Kikwete afunguka yaliyojiri CCM mpaka Hayati Magufuli akapeperusha bendera ya CCM

Kikwete afunguka yaliyojiri CCM mpaka Hayati Magufuli akapeperusha bendera ya CCM

Mzee Kikwete alitukosea sana kwa kutuletea Chizi mwenye matatizo ya Moyo.

Bora Membe kuliko Mtu aliyestahili kufungiwa Milembe na ufunguo kutupwa kwenye Volcano ya Oldonyo leNgai.

Anyway mimi binafsi nimeshamsamehe Mzee wetu Jakaya Kikwete.
Acha upuuzi wako!
 
Salim angeturudisha kwenye Ujamaa wa Kiafrika uliofeli.
Mimi ni mmoja wa watu niliompinga sana Salim.
Nadhani Salim angekuwa rais bora na ambaye angefuata angekuwa bora. Tusingeingia kwenye hii visual circle ya sasa. Tulikubali kushusha standard za urais kwa kumpa Kikwete hivyo circle imeendelea na kujitoa hapo itakuwa kazi kubwa.
 
Hajawahi kutukanwa wala kudhalilishwa, upinzani ulikuwa unafanya kazi yake inavyotakiwa upinzani ufanye
Halafu demokrasia nchi hii sio hisani ya Rais, ni haki yetu ya msingi wananchi. Tusijiweke dhalili mbele ya watawala.
Raisi aliyeruhusu Demokrasia istawi na Uchumi matokeo yake tukawa tunamtukana na kumdhalilisha.

Mimi sikuwahi hata siku moja kumsema vibaya huyu Mzee wangu.

Mungu ampe maisha marefu na siha njema
 
Mtangazaji: Watanzania wangetamani kusikia kutoka kwenye kinywa chako, nini ambacho kilitokea mwaka 2015? Matarajio ya wengi yalikuwa Benard Membe na Edward Lowassa, mmoja rafiki yako, mmoja ndugu yako ukiwaandaa wote kuwa marais lakini matokeo yakaja tofauti kabisa ambayo wengi hawakutarajia.

Kikwete: Kwanza niseme, Membe sio ndugu yangu(Kicheko), hatuna undugu kabisa, Membe Mmwera mie Mkwere, hakuna undugu mengine maneno ya siasa, nimeshangaa kweli.

Membe nimekuja kumfahamu baadae sana maishani.

Mchakato ule tumeufanya kuwa ni mchakato open, sisi 95 tulikuwa wagombea 17, 2005 tulikuwa wagombea 11, 2015 kulikuwa na wagombea 42.

Kwa utaratibu ambao CCM tumeweka hatuwezi kupeleka wote 42. Kazi ya kamati kuu ni kufanya shortlist ya watu watano, tukafanya shortlist ya watu watano, wanaume 3 na wanawake 2.

Tukawa na mjadala mkubwa sana kwanza kwenye kamati ya maadili, tunaangalia mambo mengi, afya zao, tabia, makandokando, vitu vingi hatimae tukaja na orodha ya watu watano.

Tulivyokwenda kwenye kamati kuu ikawa na mjadala mkubwa sana, kwanini huyu mmemuacha.

Wakati huo wanasema Magufuli hajawahi kuwa kiongozi yoyote kwenye chama hiki hata kuwa balozi atakuwa mwenyekiti wa chama.

Kikwete anasema walizingumza mpaka wakaona bora wapige kura na yakaja yale majina matatu yakaenda.

Mtangazaji: Wakasema umekuja nayo mfukoni!

Kikwete: Ndio inavyokuwa, orodha ya watu watano niliidraw mimi, mimi ndio mwenyekiti, mkutano ni lazima uuongoze. Unasema mimi kwa maoni yangu watano hawa. Tunafika mahali tunakubaliana, lile libaraza la wazee halina kazi nyingine zaidi ya kipindi cha transition.
Ukitaka kujuwa ubovu wa CCM ulipofikia, basi soma kwa makini haya yanayoelezwa na huyu Kikwete humu.

Ni drasa zuri sana la kujuwa jinsi chama hicho kilivyo poteza dira nyakati hizi.
 
Hawa walafi wakishafakamia hela za umma wanajisahu sana! Wakaangalia afya zao na hawakung'amua kuwa yule katili atarudisha chenji mapema. Wakaangalia makandokando na hawakukumbuka alivyojiuzia nyumba za umma, hawakukumbuka alivyowatishia kwa bunduki wahariri wa gazeti la Rai kipindi akiwa waziri! Hawa viumbe hawajielewi.
 
Yule jamaa alikuwa unfit kiafya ya akili na kimwili.
Hata magoti alikuwa hajui kupiga.

View attachment 2379626
Hapa kwenye hii picha likuwa anajua fika kuwa keshapanga wizi wa kura halafu anajifanya kupiga magoti akiwa na chawa wake.

Wala haikua laghai bali ni uchizi tu.
Naona bado unauguli jinsi Magufuli alivyokubutua akakuachia kovu!
 
Waliangalia afya na wakajua kabisa kuwa jamaa moyo wake unaitilafu katika mfumo wa umeme na wakapitisha hivyo hivyo cha ajabu yule waliokuwa wanamuita mgonjwa mpaka leo yupo hai.
Unaweza kuwa hai ila huna uwezo wa kuongoza mzee baba. Magufuli amekufa kwa magonjwa ambayo wengi tunatembea nayo. Changamoto ya Lowassa ni kwamba ugonjwa wake unapelekea hata kumbukumbu kuondoka hivyo tungemuweka kando tu kwa namna yoyote ingali yuko hai.
 
Yule jiwe nao mlipipitia file la afya yake??
 
kikwapi sasa, sema tu ulikusudia lowassa asipate nafasi, chuki zako binafsi, wewe na samwel sita. Na Mungu kakuacha ili uone John afya imemuondoa, samweli afya imemwondoa. Mzee hila na fitina sana na ubinafsi, uswahili
 
Back
Top Bottom