Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Habari ,Mimi namuunga mkono mheshimiwa sendeka kwa kutaka kuleta hoja binafsi ya kurudisha nyumba za serikali. Nyumba ambazo waligawana kina Magufuli, Mkapa, ma swahiba zao na vimada wao. Naomba CCM na Chadema walivalie njuga hili swala na waweke itikadi za kichama pembeni.
 
Tunahitaji rais ambaye anaweza kuwa na uthubutu wa kutimiza hilo jukumu la kurudisha nyumba za walala hoi nafikiri katika wagombea wetu wa 2015 lazima tuwaandalie DO LIST na hilo jukumu liwemo hatuhitaji tena SERA kwani nimegundua ni sanaa tupu.
 
Chini ya serikali ya CCM nyumba kurudi ni sawa na mtoto aliyezaliwa kurudi tena tumboni mwa mama yake
 
Hata kama nyumba zilikuwa hoi serikali ingeweza kujenga nyumba mpya katika kiwanja hicho hicho. Mbona serikali hiyo hiyo ilitangaza kuwa inajenga nyumba mpya za wafanyikazi wake?
Kama unakubali walishindwa kuzikarabati utasemaje tena "hata kama nyumba zilikuwa hoi serikali ingeweza kujenga nyumba mpya..." Ni sawa na mtu yuko broke anakwambia nimeshindwa ku maintain gari langu zee zee naliuza, unamwambia basi pole, nunua jipya! Kama dai lao ni kwamba hawawezi kuzi manage financially hiyo ina include hawawezi kuzibomoa na kuzijenga upya!

Maintenance cost haikuwa kubwa ila wizi mkubwa ulikuwa unafanywa na watumishi wa serikali na wakandarasi. ...Serikali ilipaswa kutengeneza mkakati maalum wa kutengeneza nyumba hizo au kujenga mpya
Kama tatizo ni ufisadi wa watumishi wa serikali na makandarasi sasa hizo nyumba mpya zingejengwa na nani na kusimamiwa na watumishi wa wapi, serikali ya Zambia?

Mbona hamueleweki? Ushasema mfumo wa kuzi maintain ulikuwa una matatizo halafu solution yake ni kujenga nyingine, this is really absurd, I am sorry to say that, but I just can't comprehend this fuzzy stuff you are saying here.

Nyumba za serikali ziliuzwa kwa sababu ya shinikizo la IMF na wahisani (tena sio shinikizo, simple agizo, maana wao ndio mabwana zetu wanaotulisha). Walisema serikali haiwezi kuwa kwenye real estate service, hasa ukizingatia kwao waziri hapewi nyumba ya bure, gari, sijui posho ya mafuta, dereva etc. Kitu ambacho nakikubali 100%. Ok, so they sat down and haggled over how do you dispose of this litany of assets that you have? Wazo la kupigwa mnada halikupita, ikaonekana watakaonunua ni Rostam Aziz na Manji na waarabu wa Dowans, au type za Mengi na Chenge na Lowassa, wale wale.One example, Tanzania Breweries iliuza nyumba zake zilizoko prime areas and not surprisingly walionunua si raia, achilia mbali si wazawa. Hatuna robust immigration enforcement ya kujua nani raia nani kanunua passport. Ndo wakauziwa watumishi kwa sharti kwamba wasiziuze tena kwa miaka 100.

Another important dimension about the sale that is always overlooked relates to the scope of the exercise, the issue of "prime areas... expensive plots." It wasn't only the properties in Masaki na Oysterbay which were involved here. Rank and file government employees and the public at large have been buying NHC houses uswahilini zile za corridor katikati chumba huku na huku way before and after agizo la Mkapa, mtawanyang'anya hawa pia, na za msajili zilizouzwa? Watu wa hali ya chini na ya kawaida nao waliuziwa nyumba, mbona hizi haziongelewi? Tena za Nationa Housing za uswahilini, unlike za Masaki, hazikuuzwa na masharti, ndo maana wanunuzi wanaziuza upya, matajiri wanazibomolea mbali wanaendeleza business plans zao, residential areas za wazawa get gentrified, wazawa misplaced. Haya hayasemwi haya. Hata kidogo.

