Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki

Hongera zao wakatoliki kwa hilo suala la maendeleo, lakini chondechonde Kikwete, hizo ahadi unazoahidi kila uchao, watu wanaandika umesema ajira 8,000 ingawa hujafafanua, zisije kukutokea puan i siku moja. Lakini mbunge wa huko jasiri kumwambia leo huko ndiyo wanapata uhuru, kwahiyo miaka 50 ya uhuru huko haipo, safi sana kuwa mwazi.
 
Kimsingi waislamu hawana cha kumfanya raisi aje akifungue.......... wao kila kukicha kodi zinaibwa na wakristu lakini hakuna anayekwenda mahakamani kuwashitaki hao wakristu kwa wizi wanaousema........ WAMECHUKULIWA KIWANJA PALE KIBASILA (MCHICHA) WAPO KIMYAAA MPAKA SASA.......... Na kwa jinsi wanavyopeleka mambo yao hovyo USISHANGAE UPANUZI WA BARABARA NYINGI UNAHUSISHA UBOMOAJI WA MISIKITI.... They dont plan ujenzi .... they dont see next 20 years kama hapo wanapojenga patapita barabara e.g msikiti wa mtoni mtongani........
 
Hongera Kanisa Katoliki lakini tusifanye hii issue ni ya kidini ndugu zangu...

Ni Tanzania kila mtu ana haki, yeah wanataka Kadhi lakini rais kasema hapana;

Tufurahie huu Umeme utanufaisha wote hautajali Dini, Rangi, Kabila...

Asante nngu kwa kuliona hilo. Masuala ya dini yawekwe pembeni. Mradi huu unanufaisha wote bila kujali wanaabudu wapi.
 
Anaweza kuwa kafanikiwa in one way or the other, lakini kila alichouliza kajibiwa ila NAMSIFU KWA UBISHI...............
 
Mkuu sijui unaandika kutokana na jinsi unavyofikiria wewe au kweli umezisoma katiba za Iran na Saudia. Katiba yao haisemi kunywa Pombe ni haramu isipokuwa inafuata Sharia Law na katika kutafsiri Sheria hizo, wanasheria na mahakama hutumia vifungu vya sheria (act) ambavyo sii lazima vimeandikwa ndani ya katiba mama with specific instructions kama madai yako. Narudia kusema hakuna katiba mama inayosema Pombe ni haramu (Iran na Saudia) wala hapa kwetu Tanzania hakuna mahala ktk katiba mama imeandika Ushoga ni haramu na kutoa specific instructions...Hilo kwanza.

Katiba imetamka kwamba serikali yetu haina dini na nimewauliza ina maana gani ktk usemi huu - hadi sasa hivi mnazungusha huku na kule kujibu hamtaki na kama kweli wewe mpenzi wa haki tuirudie katiba na kuitafsiri ipaswavyo na sii kulazimisha kudai katiba mama lazima iseme kwamba ni haramu kushirikiana na vyombo vya dini. halafu mnaipotosha maana swala sio kushirkiana serikali inaweza kushirikiana na chombo chochote kile isipokuwa kuunda Partnership na chombo kimoja cha dini kwa kutumia kodi zetu hii ndio hoja yetu ambayo nina hakika inatokana ana muafaka wa MoU.. na tunasema muafaka ule ulikuwa makosa makubwa ya kiutawala..

Mnachobisha nyie ni sawa kabisa na sisi enzi zile za Nyerere, kutaifisha mali za watu, means of production kuhodhiwa na serikali kisha mnakataa kwamba sisi sio Ma- Communist kwa kutafuta tofauti zetu na Ukomunist wakati mnaupiga vita Ubepari kwa hali zote!. Kifupi nitakwambia hivi Usocialist upo karibu sana na Ucomunit kuliko Ubepari hivyo Bepari akisema wewe Mcommunist bora kwanza kubali kisha elezea tofauti zako na Mkominist lakini kwangu mimi hawa ni walewale - Nyani na Ngedele...Yanayofanyika sasa hivi serikali ipo karibu sana na kanisa kiasi kwamba inafungamana na kanisa na kuunda Partnership which is very wrong!

