Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Ni aiobu kuwa na TISS halafu haya yanatokea. Mimi sikatai mitandao ina nguvu sana lakini haliwapi uhalali wa kulala usingizi wa pono wakati intruders wanaingia na kufanya wanalotaka na kuondoka!!

Hii nchi ndo baso tena!!
 
Chadema kuchukuwa nchi matope yatageuka blue band!

Nilisema sitaki kuchangia lolote kwenye mfululizo huu lakini kuhusu CDM yangu nimeamua kusema....hapa hakuna cha Dr. Slaa,nchi yetu imeenda hiyoooooooo kwa CIA na agents wake.
 
na huyo Zakhia
faili lake likoje?
nasikia sikia tu
sijui kipi ukweli kipi uwongo...
Zakhia mwanzoni kabisa alionekana atakuja kuwa Iron Lady wa Tanzania kumbuka jinsi alivyodili na mafuriko ya Moshi (akiwa mkuu wa Wilaya) lakini kuna wakati huyu mama wakubwa "walimchezea" sana hadi ikawa hakuna jinsi bali kumwacha 'afunzwe' na dunia. Na maisha yake pale Chuo cha Ushirika Moshi hayakuwapendeza baadhi ya watu!!
 
Habari hii inatosha kuwa kitabu na mtu akawa tajiri tosha.
 
Gen Davis Mwamunyange JKT ilikuwa kazi kama kazi zingine za kijeshi, yeye Davis ni wa JWTZ toka kitengo nyeti, na jeshini hakuna dharau kwa mkubwa mengine ni uzushi tuu!!!!!!!!!!

kwa sababu unaona watu wanapiga saluti basi ndiyo unahisi hakuna dharau. Hivi Makame Rashid alikuwa anaheshimiwa?
 
Mkuu Mzee Busara, CDF Davis Mwamunyange sio msafi kihivyo unavyodhania, kuna issues zake za Afrika Kusini na nyingine za London ambazo ni za Davis Mwamunyange zaidi ya huyu umjuaye, tumezihifadhi tu kwa heshima yake!.

Kwenye red hapo ina maana wengine hawana heshima zao?
 
Zakhia mwanzoni kabisa alionekana atakuja kuwa Iron Lady wa Tanzania kumbuka jinsi alivyodili na mafuriko ya Moshi (akiwa mkuu wa Wilaya) lakini kuna wakati huyu mama wakubwa "walimchezea" sana hadi ikawa hakuna jinsi bali kumwacha 'afunzwe' na dunia. Na maisha yake pale Chuo cha Ushirika Moshi hayakuwapendeza baadhi ya watu!!

mkuu basi hata uni pm kama huwezi taja watu hapa
 
Hivi lile jengo la TISS pale karibu na TRA Sokoine Drive lina vifaa vipya vya kisasa kuendena na wakati huu tulio nao? Tangu enzi za mitarimbo mpaka sasa mbinu ni zile zile!! Nakumbuka miaka ya 1980 - 1983 Pale TISS Sokoine Drive kulikuwa na Jamaa mmoja anaitwa Mgono, alikuwa kila mara Beatle lake likimzimikia anakwenda kuliegesha pale Steak Inn na kulalamika " shushushu gani kumiliki Peugeot ni mbinde" TISS bado iko ville vile!!
 
JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)
Mr President,

Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).

Mtandao

Ninachozungumzia hapa ni kundi kubwa na hatari linaloaminika kuongozwa na Edward, Rostam, Othman, Apson, Karume na Shein na Mkapa. Ninakufahamu vizuri sana na ungekuwa uwezo wako, hawa wote ungeweza kufanya uwezalo ili kumweka madarakani mtu unayemtaka kwa maana ya Asha au Nahodha. Huu ni mtandao unaofanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana. Ukitaka kuamini, jiulize swali la kipuuzi sana kuwa kwanini kila plans unazofanya (zisizo na faida) kwa kundi hili zote zimefail?

