Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)


Greater is He who is in us than who is in them....Nimefurahi kuona kuwa wako sehemu zote lakini siyo rohoni!
 
TISS haina nguvu zaidi ya umma, hakuna kilichokuwa na nguvu zaidi ya UMMA katika taifa lolote lile. Abdulla Al Senussi alikuwa Chief of Intelligence wa Ghadafi, yu wapi leo?

Ngoja nami nisisitize kama alivyokuwa akisisitiza Iddi Amin..........."and ZIS IS VERI IMPORTANT!"
 
Duh, hii thread niliignore ilipoanza. Leo imenipotezea masaa karibu matatu kuipitia. Naona mlta hoja na na huyu bwana mtoahabari ni mtu yuleyuel. Mtoa habari anavyoandika inaonekana kabisa kuwa siyo mgeni humu ila kaamua kutumia hilo jina kwenye hii thread kwa malengo yake. Baada ya hii thread hatutamuona tena, kwani atarudia identity yake.

Kwa mtizamo huo, naona kinachoendelea hapa ni mazingaombwe tu!!!
 
Ngoja nami nisisitize kama alivyokuwa akisisitiza Iddi Amin..........."and ZIS IS VERI IMPORTANT!"

Ambao ni sauti ya Mungu naye huifanya busara ya wanadamu kuwa upumbavu. Ambapo hutumia vitu vidhaifu kuviaibisha vile vyenye nguvu. Alleluja hosiana to the King! Sijui kwa nini mwaka huu mimi na raha sana.
 
tatizo lako ni moja tu ..''lack of power from within and cpativity of negativity''...hapo ulipo unatawaliwa na ''power of disguise'' na ndio maana unasema hii habari ni mazingaombwe.....masaa 3 umeyamaliza kwa kusoma mazingaombwe???!! hukuwahi kuyajua haya....hukutegemea kama kuna haya....umetolewa porini na kuletwa barabarani sasa unashangaa tu na kuona ni mazinagaombwe.....jiamini iatakusaidia sana
 
...nadhani itakuwa ni muendelezo baada ya kumaliza kazi wtapotezwa pia.
I was thinking the same...

Sasa ndo namwelewa mtoahabari pale aliposema ni nguvu ya umma tu, zaidi ya hapo ni kama mafisadi wameshatuzingira kabisa!
 
Mkuu Mr Zero, hivi waliyekuwa wakimwita Mr Zero ni Sumaye?

Kwa uzoefu wangu humu ndani, mmefanana sana kwa namna mbali mbali...
 

prof mwaikusa aliuwawa na watu wa paul kagame kutokana na "ukaidi' wake wa kumtetea mfanyabiashara mkubwa wa rwanda ya rais Habyarimana Yusuf Munyakazi kiasi cha kufanikiwa kuzuia mfanyabiashara huyo kurejeshwa rwanda ili akahukumiwe rwanda kama alivyotaka kagame,katika utetezi wake prof alijenga hoja kwamba mteja wake (Yusuf Munyakazi) kama kesi yake ikihamishiwa rwanda hatapata fair trial,kufuatia ushawishi wa serikali ya Rwanda kwa prof mwaikusa kukwama ndipo vikaanza vitisho na badae mauaji yale kutokea...na Ushahidi wa hili upo wazi, Prof Peter Erlinder kama mnakumbuka aliomba kuwasilisha utetezi wake kwa wateja anaowawakilisha kwenye mahakama ya kimataifa ya Rwanda kwa kupitia picha za video yaani 'video conference'.

Katika kutilia nguvu omba lake hilo alisema usalama wake ungekua mashakani kama angekuwapo mahakamani Arusha kimwili kwa kuwa Serikali ya Rwanda inatekeleza mpango wa kuwaua watetezi wote wa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari. Profesa Peter ambaye ni mwanasheria wa Kimarekani alienda mbali zaidi kwa kusema hataki yampate yaliyompata mwanasheria mwenzie Profesa Juani Mwaikusa..!

Kuhusu TETESI za Balali kuonekana kwenye mall mimi simo.
 

sasa mkuu pamoja na hawa jamaa wa rwanda kuingia nchini na kufanya mauaji kwa mtanzania ambae ni mtu aliyekwenda shule na analisaidia Taifa kwa kazi mbarimbari,inakuwaje nchi yetu kukaa kimya na kukubari mauaji yanafanyika kwa lengo la muilinda rwanda? je ni halali kwa majasusi wa nchi moja kuingia na kupoteza maisha ya raia wa nchi nyingine bila wakulu wa nchi kujua?
 

Nilipotoa tahadhari hapo awali kuhusu mazungumzo juu ya ENL huko kwenye mabaa ni kwamba, vijana wote wa mjini wenye akili zao timamu, elimu nzuri, na pesa zao, kama wale wanaojiita G8, na wengineo wengi, wote wapo upande wa ENL, na wapo vitani na wote wale watakaothubutu kuchafua hali ya hewa juu ya God Father. Iwe ni kwenye mabaa, gesti, mahoteli makubwa kwa madogo, gymkhana, maeneo ya starehe ufukweni, au popote pale, vijana hawa wapo kazini, masikio yao ni marefu na mikono yao kunyamazisha maadui, ni mirefu zaidi, kuliko ile iliyopo ndani ya Ghorofa jipya la TISS, Ostabei.

