Nakuja Bongo nitakufuata rasmi Ofisini...Wildcard,
Wewe inabidi nikutafute tufanye huu mjadala ana kwa ana. Tuongee bila kuweka records kama tufanyavyo humu. Kisha tukubaliane kutokubaliana au tukubaliane kukubaliana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakuja Bongo nitakufuata rasmi Ofisini...Wildcard,
Wewe inabidi nikutafute tufanye huu mjadala ana kwa ana. Tuongee bila kuweka records kama tufanyavyo humu. Kisha tukubaliane kutokubaliana au tukubaliane kukubaliana.
WildCard, japo mimi nasimama na Lowassa kwenye ukweli, lakini nakuunga mkono, kama unaamini JMK anamgwaya kumfikisha mahakamani, its fine, then baada ya uchaguzi naunga mkono 100% kwa 100% EL afikishwe mahakamani kueleza alikoutoa utajiri, ila nashauri kwanza atangulizwe yule mwenye zigo halisi la Richmond, na sio Lowassa, yeye ni mbebaji tuu!.KATIBA MPYA itamtupa Lowasa wako mbali kabisa kama sio JELA. Kama JMK anamgwaya kumfikisha mahakamani sasa, 2015 baada ya uchaguzi mkuu tutajua la kufanya na Rais mpya atakayekuwepo. Mali na Rasilmali za WATANZANIA lazima zirudi.
Mkuu KALABASH, du!, unakumbuka mpaka such details?, au ilikuwa inakuja pale kwa Mzee Msa Hassan?.Umenikumbusha mbali kuhusu hiyo Volkswagen TAP 180, Tena niongezee kuwa ilikuwa left hand drive(LHD)
Lol...sasa naweza kusema kwa uhakika kabisa hata mzee wa vijisenti nae 'tulimwonea'...maana ni kweli vilikuwa 'vijisenti'! Pasco, honestly, hivi kumtetea kote huku EL ni kwa maslahi ya nchi yetu ya Tanzania? Kweli!?....Lowassa kajenga vijumba viwili vitatu vinaonekana, na kile kishule pale, basi ndio imekuwa taabu!...
THE ROMANTIC [TR] kwa kawaida msimamo wangu humu ndani kwa wanajf ndani nilishaweka wazi kwamba mimi TANZANIA MBELE.Mimi na vyama vya siasa paka na panya.Nimefuatilia jukwaani mchango wako wewe kwangu si mmoja wa wale TANZANIA MBELE.Hivyo basi mchango wako umenipelekea kufanya utafiti japo kidogo tu ili nijue kabla sijasema mengi dhidi yako kupitia michango yako humu ndani basi nijaribu kukujulisha kuwa wewe simmoja wa watu wanaostahiki kuchangia mada [thread ] za Hutaki Unaacha [HU] kwa kuwa wewe na yeye hamsafili mashua moja mwenzio anazungumzia issues unazungumzia watu.
Japo unaweza kunyoosha kidole kwa kuona kataja watu, kwa tulipofika kwa kuwa tatizo letu ni watu waliochafua mfumo basi hana budi kuwaingiza kwenye thread zake ili kutupatia mtililiko wa mkakati tatizo uliotusibu Watanzania.Basi kama unaupeo hafifu hakika HU utaishi kudandia vijisehemu vidogo visivyo na uzito nawe kuvigeuza mazungumzo yako na kushindwa kubeba ujumbe ulio ndani ya ujumbe mzima.Ili kumjua HU yakupasa uwe INNATE vinginevyo si lazima kuchangia unaweza kusoma,japo sikukatishi tamaa ukijifunza waweza kuwa na mchango mzuri sana ndani ya JF.
Ukitaka kujua ujui unachofanya angalia Identity name yako uliyochagua THE ROMANTIC [eeeeeeeeh thats teens kind of a identity].Soma defition ya Romantic kisha kaa chini tafuta aina mpya ya Identity kisha ludi ndani ya nyumba JF tutangazie Identity yako mpya wanaume na akili zetu basi tutajua kuwa hata mchango wako utafanana basi na ujio wa jina lako jipya.
Kwa kukusaidia definition ya Identity yako
THE ROMANTIC is If you say that someone has a romantic view or idea of something, you are critical of them because their view of it is unrealistic and they think that thing is better or more exciting than it really is.
Hivyo sio makosa yako kwa a true great thinker kwa uchache naweza kusema maneno machache kukuhusu wewe kupitia sentensi nyekundu hapo juu.
Sugu zamani aliitwa MR II Proud,kijana alipokuwa akatafakari sana akaona la anakoelekea anaitaji kubadilika na kuwa mtu mzima mwenye msimamo wake makini,akachagua jina kwa utafiti wake akona sugu linamfaa akatuwekea jina jipya SUGU na kutupatia tafsiri yake watanzania kwanini amechagua jina hilo na watanzania kumkubalia kuwa kweli kwa alikopita na kuyatenda basi anastaki hatimae leo hii ni Mbunge wa Kuchagulia Mbeya Tena Mkoa wenye watu makini na waelewa.