1. Shein ni nani?

Nataka nikukumbushe ''issue'' ya Omar Juma. Huyu alikuwa threat kubwa kwa kundi lenu kwa ajili ya 2005. Mtandao wake ukibebwa na Mkapa ulikuwa ni hatari sana. The only way ilikuwa ni ''kumwondoa'' na hilo liliwezekana. Siku nikiwa na muda nitaeleza mchezo wote ulivyofanyika. Wakati jina limeletwa tukiwa hotel moja maarufu hapa Dar, nakumbuka hukuweza kumfahamu Shein wala kulitamka jina lake vizuri. Ulikosea mara tatu kulitamka. Tukacheka wote. Hatimaye Shein akawa makamu wa rais.

Baada ya wenzako kukuweka madarakani (mgombea ndani ya CCM), kosa ambalo Shein hataweza kukusamehe katika maisha yake (Mimi sio Mungu, kwani anaweza kukusamehe vilevile) ni pale ulipo-attempt kumfanya Zakhia kuwa makamu wa rais. Asingekuwa Edward, Rostam, Mkapa na Karume, leo hii Shein angekuwa mwenyekiti wa TPDC au TANAPA!. Kitendo cha Shein kuletwa na kundi hili, kutetewa na kundi hili achilia mbali kushawishiwa na kundi hili agombee urais wa Zanzibar ili kummaliza nguvu Nahodha chaguo lako kinamfanya awe mtiifu kwao kuliko hata kwa Mwanamwema!. Unafahamu vizuri Shein alivyoshinda urais Zanzibar, rafiki zako walikuchezea akili wakikuambia kuwa wamemleta Shein ili kupunguza kura za Bilal na ulipomkubali Shein wao wakaenda kumpigia Bilal kampeni wakijua kazi ya kumweka Shein imekamilika. Baada ya hapo uliendelea kumng'ang'ania Zakhia kuwa makamu. Mkapa akishirikiana na Rostam (ambaye alikuwa akim-install Bilal kuwa makamu huku yeye akiwa South Africa kuangalia World Cup) walimweka Bilal hapo alipo.

Shein hakushinda uchaguzi Zanzibar. Kilichofanyika ni Mkapa, Rostam, Karume kumhonga pesa za kutosha sana Maalim kupitia kwa kijana wao hatari sana Jussa (kumbuka huyu aliletwa na Rosatm ili umteue awe mbunge). Today, umeshindwa kumweka mtu wako Zanzibar na makamu wa rais Muungano. Walichoweza kufanikisha ni kuiteka Zanzibar yote (Bilal na Shein). Nakukumbusha ya kwamba, ili uwe mgombea kupitia CCM, unahitaji Zanzibar na 'Lake Zone'. Kule 'Lake Zone' wamekushinda. Hilo unalifahamu vizuri. Hii ndiyo maana Wanzanzibar wamekutesa sana ndani ya CC iliyopita. Ili kukuonyesha kwamba hufai, Shein kampa udaktari wa heshima ''Baba yake'' mdogo Karume. Ninafahamu jinsi unavyojikosha kwa Anne kwa kumpa nishani ili kusiwe na vote of no confidence mwakani hasa kwa sakata la Richmond na Twiga. Napenda kumhakikishia Anne ya kwamba that's a strategy anayoitumia Mugabe ya kuwamaliza watu. JK ameiiga huko. Naomba Anne uwe makini sana. Waweza kufa kwa ''presha'' usipoangalia.

2. Karume ni nani?

Huyu alipigiwa kampeni kubwa sana na Edward na Rostam mwaka 2000 licha ya CCM Zanzibar kumkata jina lake. Kwa hili Karume hawezi kuwasahau hawa jamaa mpaka anakufa. Karume alikupinga Butiama. Yeye, Edward na Rostam wakaenda ku-design ''mwafaka'' wao wanaoujua ambao leo hii unafanya kazi Zanzibar. Nataka nikukumbushe mara ya pili kuwa Jussa aliletwa kwako na Rostam ili umpe ubunge. Think twice! Karume ndiye rais aliyeleta maendeleo makubwa Zanzibar. Shein will do more than what Karume did. Usishangae ukisikia Karume kuwa makamu wa Lowassa 2015!. Karume ana msimamo. Hayumbi na bahati mbaya sana hakuogopi.


