Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mtangazaji: Watanzania wangetamani kusikia kutoka kwenye kinywa chako, nini ambacho kilitokea mwaka 2015? Matarajio ya wengi yalikuwa Benard Membe na Edward Lowassa, mmoja rafiki yako, mmoja ndugu yako ukiwaandaa wote kuwa marais lakini matokeo yakaja tofauti kabisa ambayo wengi hawakutarajia.
Kikwete: Kwanza niseme, Membe sio ndugu yangu(Kicheko), hatuna undugu kabisa, Membe Mmwera mie Mkwere, hakuna undugu mengine maneno ya siasa, nimeshangaa kweli.
Membe nimekuja kumfahamu baadae sana maishani.
Mchakato ule tumeufanya kuwa ni mchakato open, sisi 95 tulikuwa wagombea 17, 2005 tulikuwa wagombea 11, 2015 kulikuwa na wagombea 42.
Kwa utaratibu ambao CCM tumeweka hatuwezi kupeleka wote 42. Kazi ya kamati kuu ni kufanya shortlist ya watu watano, tukafanya shortlist ya watu watano, wanaume 3 na wanawake 2.
Tukawa na mjadala mkubwa sana kwanza kwenye kamati ya maadili, tunaangalia mambo mengi, afya zao, tabia, makandokando, vitu vingi hatimae tukaja na orodha ya watu watano.
Tulivyokwenda kwenye kamati kuu ikawa na mjadala mkubwa sana, kwanini huyu mmemuacha.
Wakati huo wanasema Magufuli hajawahi kuwa kiongozi yoyote kwenye chama hiki hata kuwa balozi atakuwa mwenyekiti wa chama.
Kikwete anasema walizingumza mpaka wakaona bora wapige kura na yakaja yale majina matatu yakaenda.
Mtangazaji: Wakasema umekuja nayo mfukoni!
Kikwete: Ndio inavyokuwa, orodha ya watu watano niliidraw mimi, mimi ndio mwenyekiti, mkutano ni lazima uuongoze. Unasema mimi kwa maoni yangu watano hawa. Tunafika mahali tunakubaliana, lile libaraza la wazee halina kazi nyingine zaidi ya kipindi cha transition.