Hivyo hivyo Dudu baya alichagua jina yaliyojili kwenye jina lake watanzania wote imekuwa historia kwenye mziki wa kizazi kipya,maskini akakaa chini akaona du jina hili uwenda ndio sababu akajigeuza kuwa Dudu zuri,lakini maskini hakujua kuwa bado DUDU ajaliiacha hivyo basi imekuwa ndio mwisho wake hajulikani hata yuko wapi.
THE ROMANTIC bado unao muda jipange
Jack Zoka ni mzee ninayemheshimu sana, nimemfahamu miaka ya 80, wakati ule akiwa afisa TISS kwenye ubalozi wetu Harare, Sir George Kahama akiwa Balozi wetu pale.
Mtoa habari sio bar ya salender bridge kaka! Pink cocunut? Au mie ndo nipo outdated? Ngoja Romantic kama atathubutu aseme! Lol
FP,![]()
President Julius Nyerere is pictured on January 16th when he addressed an open air rally where the detained former Tanzania Minister and Vice-President of Zanzibar was brought to face the people. Mr. Kassim Hanga (seated between two police officers) is under detention with a number of other top Tanzanians after allegedly boasting that he had been called from voluntary exile in Guinea to lead an army coup on Zanzibar.
source: Mzalendo.net
WildCard, japo mimi nasimama na Lowassa kwenye ukweli, lakini nakuunga mkono, kama unaamini JMK anamgwaya kumfikisha mahakamani, its fine, then baada ya uchaguzi naunga mkono 100% kwa 100% EL afikishwe mahakamani kueleza alikoutoa utajiri, ila nashauri kwanza atangulizwe yule mwenye zigo halisi la Richmond, na sio Lowassa, yeye ni mbebaji tuu!.
Kama hoja ni utajiri, kwa taarifa yenu, Lowassa ndio mwenye afadhali!, jee ungewajua wamiliki halisi wa Ngurdoto?!, Grumet?!, Haidery Plaza, hata huyo mwenye Scandanavia Express mnaemjua siye peke yake!, mwenye Sumri mnayemjua siyo peke yake! kosa la Lowassa ni kuwa mkweli kwenye umiliki wa mali zake kuweka yeye na mkewe ndio wamiliki pekee wa 50% 50%, hao mafisadi wengine wanaotumia majina ya ndugu, jamaa na marafiki zao, kwa vile hamwajui walimili halisi, basi ni kelele nyingii Lowassa fisadi mkuu!. Hata fisadi aliyekubuhu kabisa RA, anamiliki makampuni 17, kati ya hayo ni makampuni matatu tuu ndio jina lake lipo, Caspian, Vodacom na New Habari, the rest ni majina ya ndugu!.
Mafisadi wanaotutia uchungu sana sisi, ni hawa wenzetu wenye ngozi nyeusi!, lakini wenzetu wenye ngozi nyeupe, wala hawatusumbui!. Kwa wale wa zamani mlioisoma ile ripoti ya Tume ya Warioba kuhusu rushwa, vinara wa rishwa wametajwa wazi wazi na hakuna hatuo zozote zilizochukuliwa!.
Mfano kuna kampuni X, kampuni hiyo inazozo kampuni zake tanzu U, V, W, X, Y Z!
Kampuni U ni import export, inaagiza mzigo
Kampuni V ni Shipping company inausafirisha huo mzigo.
Kampuni W ni Clearing Agent inauclear ule mzigo
Kampuni X Transporter inausafirisha ule mzigo kama goods on transit (bila kulipiwa ushuru)
Kampuni Y ni Insurance Company inauwekea bima huo mzigo
Kampuni Z ni Storage Company inauhifadhi huo mzigo (storage facilities)
Kampuni hiyo inaagiza millions of tons za bidhaa, makampuni yote yanaingia kazini, paper work inaonyesha bidhaa zimewasili nchini zimekuwa cleared duty free, zimesafirishwa on transit, ila kabla hazijavukla mpaka zime vanish into thin air, mwenye mali anashitaki ile kampuni ambayo haukutimiza wajibu wake, kampuni yake ya bima, insimamia, bidhaa zina end up madukani kwetu!
Funny enough, hizo kampuni zina make, billions lakini hazina any fixed assets!, wamiliki wanaishi msajili wa majumba, magari ya transport ni ya kukodi, maghala ni ya kukodi, hiyo super profit inakwenda wapi?. Hao hamuwaoni!. Lowassa kajenga vijumba viwili vitatu vinaonekana, na kile kishule pale, basi ndio imekuwa taabu!.