NITAENDELA SIKU NYINGINE WAPENDWA WANA JF
JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)
Previously:
JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Karume na Jussa ni wamoja na wanafahamiana vizuri sana kuliko wewe unavyofikiri. Kundi hili linao uwezo wa kuvunja Muungano muda wowote linaoutaka na kuanzisha serikali tatu na baada ya malengo kutimia likaanzisha serikali moja!. Ni vigumu kuelewa ni yapi majukumu ya Karume ndani ya hili kundi na nani kampa majukumu hayo na wapi kiburi cha Karume kimeegemea. Ni swala la historia ndefu sana ambayo nitaiunganisha vizuri baada ya kumchambua Rostam ambaye nitachukua muda mrefu kumchambua kuliko mwingine yeyote katika kundi hili.

Nafikiri urafiki wako na Karume waweza kuwa umeingia doa kipindi cha 2007 hivi wakati umeletewa zile briefcase zilizojaa dola na kumhukumu Karume kabla hujaenda uarabuni!. Hivi zile dola zilienda wapi Mh Rais?. Zilikuwa nyingi kwelikweli. Hata hivyo Karume anaweza kweli kusahau mchezo mliotaka kumfanyia wewe na Nahodha kuhusiana na mwafaka kabla ya kipindi chake kuisha na kupelekea kumtishia Nahodha nafasi yake ya Waziri Kiongozi? Nahodha akabaki analia wakati wewe umemruka tayari baada ya kuona umezidiwa nguvu?. Mr President, unawafahamu waliokuwa nyuma ya mchezo huu? Basi hao hao kwa miaka mingi wangekwishakumaliza lakini Edward alionekana "kukupenda’" zaidi na yeye amekuwa akiwawekea ngumu yaani kukulinda lakini kwa bahati mbaya sana, amewakubalia hivyo kufanya ‘‘game’’ kuwa kali. Edward anaweza kukulinda baadaye. Lakini hutaweza kufanya biashara yeyote ile na waweza kubaki na "njaa" kali sana baada ya kustaafu. ‘‘Game’’ hii ni hatari kwasababu lazima imuweke Karume kwenye nafasi za juu za uongozi wa taifa hili 2015. Mh Rais naomba umuulize Mama Maria Nyerere akwambie vitisho alivyopewa na Karume na Mkapa kuhusiana na mwanaye makongoro wakati wewe unaendesha kikao cha NEC. Hata hivyo ni vizuri ukajiuliza swali la kitoto kama hili: Je ni kwanini Karume na wenzake walikushinikiza sana umteue Tom Apson kuwa mbunge wao wakikudanganya kwamba Tom amefanya kazi nzuri ya kuiba siri za Apson na malecela na wengine? Think twice Jakaya!.

3. Rostam ni nani?

Licha ya kuwa rais wa nchi hii tena Kamanda mkuu wa vyombo vyote vya usalama, umeshindwa kumfahamu Rostam kwa undani zaidi. Nikiri kwamba, bado hujamfahamu Rostam vizuri na sidhani kama ‘’vijana’’ wako wanamfahamu vizuri. Kabla sijamwelezea vizuri, naomba nikukumbushe kitu kimoja. Hivi ilikuwaje mwaka 1995 wakati kambi yako inaomboleza baada ya kushindwa urais, Rostam alionekana kwenye sherehe ya kumpongeza Mkapa tena akiwa na Mkapa na kwa mazungumzo marefu sana?. Je aliwasaliti nyie washirika wake?.

Nikiri tena kuwa, Rostam aweza kuwa mtu hatari, mwenye akili ya haraka sana lakini mwenye kuzichezea kwa akili ya juu sana siasa za Tanzania kuliko mtu yeyote aliye hai niliyeweza kumfahamu hapa Tanzania. Huyu akiwa pale LSE UK, alijenga urafiki mkubwa sana na binti wa mkubwa mmoja na muhimu katika Tehran (siasa za Iran). Haikufahamika kwa haraka ni nini alichokuwa akikitafuta kwa huyo binti na nani alimtuma ajenge huo urafiki ghafla kiasi hicho. Hili ninalolisema kwa sasa hata Lowassa hawezi kulifahamu, si wewe peke yako.

