba hizo ili hatimaye zirejeshwe Serikalini.
Inaelezwa ya kuwa kitakachotathmiwa ni kiasi gani cha fedha kilichokwisha lipwa na kila aliyenunua, ikizingatiwa ya kuwa si wote ambao wamekwisha kumaliza kuzilipia nyumba hizo.
Habari ndani ya Wizara ya Miundombinu zinaeleza ya kuwa waliozinunua watatakiwa kuzirejesha na kulipwa kiasi ambacho kila mmoja alikuwa amekwishalipa kwa mujibu ya mikataba waliyopewa.
Inaelezwa kwamba Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo Serikalini kwa vile hivi sasa Serikali inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba kwa watumishi wake wanaoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali na wanaohamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa sababu hiyo serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwapangisha katika hoteli wafanyakazi wengi wapya wanaokosa nyumba katika maeneo wanayopangiwa kufanya kazi, kimesema chanzo chetu cha habari.
Sababu nyingine ni kwamba Serikali imeona kwamba nyumba hizo bado zinatakiwa kuendelea kubakia katika mikono ya serikali kwa sababu ziko katika maeneo yaliyotengwa na maalumu kwa ajili ya viongozi na watumishi wa Serikali.
Chanzo chetu cha habari kilisema kwamba tathmini ya nyumba hizo imeanza kufanywa na Wizara ya Miundombinu ambayo itawasilisha ripoti yake kwa Rais Kikwete kwa ajili ya utekelezaji.
Waziri wa Miundombinu, Basil Mramba hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kwa vile anafuatana na Waziri Mkuu Edward Lowassa katika ziara Mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Miundombinu Dk Makongoro Mahanga alipoulizwa hakukataa wala kukubali kuhusiana na suala hilo.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa nyumba za serikali zilizouzwa nchi nzima tangu mwaka 2002 ni 6,000.
Mauzo ya nyumba hizo yalikuwa yakifanywa kwa awamu na Wakala wa Nyumba za Serikali chini ya Ofisa Mkuu Mtendaji wake, Togolai Kimweri.
Serikali ya awamu ya Tatu ilisema wakati huo ya kuwa fedha zilizopatikana zingetumika kujengea nyumba nyingine kwa ajili ya watumishi wa serikali katika maeneo mbali mbali kama Dar es Salaaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Baadhi ya nyumba hizo zimekwisha kujengwa Dar es Salaam kwa ajili ya maofisa waandamazi wa Serikali wakiwamo Mawaziri.
Uchunguzi unaonyesha ya kuwa wakati Kikwete akidhamiria kuzirejesha nyumba hizo Serikalini, baadhi ya watumishi wa Serikali waliozinunua wamezifanyia ukarabati.
Wengine wamejenga nyuma nyingine ndani ya viwanja vya nyumba hizo ambavyo ni vikubwa, yaani low density
Vivyo vivyo wengine wamepangisha kwa makampuni binafsi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na nyingine zimejengwa maduka ya biashara na ofisi kwenye uzio wa nyumba hizo, hususan zilizopo karibu na barabara.
Uuzaji wa nyumba hizo za Serikali ulioanza mwaka 2002 ulisababisha malumbano na mzozo mkubwa miongoni mwa watanzania, wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, baadhi wakipinga kuuzwa kwake.
Baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya siasa walionyesha masikitiko yao kwa hatua ya kuuzwa nyumba hizo, hasa kwa bei ndogo, wakisema haikulingana na thamani na tathmini ya nyumba na viwanja vya nyumba hizo, kwa pamoja.
Wananchi pia walitaka uwepo uwazi wa majina ya watumishi waliouziwa nyumba hizo na bei waliyonunulia, jambo ambalo Serikali ilikataa kulitekeleza.
Serikali ya Awamu ya Tatu ilisisitiza kuziuza nyumba hizo, ikisema itakuwa ikijenga nyingine kutokana na malipo ya ununuzi wa nyumba hizo.
Miongoni mwa walionunua nyumba hizo ni mawaziri wengi, kama si wote, wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, hasa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma, kwa kuwa walikuwa wakiishi katika nyumba hizo.
Chanzo: Mtanzania Jumapili Toleo Namba 3784