Kikwete amteua Batilda Salha Burian kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan

Kikwete amteua Batilda Salha Burian kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan

Ngoja aendo huko japan kwa miezi minane iliyobaki kwa maana UKAWA wakiingia basi kila nafasi hizi za kujuana kitafumuliwa ; pawepo na ku-apply siyo mtu huyo huyo Mkuu wa mkoa, Mbunge mara Diwani or Balozi???
 
Kama kawaida yake jk yeye hachagui viongozi kwa uwezo wao yeye anawachagua ilimradi kujuana na kupeana ulaji, balozi mzigo kachaguliwa
 
Sasa mbona jembe limepelekwa mbali na Arusha tena? Manake kimkakati Nairobi ilikuwa karibu, mtu kwa gari tu anakuja weekend kuzungukia jimbo tarajali. Au ndo kusema walishakata tamaa na jimbo la Arusha?

Sio yeye tu, chama chote kimeshakata tamaa na Arusha! Matumaini pekee ni jimbo la Le Mutuz
 
Hongera sana Batilda...Jitahidi Upate Mtoto huko ili awe Raia wa Japan kwa mujibu wa sharia ... Bongo hakuna dili zaidi ya matusi na majungu ... CCM nayo ndo ishajifia kiaina ...
 
batilda-2.jpg


Dah! Ana mdomo mzuri huyu! Hadi machale ya dauni yamenicheza kudadeki walahi walasuli!
 
Wakuu hivi Captain masawe aliekuwa mkuu wa mkoa wa kagera yupo wapiii au kastaafu naee maana toka kawekwa kipoloo simuoni
 
Sasa mbona jembe limepelekwa mbali na Arusha tena? Manake kimkakati Nairobi ilikuwa karibu, mtu kwa gari tu anakuja weekend kuzungukia jimbo tarajali. Au ndo kusema walishakata tamaa na jimbo la Arusha?

Walishajikatiaga tamaaa zamani saaana
Wameona hesabu zinagomaa
 
Rais Kikwete amemteua Batilda Salha Burian kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Japan kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini humo Bi. Salome Sijaona ambaye amestaafu. Vilevile Rais Kikwete amemteua Bw. John Michael Haule kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya kuchukua nafasi ya Batilda. Kabla ya uteuzi huu Bw. John Haule alikuwa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

Hivi wanajamvi hii speed ya kuteua wtu mwishoni mwishoni hivi huyu jamaa mbona imezidi saana mpaka anatutishaaa
 
Kutoka KATIBU MKUU Wizara Mambo ya nje hadi kuwa Balozi Kenya?

Huyu Mzee Haule John likely KAHARIBU sehemu hapo wanamshikiza tu hadi astaafu!Ningekuwa mm ningekataa na ningejizuru
 
Actually kamhamisha toka kuwa balozi wetu nchini Kenya kwenda Japan. Labda anataka akakae mbali na yule jamaa aliye waumbua wakati wa BMK (ex-Chief Justice wa Zanzibar)

Aaaah! kuna neno umelizima hapa! Hebu eleza kidogo tuone matatizo yao hawa viumbe wanaojiita serikali bhana!
 
Japan ni nchi tajiri na iliyoendelea sijui sera zetu zikoje katika kujifunza ili kujikwamua toka kwenye hili tope jeusi!!! watu makini na wenye akili saana wanatakiwa kwenye hizi balozi, Tanzania ni nchi masikini saana ambayo inahitaji kupata uzoefu hapa ambao ni zaidi ya mahusiano,,, MBONA AKINA MAMA WENGI KWENYE HIZI NAFASI ZA KUTEULIWA NI WALE WENYE MVUTO KISURA NA MAUMBILE???
 
Kutoka katibu mkuu wa wizara mpaka balozi,nje ya nchi,dah!!

Mimi mwenyewe hapo ndiyo nashangaa sana, huyu jamaa wamemdemote mbaya bora hata wangemdemotia USA sasa wanampeleka hapo kwa Wakikuyu
 
Hivi wanajamvi hii speed ya kuteua wtu mwishoni mwishoni hivi huyu jamaa mbona imezidi saana mpaka anatutishaaa

Mpaka akishabadilisha wakuu wa wilaya ndiyo itakuwa mwisho wa uteuzi wake
 
Back
Top Bottom