Kikwete afunguka yaliyojiri CCM mpaka Hayati Magufuli akapeperusha bendera ya CCM

Kikwete afunguka yaliyojiri CCM mpaka Hayati Magufuli akapeperusha bendera ya CCM

Mzee Kikwete alitukosea sana kwa kutuletea Chizi mwenye matatizo ya Moyo.

Bora Membe kuliko Mtu aliyestahili kufungiwa Milembe na ufunguo kutupwa kwenye Volcano ya Oldonyo leNgai.

Anyway... mimi binafsi nimeshamsamehe Mzee wetu Jakaya Kikwete.
Magufuli alikuwa miongoni mwa mawaziri waliokuwa na sifa nzuri sana enzi zake
 
Magufuli alikuwa miongoni mwa mawaziri waliokuwa na sifa nzuri sana enzi zake
Nenda ukazione Barabara zote alizozisimamia ni mabonde matupu.
Mfano hiyo Balabala ya Tabora Kigwa hadi Itigi na Balabala ya Tabora Puge hadi Nzega

Barabara ya Chato hadi Bwanga na Katoro mashimo na viraka.

Barabara ya kutoka Maswa hadi Lamadi utasema uko kwenye mtumbwi.
 
Nadhani Salim angekuwa rais bora na ambaye angefuata angekuwa bora. Tusingeingia kwenye hii visual circle ya sasa. Tulikubali kushusha standard za urais kwa kumpa Kikwete hivyo circle imeendelea na kujitoa hapo itakuwa kazi kubwa.
Hakuna aisee, yule naye ni mlolongo wa idealists kama Nyerere, lakini action kidogo sana. But, hivi kweli hata huo mchujo, JK akaona ile list ya wale watano was the best? kweli?
 
Hakuna aisee, yule naye ni mlolongo wa idealists kama Nyerere, lakini action kidogo sana. But, hivi kweli hata huo mchujo, JK akaona ile list ya wale watano was the best? kweli?
Turudi nyuma. Nyerere alikuwa idealist na hakuwa na action? Are you kidding me? Unajua mpaka sasa hivi Nyerere ndiye rais bora kuliko marais wote ambao tumekuwa nao Tanzania? Unajua extent ambayo Kikwete ameharibu nchi yetu? Unaona jinsi viongozi wengi wabovu na vilaza walivyoweza kujipenyeza kwenye system na kuwaondoa tena itakuwa ni kazi kubwa? Mtanlaumu Samia, mtamlaumu Magufuli ila Tanzania imeanza kwenda kombo pale Kikwete alipopata urais wa kununua kwa fedha. Au pengine sahihi zaidi tumlaumu Mkapa kwa kutoweza kudhibiti waliotumia fedha kupata urais. Ilatakiwa afanye kama Kikwete alivyofanya kwa Lowassa.
 
Mzee anakazia kuwa kipindi cha transition huwa ni cha wazee!!

Maana yake ni kwamba;-

Hata sasa tupo kwenye transition hivyo wazee wanakisimamia vema kipindi hiki tena Sana!!

Mzee amekuwa active Sana kulikoni!?

Kuna nini huko!?

Lowasa hajambo!?na siku nyingi sijamsikia kabisaa!!
 
Unaweza kuwa hai ila huna uwezo wa kuongoza mzee baba. Magufuli amekufa kwa magonjwa ambayo wengi tunatembea nayo. Changamoto ya Lowassa ni kwamba ugonjwa wake unapelekea hata kumbukumbu kuondoka hivyo tungemuweka kando tu kwa namna yoyote ingali yuko hai.
Kwani ule ugonjwa wa Magufuli ulikuwa ni shida kubwa. Kuna watu wengi tu wana hitilafu aliyokuwa nayo na wanaishi maisha ya kawaida. Ni kwa vile alikuwa mbishi na akaacha kuchukuwa tahadhari kwenye korona ikampata kwa kirahisi. Alitakiwa ajihadhari na chanjo zikianza kutumika achome mara moja.
 
Mtangazaji: Watanzania wangetamani kusikia kutoka kwenye kinywa chako, nini ambacho kilitokea mwaka 2015? Matarajio ya wengi yalikuwa Benard Membe na Edward Lowassa, mmoja rafiki yako, mmoja ndugu yako ukiwaandaa wote kuwa marais lakini matokeo yakaja tofauti kabisa ambayo wengi hawakutarajia.

Kikwete: Kwanza niseme, Membe sio ndugu yangu(Kicheko), hatuna undugu kabisa, Membe Mmwera mie Mkwere, hakuna undugu mengine maneno ya siasa, nimeshangaa kweli.

Membe nimekuja kumfahamu baadae sana maishani.

Mchakato ule tumeufanya kuwa ni mchakato open, sisi 95 tulikuwa wagombea 17, 2005 tulikuwa wagombea 11, 2015 kulikuwa na wagombea 42.

Kwa utaratibu ambao CCM tumeweka hatuwezi kupeleka wote 42. Kazi ya kamati kuu ni kufanya shortlist ya watu watano, tukafanya shortlist ya watu watano, wanaume 3 na wanawake 2.

Tukawa na mjadala mkubwa sana kwanza kwenye kamati ya maadili, tunaangalia mambo mengi, afya zao, tabia, makandokando, vitu vingi hatimae tukaja na orodha ya watu watano.

Tulivyokwenda kwenye kamati kuu ikawa na mjadala mkubwa sana, kwanini huyu mmemuacha.

Wakati huo wanasema Magufuli hajawahi kuwa kiongozi yoyote kwenye chama hiki hata kuwa balozi atakuwa mwenyekiti wa chama.