Tumkatae Lowassa kwa mengine, hili la ufisadi nasema no!, a Big NO, mwenye zigo lake yupo asipomtua, Lowassa atalibwaga na mtamuona mwenye zigo lake akilikusanya likisha bwaga!.
Pasco (wa jf)
Mkuu mbona sasa unaji contradict? Kwenye uzi huu huu (ukusara fulani) umeandika kwamba ENL kuchukua nchi hii ni lazima na ni kama count down ya new year,, sasa mbona unakuja kivingine tena?? Unaanza kunitia mashaka
Mke wa Hanga bado yupo. Ana maelezo mazuri tu juu ya kifo cha mmewe. Mtafute maeneo ya Upanga. Ya Sokoine tuliyaona sote kama tulivyoyaona ya Dr OA Juma.
Wildcard,
Umejivisha upofu na kusahau. Mtu ambaye maisha yake yote ya ujana kasoro miaka 23 iliyopita alikua anamiliki Volkswagen TAP 180 anawezaje kufanya starehe za aina ya G8?.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Naona nakaribia kunyamaza maana argument zingine utafikiri mtu umeibiwa password ya JF! LOL
Uchaguzi wa NEC Ni November katikati, na huko amejipanga kupata wajumbe wa kutosha, na vile vile wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa idadi nzuri kutoka kanda ya ziwa na huko visiwani.Twendeni pole pole tu kwani nina Imani ya kwamba 2015 mambo yatakuwa mazito kwa upande wa siasa,ULE UCHAGUZI WA NEC UTAFANYIKA LINI? Maana Mi nafikiri kutachimbika pale watakapofikia upande wa uchaguzi!
Mtoa habari kama sikosei kwenye page moja humu umesema kwamba kwa sasa kuna baadhi ya vijana wa tiss wameshaanza kuside na lowassa kwamba inaonekana anaonewa,pili inavyoonekana jamaa amekamata system kwa kiwango kikubwa tu pia kuna sehemu umesema kwamba wa kumzuia lowassa asiingie ikulu ni UMMA,mimi kwa mtazamo wangu UMMA hauwezi kumzuia,na nyie vilevile credibility yenu machoni na mioyoni mwa wengi wetu imepotea,NO ONE HAS THE BALLS TO STOP HIM Mark my words kama mkulu tu anamgwaya itakuwa nyie?Hicho ni kiapo ambacho wengi wetu tumekula kwamba tutapigana mpaka tone letu la mwisho la damu, na kuacha walio hai waendelee na mapambano hadi adui aanguke. Ni wazi kwamba vita hivi ni vigumu sana kuvishinda, lakini inshalah...
Jamaa yuko maandishi yake yako very technical,ukiingia kichwa kichwa utacheza ngoma ya lowassa bila kujielewa,si unasikia kuna watu wanakwambia kesho maofisini na kwenye barza za kahawa wataipata?hapo lengo la "mleta mada" hutaki unaacha litakua limetimia au halijatimia kwa watz wa kawaida ambao wanapenda sana kuhadithiwa ili wakahadithie kama walikuwepo mahali husika?si unajua wabongo wanavyopenda kuonekana ni watu wa usalama wa taifa kwa kuhadithia story za "hatari" huko uswahilini kwetu?tuwe makini.
Leo utaambiwa Rashid othman kwa kuwa ana undugu wa damu na jaji wetu mkuu na ro inasemekana alichaguliwa na Lowassa na rostam nae pia kawekwa na hao japo hawakuwako madarakani jaji mkuu akichaguliwa,lakini wabongo kwa kupenda stori wanakubali bila kuchallenge,leo utaambiwa lowassa na rostam wana miguvu mpaka ya kutishia watu wasizungumze kwenye vijiwe lakini ukiuliza jamani eeeh hawa watu wakubwa kuliko chama na serikali walioshika kila sehemu nyeti si waliapa jimbo la igunga litaenda upinzani sasa imekuwaje bila msaada plus hujuma zao ccm imeshinda igunga?hawakujibu utaambiwa aidha hutaki unaacha au tulikua tunatoa taarifa tu,basi ili mradi sarakasi za maneno zisizoisha lakini wabongo wa wengi wa humu bado wako usingizini,hawahoji hoja za wazi kama hizi zinazohitaji ufafanuzi zaidi,wanataka stori zaidi za kwenda kutishia watu mitaani!
Figure It Out For Yourself
You've Got it Coming !
The guilty are always Afraid !
Hit Them Where It Hurts !
I Hold The Four Aces !
An Ear To The Ground !
Time for shock treatment !
Goldfish have no hiding place !
This is for real !
Do Me A Favour, Drop Dead !
The Vulture Is A Patient Bird !
My laugh comes last !
Believe this - You,ll believe Anything !
Ha, ha, haaa... Thank you James Hadley Chase.
Wasanii wanafunzi ...they tend to overact !
Funika kikombe, mwanaharamu apite !