Huu ni uongo na ni vitisho vya kitoto,eti G8 hii nchi yetu inakoelekea na hizi propaganda sijui mwisho wake ila kiufupi mimi club ntaenda na lowassa ntaendelea kusema hatufai na yeye mwenyewe kila nitakapokutana nae akileta majisisifu yake kama kawaida yake akishakunywa whisky ntamwambia hafai kuwa rais,halafu nione hao G8 Sijui nani watakachofanya,yani mimi mtu kama Davis Mosha kaja mjini hapa namuona eti nishindwe kutoa mawazo kwa kumuogopa kisa G8..mavi ya kuku,yani brother kidogo nilikua nakuamini ila ulipowataja hao walevi wakuja hapa mjini G8 Nimekuteremsha zaidi bora ungeendelea na hadithi zako za kwenye corridor za tiss!

Kuhusu ridhiwani na pia miraji hawakupelekwa kusoma nje na IMMMA!hii sio kweli aliyewapeleka hao watoto na kujaribu kuwasomesha alikua ni James Sinclair,na huyo ridhiwani alikua anakaa nyumbani kwa huyo mzungu mpaka baadae alipomwambia baba yake kwamba hataki kuishi na mbwa ndani (unajua wazungu na mbwa tena)ndipo huyo mzungu alipoamua kumlipia apartments!! sio lau wala ishengoma brother
 

Za Rwanda nazo ni tetesi, kama zilivyo tetesi za huko Mall Nepal.
 

SEMA WEWE KAKA NIMESEMA HAPO JUU KUHUSU G8 akina EDSON wamenikebehi.

Mtoahabari Kawachota akili.
 
Sawa. Mimi nachofanya ni kutoa taarifa tu, sio zaidi ya hapo.

taarifa zako zimejaa vitisho unajaribu ku create fear ili watu wasimjadili lowassa kwa kuwaogopa kina davis mosha,we kama unawaogopa shauri yako kaka,lakini kiukweli hawana lolote wale ni misifa jazz band,huyo lowassa mwenyewe pengine wanazisikia tu habari zake,wadau niwaambie kitu kwanza hakuna mtu muoga kama lowassa,mnajua kwanini siku hizi ananywea whisky zake nyumbani wakati alikua member mwenzetu mzuri tu kwenye kikao chetu cha jioni?anadai eti ana maadui wengi nae anaogopa kuuawawa kama huyu jamaa anaetuletea taarifa anavyotaka na sisi tuogope tuanze kunywea vyumbani kama jamaa!nyie endeleeni kusikiliza hivyo vitisho visivyokuwepo,taarifa za huyu jamaa zinataka kuwanyang'anya uhuru wenu wazee wenu walioudai kutoka kwa muingereza kwa niaba yenu,mtoa taarifa waambie waliokupa hizi taarifa wanadhani zinaweza kumtisha mtu kama jenerali ulimwengu,ami mpungwe,kleist sykes,wendo mwapachu n.k.,muulize lowassa,kwanini siku hizi haji club?mbona chenge anakuja?
 
G8 si ya kupuuza! Mtajua system ikibadilika,Mtoa habari amefanya niamini hii kitu niliyokuwa naambiwa naona za vijiweni hizi!
 
Reactions: DSN
Za Rwanda nazo ni tetesi, kama zilivyo tetesi za huko Mall Nepal.

Ni tetesi lakini hazifanani na za marehemu Balali kuoneka akishop in a mall...!ni wazi kwamba kulikua na kitisho serious thats why kuna mtu akagoma kuja kufanya kazi live arusha akasisitize atumie video na hilo likafanyika!
 
G8 si ya kupuuza! Mtajua system ikibadilika,Mtoa habari amefanya niamini hii kitu niliyokuwa naambiwa naona za vijiweni hizi!

kwa hiyo na wewe umeingia kwenye mtego wa hizi habari alizopewa mtoa habari azilete hapa na sio kwingine,so kweli utaacha kutoa mawazo yako huru na kuamua kudumisha fikra za mwenyekiti lowassa kwa kuliogopa hilo genge la walevi wachumia tumbo wanaojipendekeza kwa lowassa ili aje kuwapa tender kama atashinda?
 
Mkuu kwa mnyonge mie ndio maana natumia jina feki hapa(hata wewe vile vile!).hao wapambe Godfather wao Lowasa! Mie hata dhamana itabidi aje mjomba wangu muuza Mbandule kule Nyarutunguru kuokoa jahazi!
 
WIKI LEAKS Huwa anatoa ushahidi. Kama unao chukuwa fursa hii kwa kuudhihirisha uwanjani. Ama kama ni dhana yako tu.....Jihadhari. Nina experience mbaya sana juu ya uzushi kama huu. If it falls in wrong hands waweza kuzusha mlima toka kwenye kichuguu. Hasa kama swala linalo husu amani ya taifa. Nina uhakika kama ni kweli mwenyewe ameshapata habari.

If A is a success in life, then A equals x plus y plus z. Work is x; y is play; and z is keeping your mouth shut.
 

Pengine sijaeleweka. Sina maana ya kwamba watu hawa ni wa kuogopa, hivyo wazalendo wa nchi hii wafunge midomo yao. Ujumbe wangu kwa wazalendo wote wa nchi hii ni kwamba vijana hao wapo kazini, kila sehemu, hivyo ni muhimu kulijua hilo, sasa kwa wale watakaochukulia hivi ni vitisho, sawa, kwa wale watakaochukulia hii ni taarifa muhimu ya kuijua katika mapambano, nayo sawa tu. Mimi sina nia nyingine zaidi ya kutoa tu taarifa.

Hawa ni watu hatari, na kupambana nao ni muhumi lakini pale tu kila mpambanaji atakapokuwa na taarifa. Kama Jenerali Ulimwengu ni mtu wako wa karibu, muulize jinsi gani kina EL walivyomfanyia unyama miaka ya nyuma pale walipokodi watu kwenda kumwingilia kinyume na maumbile. Hawa watu ni wanyama, na ndio kiini cha tahadhari nazotoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…