Kikwete afunguka yaliyojiri CCM mpaka Hayati Magufuli akapeperusha bendera ya CCM

Kikwete afunguka yaliyojiri CCM mpaka Hayati Magufuli akapeperusha bendera ya CCM

Yule jiwe nao mlipipitia file la afya yake??
Swali zuri sana
thinkstupid.png
 
Mzee Kikwete alitukosea sana kwa kutuletea Chizi mwenye matatizo ya Moyo.
Anyway... mimi binafsi nimeshamsamehe Mzee wetu Jakaya Kikwete.
Kama chadema walivyotukosea kutuletea zezeta tundu lisu 2020 ambaye #dishlimetilt wazi wazi.
Mimi sijamsamehe mbowe, hawezi kutudharau mara mbili mfululizo. 2015 akatuletea fisadi lowassa, 2020 akatuletea chizi lisu.
 
Waliangalia afya na wakajua kabisa kuwa jamaa moyo wake unaitilafu katika mfumo wa umeme na wakapitisha hivyo hivyo cha ajabu yule waliokuwa wanamuita mgonjwa mpaka leo yupo hai.
Nadhani hili la afya kaliingiza kwenye sifa walizotazama kwa lengo la kumwondoa Mwandosya.

Sijui bahati iliyokuwaje CCM haikufa chini ya Kikwete.

Matakataka yote yanayoonekana ndani ya chama hicho yalishamiri sana wakati wa Kikwete. Nilitabiri kwamba huo ndio ungekuwa mwisho wa CCM kama tulivyoijua tokea huko nyuma, na ikawa kweli.
 
Wewe uliona wapi Zezeta anapigwa risasi we uliona wapi?
Risasi anaweza kupigwa yeyote kutegemeana na nini kinasababisha apigwe. Kichaa akiingia nyumbani mwako akaanza kukaba koo watoto wako utamwacha eti kwa sababu ni chizi?
 
Mtangazaji: Watanzania wangetamani kusikia kutoka kwenye kinywa chako, nini ambacho kilitokea mwaka 2015? Matarajio ya wengi yalikuwa Benard Membe na Edward Lowassa, mmoja rafiki yako, mmoja ndugu yako ukiwaandaa wote kuwa marais lakini matokeo yakaja tofauti kabisa ambayo wengi hawakutarajia.

Kikwete: Kwanza niseme, Membe sio ndugu yangu(Kicheko), hatuna undugu kabisa, Membe Mmwera mie Mkwere, hakuna undugu mengine maneno ya siasa, nimeshangaa kweli.

Membe nimekuja kumfahamu baadae sana maishani.

Mchakato ule tumeufanya kuwa ni mchakato open, sisi 95 tulikuwa wagombea 17, 2005 tulikuwa wagombea 11, 2015 kulikuwa na wagombea 42.

Kwa utaratibu ambao CCM tumeweka hatuwezi kupeleka wote 42. Kazi ya kamati kuu ni kufanya shortlist ya watu watano, tukafanya shortlist ya watu watano, wanaume 3 na wanawake 2.

Tukawa na mjadala mkubwa sana kwanza kwenye kamati ya maadili, tunaangalia mambo mengi, afya zao, tabia, makandokando, vitu vingi hatimae tukaja na orodha ya watu watano.

Tulivyokwenda kwenye kamati kuu ikawa na mjadala mkubwa sana, kwanini huyu mmemuacha.

Wakati huo wanasema Magufuli hajawahi kuwa kiongozi yoyote kwenye chama hiki hata kuwa balozi atakuwa mwenyekiti wa chama.

Kikwete anasema walizingumza mpaka wakaona bora wapige kura na yakaja yale majina matatu yakaenda.

Mtangazaji: Wakasema umekuja nayo mfukoni!

Kikwete: Ndio inavyokuwa, orodha ya watu watano niliidraw mimi, mimi ndio mwenyekiti, mkutano ni lazima uuongoze. Unasema mimi kwa maoni yangu watano hawa. Tunafika mahali tunakubaliana, lile libaraza la wazee halina kazi nyingine zaidi ya kipindi cha transition.
Nimeipenda hii, kuna kitu hapa JK hakukisema, kitu kinachoitwa , "the inner core" JPM aliisha chaguliwa kabla ya 2014 na iliamuliwa lazima awe JPM kwasababu fulani ya ajabu!. Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
P
 
Kikwete anasema walizingumza mpaka wakaona bora wapige kura na yakaja yale majina matatu yakaenda.

Mtangazaji: Wakasema umekuja nayo mfukoni!

Kikwete: Ndio inavyokuwa, orodha ya watu watano niliidraw mimi, mimi ndio mwenyekiti, mkutano ni lazima uuongoze. Unasema mimi kwa maoni yangu watano hawa. Tunafika mahali tunakubaliana, lile libaraza la wazee halina kazi nyingine zaidi ya kipindi cha transition.
 
Turudi nyuma. Nyerere alikuwa idealist na hakuwa na action? Are you kidding me? Unajua mpaka sasa hivi Nyerere ndiye rais bora kuliko marais wote ambao tumekuwa nao Tanzania? Unajua extent ambayo Kikwete ameharibu nchi yetu? Unaona jinsi viongozi wengi wabovu na vilaza walivyoweza kujipenyeza kwenye system na kuwaondoa tena itakuwa ni kazi kubwa? Mtanlaumu Samia, mtamlaumu Magufuli ila Tanzania imeanza kwenda kombo pale Kikwete alipopata urais wa kununua kwa fedha. Au pengine sahihi zaidi tumlaumu Mkapa kwa kutoweza kudhibiti waliotumia fedha kupata urais. Ilatakiwa afanye kama Kikwete alivyofanya kwa Lowassa.
Ukiijua historia ya Tanzania, hautashangaa nilichokisema. Ni kutokana na utawala wa Nyerere, ndipo hapo nchi ilipopoteza muelekeo kwa kuwa na kiongozi aliyekuwa idealist zaidi. 1. Ni miongoni wa marais waliopinga Africa kuwa Union na rais mmoja. Alipendekeza tuanze na regional setting kama EAC ambayo alikuja changia kuiua mwenyewe. 2. Alifuta vyama vya upinzani. 3 Alifuta Uchifu (Utawala/uongozi wa asili). 4. Akafuta cooperative unions zilzokuwa zinafanya vizuri sana. 5. Akaanzisha azimio la Arusha ambalo halikuwa realistic. mwenyewe likamshinda. 6. Akataifisha mali. Uchumi ukafa. 7. kaanzisha vijiji vya ujamaa, maduka ya ushirika. 8. Akaleta madaraka mikoani. 9. Akaanzisha vyama vya ushirika vyake bila kufuata misingi ya ushirika. Meneja anatoka songea kwenda kuendesha chama Bukoba. Ikamshinda pia. 10. Vita ya uganda, 11. Kusaidia ukombozi wa Africa kwa ukombozi wa Africa kwa gharama ya watanzania. Matokeo yake nci zilipopata uhuru wala hazija reciprocate. Bila viza kwa watanzaniaSouth africa ni juzi tu. 12. Alijua ubovu wa katiba but hakuirekebisha. 13. Aliitengeneza CCM na mfumo wa kuongoza nchi ambao ndo matokeo ya leo. nk nk nk nk. Soma na kuielewa historia tuje kuongea
 
Back
Top Bottom