Kikwete anasema walizingumza mpaka wakaona bora wapige kura na yakaja yale majina matatu yakaenda.

Mtangazaji: Wakasema umekuja nayo mfukoni!

Kikwete: Ndio inavyokuwa, orodha ya watu watano niliidraw mimi, mimi ndio mwenyekiti, mkutano ni lazima uuongoze. Unasema mimi kwa maoni yangu watano hawa. Tunafika mahali tunakubaliana, lile libaraza la wazee halina kazi nyingine zaidi ya kipindi cha transition.
“I’m not really supposed to say that but it’s obvious fact. And you know, when stupid people vote, you know who they nominate? Other stupid people.”

The “very low-quality people that vote in their primaries” are “producing predictably very low-quality candidates,” Carville said. “It’s evident right in front of you.”

this very much applies here in Tz. 95% are very low quality people
 
Kikwete yuko sahihi sana

Anachojaribu kuongea kuwa kama unajipanga kuja kushika post kubwa kama Uraisi ,uspika wa bunge au ujuaji mkuu anza mapema kutojihusisha na makandokando mazito

Lowasa na Membe walikuwa na makando kando mazito mno post walizofikia walitakiwa kuachana na makandokando mazito mapema .Ni somo kwa yeyote anayetaka post kubwa za juu mihimili yote mbeleni kama wanautaka Uraisi,uspika au ujaji mkuu.Wawahi ku clean their CV plates many years before!!
 
Mtangazaji: Watanzania wangetamani kusikia kutoka kwenye kinywa chako, nini ambacho kilitokea mwaka 2015? Matarajio ya wengi yalikuwa Benard Membe na Edward Lowassa, mmoja rafiki yako, mmoja ndugu yako ukiwaandaa wote kuwa marais lakini matokeo yakaja tofauti kabisa ambayo wengi hawakutarajia.

Kikwete: Kwanza niseme, Membe sio ndugu yangu(Kicheko), hatuna undugu kabisa, Membe Mmwera mie Mkwere, hakuna undugu mengine maneno ya siasa, nimeshangaa kweli.

Membe nimekuja kumfahamu baadae sana maishani.

Mchakato ule tumeufanya kuwa ni mchakato open, sisi 95 tulikuwa wagombea 17, 2005 tulikuwa wagombea 11, 2015 kulikuwa na wagombea 42.

Kwa utaratibu ambao CCM tumeweka hatuwezi kupeleka wote 42. Kazi ya kamati kuu ni kufanya shortlist ya watu watano, tukafanya shortlist ya watu watano, wanaume 3 na wanawake 2.

Tukawa na mjadala mkubwa sana kwanza kwenye kamati ya maadili, tunaangalia mambo mengi, afya zao, tabia, makandokando, vitu vingi hatimae tukaja na orodha ya watu watano.

Tulivyokwenda kwenye kamati kuu ikawa na mjadala mkubwa sana, kwanini huyu mmemuacha.

Wakati huo wanasema Magufuli hajawahi kuwa kiongozi yoyote kwenye chama hiki hata kuwa balozi atakuwa mwenyekiti wa chama.

Kikwete anasema walizingumza mpaka wakaona bora wapige kura na yakaja yale majina matatu yakaenda.

Mtangazaji: Wakasema umekuja nayo mfukoni!

Kikwete: Ndio inavyokuwa, orodha ya watu watano niliidraw mimi, mimi ndio mwenyekiti, mkutano ni lazima uuongoze. Unasema mimi kwa maoni yangu watano hawa. Tunafika mahali tunakubaliana, lile libaraza la wazee halina kazi nyingine zaidi ya kipindi cha transition.
Kwahyo kumbe kweli alikuja na majina yake mfukoni

Long live mzee JK huna makuu.
 
Alisifuye jua limemwangaza Nina hakoka kuna watu wenye ufahamu watakaona uzuri ktk ubaya unaosemwa juu ya mwendazake
Kama alikuwa kichaa basi alitufaa sana na hatutomsahau.
 
Alikuwa akijiona kuwa yeye ni bora kuliko Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete

Hata busara alikuwa hana.

what.png

Hafai ndio maana Yarabi alitunusuru.
 
Mwandishi angemuuliza nini kilitokea kwa Gas yetu mtwara hadi wakafanya udhulumati mkubwa sana kwa wa Tz kupitia wabunge wa ccm.
Swali la gesi hata asipoulizwa dunian lakin kwa alichotufanyia huyu mzee mtanashati ataulizwa tu huko purgatory. Ili akifeli utetez ashushwe kwenye tanuru vizuri
 
Swali la gesi hata asipoulizwa dunian lakin kwa alichotufanyia huyu mzee mtanashati ataulizwa tu huko purgatory. Ili akifeli utetez ashushwe kwenye tanuru vizuri
Hilo la gas halisemwagi kabisa ikifikia hapo anaibuliwa mwendazake ili hilo lisisemwe.
 
Hilo la gas halisemwagi kabisa ikifikia hapo anaibuliwa mwendazake ili hilo lisisemwe.
Baada ya kuwajua wazungu vizuri nimekubali tunahitaji mfumo wetu wa kutawalana hata kama ni modified democracy. Democracy ni silaha mbaya sana pale inapotumiwa kuharibiana.
Nimeshajiridhisha hakuna namna rais wa Africa anaweza kubaki kwenye nafas hiyo hapo hapo akiwa tishio kwa wazungu.
Hii dunia, waafrica tunafanya fair play wakati kuna majamaa huko wanacheza na visu na viwembe mfukoni.
 
Back
Top Bottom