Mfumo wa kiutawala unavyofanywa sasa hivi na CCM ambayo maajabu wanaChadema mnaichukia mnakubaliana na sera hizi za CCM jambo ambalo kisiasa linanifanya nijiulize kwa nini nyie sio CCM ikiwa sera za Udini zinazopendelea kundi moja mnazikubali?.. Halafu kesho mtaanza tena kumtukana JK wakati anatimiza wajibu wenu kama mnavyotaka. Wakati huo huo Waislaam nao wanampa support JK ambaye anazidi kuwagawa na kuwakandamiza. Hizi siasa zenu kama sio Unafiki tena ktk imani za dini kitu gani?...
 
Muzee uzee unakuingia vibaya au? weekend ilikuwa ndefu kidogo, hapo ni kwamba serikali kutokana na ukwasi walishindwa kufanya huo mradi ndio kanisa likaona kwamba linaweza kuinvest sasa kama wamekosea basi tuwasome fatwaa

Acha ujinga ndugu soma mradi umefadhiliwa na nani,
kanisa Katoliki jimbo la Njombe linatekeleza mradi huo kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ACRA.

Aliwataja wahisani wengine kuwa ni wizara ya mambo ya nje ya Italia,mkoa wa Lombaridia-Ilaty,Itervita,Foranzione Cariplo na umoja wa nchi za Ulaya
 
Mkandara hilo la maana ya serikali kutokuwa na dini limeshajibiwa mara kadhaa kwenye thread hii. Labda useme majibu hayo hayaendani na vile unavyotaka wewe, in which case inabidi wewe ndio utumabie hiyo maana unayotaka au unayoona ni sahihi.

Labda tujaribu kurudi kwenye hoja/habari ya msingi...JK amefungua mradi wa umeme huko Njombe ambao umeasisiwa na kanisa katoliki likishirikisha wadau mbalimbali (wakatoliki na wasio wakatoliki). Labda sasa ufafanue hoja yako ya kikatiba ya serikali kutokuwa na dini (au serikali kuwa na dini, for that matter!), katika muktadha wa mradi huu wa umeme. Hii itasadie tuwe na mjadala unaoeleweka badala ya ku 'flip flop' kwenye manung'uniko kadhaa ya waislamu wa Tanzania.
 
Unajua watu wengine hata kufikiri kwao kuna kikomo..inasikitisha sana. Hivi tuliwakataa Richmond kwa sababu gani? nipeni sababu zote ambazo tuliwakataa Richmond hata kiutaalam kisha tutazame je kanisa lina sifa hizo za uzalishaji umeme? Jamani why kanisa lizalishe umeme na kuuza kwa wananchi - I guess ndio Taasisi ya kwanza nchini kupewa nafasi hiyo..
Hivi kweli kuna tofauti na Utawala, tukitumia sababu ya kutoa huduma kwa wananchi wote!
Basi bora wapewe nchi kabisa, watawale lijulikane moja..
 
Alojibu tulimalizana na hakurudi tena nataka wewe jibu lako kisha tujadili tu kuhusu katiba na sio vinginevyo..maanake toka nimemjibu hamkurudi tena mkabadilisha hoja ikawa Mkandara mkimbizi..Makosa sio kufungua mradi huu kwa sababu muafaka wa MoU unawapa sheria kama ulivyotokea Muafaka wa CCM na CUF walipomaliza kupitisha na wakaunda chama chao nje kabisa ya kuvishirikisha vyama vingine. Na ndio maana leo mnawaita CUF ni CCM - B... Mtazamo ni ule ule haubadiliki ktk swala hili la kanisa na CCM.
 

Huu sasa ni wivu, kwani wengine walianzisha project kama hii wakazuiwa?
 
Humu kuna watu wanaugua udiniasis! Poleni sana maana virusi vya huo ugonjwa havina dawa zaidi ya kufikiri nje ya ugonjwa wenyewe!
 

