Hutaki Unaacha,
Kwanza asante kwa hii. Wanabodi hii mada si ya kupuuzwa hata kidogo bali ni uthibitisho tuu 2015 ni CCM ni Edward Lowassa na mgombea Mwenza Amani Karume, Rais wa Zanzibar ni Maalim Seif, Makamo wa kwanza ni Ismail Jussa!. Waziri Mkuu wa rais Lowassa bado sijamjua ila King Maker!, nimemvulia kofia!.
Waraka huu ni uthibitisho wa sisi tunaompigia debe Lowassa tuko right.
It's very very unfortunate rais Jakaya Kikwete kwa Mtandao wa Lowassa, yeye si lolote sii chochote!. Yaani hawezi kufanya lolote it's too late now!.
Waraka huu umenipa mwanga ambao sikuufahamu kabla, ni ile siri ya muafaka walikuwepo Jussa na Maalim Seif tuu na Karume!. Taarifa za Shein kutoshinda uchaguzi wa Zanzibar nilizisikia na siku ya kutangazwa matokeo nilikuwepo Zanzibar, kwa Seif ninayemjua mimi, sikupata picha alikubalije!. Sasa nimeelewa, anaerum CUF ni Jussa sio Seif na ndio maana Hamad Rashid kuonyesha interest ya Ukatibu Mkuu ataharibu na ikibidi watammaliza!.
Wapenzi wa JK samahanini sana kuwaeleza yeye si chochote si lolote mbele ya EL kuelekea 2015 kwa sababu kama ni King Maker alimweka pale Sitta na akamng'oa na kumweka Anne!. Then JK hana option zaidi ya kumuahidi EL ikulu 2015 vinginevyo mwakani baada ya uchaguzi wa CCM, EL atamtaja yule mwenye zigo la Richmond alilombebea na kupitia Bunge, impechment process will be initiated na ikisail through that is the end of the road kwa CCM!. Ila RA ataiback up CUF na sio Chadema ndio maana Jussa ni strategic link!.
Suluhu pekee kwa JK na CCM kubaki salama ni kumteua Lowassa ili asimwage mboga!.
Kwa kweli baada ya kuzisoma powers za King Maker, nami Pasco wa JF najiandaa kukaa karibu na wafalme ili japo ninukie manukato!.
Kwa waraka huu, Lowassa ndio tayari Mgombea, Dr. Bilal ni spent force atapumzishwa!.
Kwa wasiojua politics is a dirty game, wait and see for yourself as 2015 draws near!. Kitu ambacho sijafahamu ni jee watu safi kama Dr. Shein, Nahodha na Dr. Mwinyi zamu zao zitakuwa lini kuuonja urais wa Muungano au urais wa Tanzania kwa Mzanzibari ni nehi kimoja?.
Pasco wa jf.