Kikwete abariki kura ya wazi

Kikwete abariki kura ya wazi

hatutaki mambo ya siri sir hapa,tunataka uwazi,anaye taka kufanya siri akafanye chumbani na mkeo

Hayo sio majibu wewe,muda mwngne utumie akili na sio kua -------- wa kuburuzwa tu na hisia za watu,unajua kwa nin waliweka kura za siri hata katika uteuzi wa rais,wabunge na diwani?usiweke akili matakon na kuja kuongea ili mradi uonekane,tunaiharibu nchi kwa upumbavu mdogo tu ambao na wewe unachangia
 
Mbona miaka yote ndio unayotumia? Inawezekana hata hujui kura ya siri ni nini unarudia tu kama kasuku.
hatutaki mambo ya siri sir hapa,tunataka uwazi,anaye taka kufanya siri akafanye chumbani na mkeo
 
Ndiyo maana tunataka maamuzi ya upatikanaji wa KATIBA MPYA uandaliwe na hili BUNGE maalumu la katiba, na siyo kundi lolote. Hivyo ni vema vyama ama makundi yoyote yasishinikize misimamo yao, ni vizuri wakubaliane kwa hoja za msingi katika mambo yote.

Kaka uko sahihi sana,nia yetu ni kuleta katiba nzuri na yenye manufaa kitanzania kwa kila aliechaguliwa kuwakilisha na sio kwenda kichama au mambo mengne,nadhan hata alieteua nae ana makosa na huo ndo ukwel
 
yeye si mbunge hivyo maoni hayo si msimamo wa wabunge binafsi. Halafu ifahamike kuwa wabunge wa bunge la muungano na wawakilishi wote ni wajumbe wa bunge la katiba wakiwa katika kundi moja na wa vyama vya upinzani kwa mujibu wa sheria. Wabunge tumieni nafasi yenu kisheria kutetea maoni ya wananchi na si misimamo ya vyama vyenu. Suala la kutumia kura ya siri au wazi liamuliwe kwa kupigiwa kura na wajumbe wote kama mlivyofanya katika kumchagua mwenyekiti wa muda. Ushauri wangu ni kwa wajumbe kutoka CCM kuwa jasiri bila kuyumbushwa na misimamo ya Chama kwani katiba ya maoni ya wananchi ikipitishwa basi itaruhusu mgombea binafsi hivyo hata kama utafukuzwa katika chama bado wananchi tunaweza kukurejesha Mjengoni.

Na imesemwa wale wabunge 90 wanaokisaliti watakiona Baada ya bunge hili kupita
 
CCM wanataka kura ya wazi lakini vikao vya kamati wanataka viwe siri!
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwenyekiti wa ccm taifa amewataka wajumbe wote wa bunge maalumu la katiba wanaotoka chama cha mapimduzi wasipige kura ya siri na yoyete atakaye unga mkono kura ya wazi atakuwa ameenda kinyume na matakwa ya chama

Ni kweli kabisa!!! Maana imeonekana jitihada za Pinda zimegonga mwamba....Mimi nasema unafiki na udhaifu wa mkuu wa kaya ndiyo unaipeleka nchi pabaya...

Kama alikuwa hataki Katiba mpya kwanini aliruhusu mchakato wa Katiba? Tume ya Warioba imetumia billions of shillings kukusanya maoni, leo CCM wanataka kuturudisha nyuma..

CCM na ilaniwe...
 
wiki nyingine hiyo inakuja tena, issue itakuwa ni wazi ama siri mpaka wiki iishe.

Ili kupata muafaka lazima kuwe na upande ulegeze, vinginevyo hatuwezi kusonga mbele.

Wala haitakua hivyo vile vifungu vinavyobishaniwa vitaachwa uchaguzi wa Mwenyekiti uanze na Baadae viapo kisha vitaamuliwa Baadae kuokoa muda
 
Kura ya Bunge la Katiba si haki ya Mjumbe mwenyewe ni haki ya Kundi au Genge unalowakilisha. Kama wewe ni Mwakilishi wa NGO lazima NGO husika ijiridhishe kama umetekeleza ulichotumwa na Taasisi yako? Mwakilishi wa Walemavu yuko pale kuwakilisha mawazo ya walemavu sio yake binafsi, walemavu wanahaki ya kujua aina ya kura aliyopiga mwakilishi wao kuepuka kununuliwa au kuuzwa kura yao. Kura ya Siri ina harufu ya wizi au vishiria vya Rushwa.
 
Kuanzia kesho tutaweza kulibaini jambo hili. Kama ni kweli tutaomba hii iwe ni katiba ya chama na siyo ya nchi/Taifa.
 
yeye mwenyewe alichaguliwa na kura za wazi ?


Kwani nyie kura za wazi zinawapunguzia nini?

Mmeanza kuogopa nini? si mlisema 75% ya rasimu ni matakwa yenu? sasa Leo mnaogopa kura ya wazi kwanini wakati nyie mnajiita makamanda?
 
wamalize hii hoja ya kura na vifungu vingine vyenye mvutano muda unaenda,ni wakati wa kuachana na ukameruni na kujadili mambo ya msingi
 
Ametamka wapi, lini na saa ngapi? Habari haijakamilika

Wewe hupendi katiba iliyotengenezwa na Chama cha Mapinduzi au wewe siyo muumini wa Serikali tatu??
Kura ya wazi ni yenyewe tuwajue kina Sendekazz
 
Hakika CCM wanakotaka kulipeleka hili Taifa ni kubaya sana... Tunaelekea kugawana mbao!!!
 
Unafiki ndiyo umewajaa CCM... Msikilize MHE. RAZA hapa alichowahi kukisema... Nini kinamfanya afunge mdomo wake?

[video]http://mzalendo.net/habari/video/video-mwishowe-hata-cheti-cha-ndoa-kitatoka-dodoma.html#comments[/video]
 
Unafiki ni kitu kibaya sana duniani na mbinguni. machoni anajifanya anataka Nchi ipate katiba nzuri, huku kiuhalisia anataka katiba ileile ya 1977 irudi.Ni bora mchawi kuliko mnafikhi
 
Back
Top Bottom