Wana JF wenzangu naamini MUNGU alitupatia dini kusaidia kufanya mahusiano yetu na maisha kwa ujumla yawe na maadili ambayo msingi mkubwa ni kuvumiliana (katika tofauti zetu kiimani na kimawazo) na kusihi kama ndugu kuifanya dunia mahala pema na pazuro zaidi kuishika.

Makelele yenu ya dini X ina hiki, diniY wanafanya hiki ambacho ni haramu n.k. Yanaharibu maana yetu nzima ya kuwa waumini wa dini tunazojifanya twaziamini na kuenzoi kuliko hata founders wake!
 
Alojibu tulimalizana na hakurudi tena nataka wewe jibu lako kisha tujadili tu kuhusu katiba na sio vinginevyo..maanake toka nimemjibu hamkurudi tena mkabadilisha hoja ikawa Mkandara mkimbizi......
Nilishajibu post #46! Tujadili kuhusu katiba katika muktadha wa mradi huu wa umeme...vinginevyo tutakuwa tunaendelea kuiharibu hii thread.

Hilo la ukimbizi hata kama lipo, sikulitoa mimi na kwa maoni yangu halina mchango katika hoja hii. Pengine aliyeliibua ilikuwa ni reaction ya kuona ati mtanzania wewe unajivunia kukaa nje ya Tanzania (nchi za kikristo!) kwa muda mrefu! Anyway tuweke hili kando ni siasa za majitaka tu.

...Makosa sio kufungua mradi huu ....
Kumbe tatizo la kikatiba ni nini hasa juu ya mradi huu?
 
Mfumo kristo yaani sisi hata hospital ya wilaya hatuna wenzetu wanazalisha umeme ?.


 
Mkandara swali kama hili sikutarajia litoke kwako ?.

 

Hivi kama ni kweli kanisa na ccm wana mou yenye uelekeo unazungumzia wewe kwa nini bakwata ni pro ccm? Si wangeisusa hiyo ccm?
 

Nakubaliana na wewe 100%
 
Narudia kuuliza hili swali
Tatizo la Tanzania nini?
  • Ni "kanisa"?
  • Ni kanisa Katoliki?
  • Ni wakristu ?
  • Ni baadhi tu ya wakirstu?
  • Ni baadhi ya waislam?
  • Ni baadhi ya wakristu na baadhi waislam
  • Ni baahi ya watanzania?
BTN
Inakuwaje kuna watu hawana aibu wanatumia jina la nyerere negatively kwenye thread hii na wakati huo huo huo wanashindwa kupata ujasiri wa kumtaja Jakaya Mrisho (Positvey au Negatively) amabaye kwenye Movie hii ni kati ya masterling wakuu
. Alafu mtu kma huyo ndiyo analijua tatizo.
 
Hivi kwani Waislam wamezuiwa kuomba misaada SAUDIA ili wafanye mambo ya maendeleo? Siamini kama Mashirika na watu binafsi UAE watakataa kufadhili miradi ya waislamu wenzao, naamini misikiti ikaweka masheikh wasomi wakaandaa proporsal zenye akili-hasa katika miradi ya viwanda vya siraha kama mabomu na bunduki watapata tu wadhamini!!!! Taratibu vidole na macho jamani, hii miradi inatunufaisha wote bila kujali mimi m-protestanti, shangazi yangu muislam au mjomba yangu mkatoliki; sote tunatibiwa kwenye Hosptitali za hawa jamaa, na watoto wetu wanasoma Vyuo vyao biila ubaguzi..hata huu umeme wao ukiunganishwa kwenye gridi ya taifa wallah Ustaadh Jumaa atafurahia kuwasha kijilaptop chake na watoto kuangalia TV bila kujali umeme wa warumi!!!
 
Kama Mrisho Kikwete, Nazir karamagi , nk na wenyewe ni shemu ya so called mfumo kristo au kanisa au Kanisa katlolkii then that name is used to mislead People.
Je kwa nini wanawa mislead watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…