In any event, one problem plaguing this nation is lack of information due to decrepit media. Ndo maana mchakato mzima wa kuuza nyumba haujulikani. Nyumba ziliuzwa kwa mlolongo na maagizoya kimaandishi, lakini hakuna hata kiumbe kimoja kwenye press outlet za Tanzania mwenye balls za kwenda Ujenzi au kuwabana Ikulu kudai decision making records zina details gani, ilikuaje, hakuna.
 
Huyu Kristofa mie naona anababaisha watu! Hizi nyumba mbona hajauliza vikao vilivyopita? Asihamishe ajenda na mafikara ya watu! Twataka aongelee hoja mwashasha kama vile: Utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Richmondi, issue ya Jairo nakadhalika.
 
kwa haya mawazo yako natamani ningekuona unavyofanana!!! nini magofu? kiwanja kitupu maeneo ya agha khan pale ni bei gani? mi kuna mshkaji wangu pale wamenunua nyumba mil 15. we nini bwana? tunaongelea nyumba zilizojengwa na watanzania wote na kuuziwa wafanyakazi pekeyao, why? unasahau gharama za kuwapangishia m awaziri na viongozi wengine wa serikali nyumba?
 
Sendeka akusudia kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuitaka serikali irudishe nyumba zote ilizowauziwa watumishi wake na zile walizouziwa ndugu wa vigogo ambao siyo watumishi wa serikali.

Mbona heading na maelezo ya ndani tofauti? Kwa kifupi nyumba hizo lazima zirudi,2015 mgombea urais wa chadema ndio tutamwambia hicho ndio kiwe kipaumbele,lazima nyumba zirudi by hooks and crooks.
 
Hakuna mtu asiyefaa na haaminiki kama COS huyu mheshimiwa. Lakini kwa suala la nyumba za serikali ni kweli zinapaswa zirudi zote na hakuna compasation kwani waliiba mchana kweupe.
 
Ni kweli katika makosa yaliyotendeka hili limechukua nafasi zaidi, tatizo nani alishughulikie kwani waliopewa hizo nyumba wengi wao bado wapo serikalini. Sijui nani ataliweza hili!!
 
Hapo kazi ipo kwani Jk, Magufuli, Mkapa na wengine wamejitualia nyumba za serikali. Yetu macho, ila baada ya 2015 kwa kuwa Chadema itaongoza serikali nyumba hizo nina uhakika zitarudi.
 

Kweli sisi watanzania ni watu wa kusahau. Mbona hakuna jipya hapa! hivi na SENDEKA nae anajifanya amesahau kuwa mwaka 2008, aliyekuwa mbunge wa Vunjo. Mh. A. Kimaro alipeleka hija hii Bungeni. Nakumbuka hata hapa jamvini wadau walijadili kidogo kwenye hii thread https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...fsi-juu-ya-uuzwaji-wa-nyumba-za-serikali.html
kwani kipi kilitokea?! Kifupi ni kwamba mustakbali wa hizi nyumba unategemea regime change, kwan wafanya maamuzi wa sasa ndio hao hao waliofaidika na uuzwaji wa hizo nyumba.

AMKENI
 
Ole sendeka anapoteza tu muda wake. Si serikali ya CCM wala ya Chadema itakayoweza fanya hivyo. Serikali itaingia katika lawsuit ya muda mrefu sana na hata ikishinda, italipa gharama nyingi sana kwani hakuna mkataba unaosema thamani ya zile nyumba itabakia kama ile ya kuuza. Thamani ya sasa na ya soko. Hata hivyo serikali imeshajenga nyumba nyingi mpya na inazidi kujenga nyingine zaidi kama njia ya kuepuka fedheha hiyo.
 
Huyu Magufuli watu wanamfanya mungu au mtakatifu wakati alichemsha wizara ya ujenzi Nyumba ya Masaki market value Tshs. 500m mtu anauziwa Tshs. 3m na kwa mkopo. Watu waache kumsifia bure si ndo huyo huyo alichemka na samaki
umekosea unakarabatiwa kwa milioni kumi inauzwa kwa miliini tatu
 

Teh! I said this beast will always emerge! Sasa ona Sendeka kaja nalo, bado na Zungu yuko njiani.
Mwito Wangu kwa wabunge na waliotuibia hizi nyumba! They ought to sort it now kwa kuzitema.kinyume cha hapo ni kuendelea ku-defer hasira NA iko siku kitu mbaya itawatokea!
Wala sidhani ni mbali sana! We ngoja hiki kizazi cha "shule za kata" kianze kupiga kura - 2015 for the first time!
 
Mkuu kama Sendeka atajipanga vizuri watu wataumbuka na nyumba zitarudi mikononi mwa wananchi/serikali. Pamoja na uporaji huo ambao wengine wanaoonekana ni watakatifu walijiporea nyumba zaidi ya tano lakini pia wamekiuka vibaya mno masharti ya iporaji waliojiwekea. Sharti mojawapo ilikiwa ni kutobadili nyumba husika kabla ya kupita miaka 25! Lakini ndani ya miaka 10 nyumba karibu zote zimebadilishwa na kujengwa mahekalu. Mungu ni mkubwa sijui walijisahau vipi wakakaweka hako kakipengele!
 
sio za serikali tu kuna zile za TTCL nazo waligawana kama za kwao baada ya kuwatoa wafanyakazi wa ttcl kama wanyama...wamegawana bila huruma na kuuziana karibu ukoo mmoja nyumba zaidi ya moja..katibu mkuu kiongozi wa zamani (sasa balozi)ndio alijichukulia ile kubwa ya masaki...
 
kwakweli inasikitisha, sijui lengo la kuziuza lilikuwa ni lipi! kwa sasa watumishi wanaoajiriwa serikalini wanakosa pa kuishi wanabaki kurandaranda na mishahala yao ya TGS D isiyo na mashiko uswahilini kana kwamba kuajiriwa ni adhabu: hivi hao waliouza hizo nyumba walisahau msemo wa KATA MTI PANDA MTI?, swali langu bado liko palepale walipouza hizo pesa zilifanya nini?
 

Ila nyumba za serikali mkuu,ni hasara kwa Taifa!

Ili apate kuwa sauti ya wanyonge,ili aingie bungeni... Ilimlazimu agawe kanga,hata pilau,mi sioni tatizo kama anatimiza wajibu wake mkubwa kwa wapiga kura wake,na raia wa nchi hii kwa ujumla..

We fikiria Yule Shamsi Vuai Nahodha,na mawaziri wengine kadhaa,bado wanalala mahotelini,(tena ya malaki kwa siku,laki 4 hadi 5)ambapo ni gharama kubwa na ni matumizi mabaya ya kodi zetu....

Ama we mkuu unalitazama kwa mtazamo upi? kwamba kuwa na mbunge halali per se.. na kisha akawa mgonga meza,kuchukua posho,basi,watakaloamua ... Basi lipite tu... Faida gani hapo..
 

Kuuzwa kwa nyumba za serikali haikufatwa haki lakini na ni hasara kwa taifa lakini imesaidia kujiundia mashujaa wetu. Nafurahi ninopofika pale kwetu kuona DR. Shayo kajenga nyumba nne ndani ya ule uwanja ambapo alinunua nyumba ya serikali. Haki ya soko ingefuatwa, wala Shayo asingemudu kununua ile nyumba na badala yake Mhindi ama Mwarabu ndio angenunua. Fikiri.

Ila wanaudhi sana wale wenye nafasi ambao huchukua mali zetu kwa bei ndogo halafu wanaishia kuwauzia wahindi ama na wawekezaji feki - sasa joint venture vipi? Nasikia mgodi wa mkaa wa Chunya wa Mr. Mboma umeuzwa. Hawa wanaturudisha kwenye utumwa.
 
kama ni mpasuko hapa nyumba ndo itaanguka kabisa (ccm) na sizani kama hayo makundi yanayokinzana kama watakuwa tayari hili litokee iwe ni kundi la mafisadi au wapiganaji wa huo ufisadi,wasiwasi uliopo ni hoja kufika kwenye meza ya spika na kujadiliwa kwa kina na hii ni kutokana na asili ya bunge letu kwa kiasi kikubwa kuwa la kuiwakilisha serikali na sio wananchi,kwa sababu itakuwa ni kama kuwazalilisha vigogo wa serikali waliojiuzia hizi nyumba..hii hoja ni ya kuungwa mkono licha ya tofauti zao kiitikadi kwa maslahi ya umma na hapa ndipo tutakapoendelea kuwajua nature ya hawa wabunge wetu kama hili litafanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…