Ni vigumu kuamini kuwa, Serikali ya Marekani imegharamia masomo ya Rostam LSE (baada ya hii task) na hii serikali kupitia Prof mmoja anayefundisha chuo kikuu kimoja UK huku akiwa ni mfanyakazi wa CIA iliweza kufanikisha urafiki mkubwa wa Rostam na huyu binti huku yeye (Prof) akiwaachia maelekezo vijana wa CIA baadhi kum-monitor Rostam na hatimaye urafiki ukawa mkubwa sana kiasi kwamba ukaweza kumfanya Rostam akubalike na Tehran.

Kwa udhamini na wito kutoka serikali ya US, Rostam akawa anakwenda mafunzo mahsusi ya ki-usalama marekani na huko alikutana na watu wengi sana muhimu wakiwemo wamiliki wa Symbion. Kwa kukudokezea tu, pesa za Kagoda ni msamaha wa deni lililofanikishwa na ushawishi wake pale Tehran. Kwa bahati mbaya sana hata Mariam (mke wa Rostam) hakuufahamu uhusiano ule akifikiri ni mapenzi mpaka pale alipojua vinginevyo (ingawa hawezi kujua behind the scene kuna nini). Malengo ya Marekani na huu urafiki (Rostam-Tehran) bado yako palepale na nilipokutana na rafiki yangu (huyu aliweza kufanya kazi nzuri sana na Shah Riza kule Middle East) wa siku nyingi sana pale Boston, akanihakikishia kuwa lengo lilipangwa kutimia 2018 au 2022 hivi!. Ni hatari sana na mtandao wa Rostam na wenzake unaweza kukufanyia lolote watakalo kama usipokuwa makini!. Kule Saudi Arabia na sehemu nyinginezo ameweza kutumiwa sana na hawa ‘‘mabosi’’ wake kwenye masuala ya biashara.

Rostam anafanya kazi kubwa na nyingi za kibiashara na kisiasa na CIA kama agent wao muhimu sana Afrika huku yeye akisaidiana na mtandao wa CIA kule South Africa na ku-control sehemu kubwa Afrika Mashariki na Kati na sehemu nyingine za afrika ambazo US itakuwa na maslahi nazo. Mambo machache aliyoweza kufanikisha ni pamoja na kumfikisha Raila hapo alipo, mikataba ya kimaslahi na Salva Kiir achilia mikono ya Rwanda na Uganda kule Congo, Madagascar, mwafaka wa Zanzibar, kujivua gamba though kosa mojawapo ni wewe kukosea implementation hivyo kum-cost na kupelekea US kumwambia ajiuzulu ubunge na ‘‘kuacha’’ siasa kitu kinachomfanya afanye siasa mara kumi ya aliyokuwa akiifanya awali.

Mr President, muulize Othman akueleze ukweli kwa kuwa hili alilifahamu ingawa hajui ni kwanini lilitokea. Kumbuka vizuri wakati Bush amekuja Tanzania. Kule Arusha, viongozi wa makampuni makubwa yanayomiliki migodi mikubwa ambayo Bush, US na CIA ina maslahi nayo kutoka karibu kila kona ya dunia walikusanyika na walielezea ni kwanini biashara haiendi vizuri. Hakuna mtanzania yeyote Yule hata Deo aliyehudhuria except Rostam. Nani alimwalika na alihudhuria akitokea wapi?! Pale waliazimia mambo makubwa na ya hatari sana. Rostam anajua vizuri what happened na maazimio yale yalilenga nini.

US imeona wewe ni shida kwa kuwa nchi ni kama inakushinda vile na haioni tena mvuto wako kwa wananchi na hii ni hatari kwa maslahi yao hasa mafuta ya Zanzibar ambayo imeshayalia timing kwa maana ya kwamba imeshirki kikamilifu kucheza ‘‘game’’ ya Rostam-Jussa-Karume-Shein kwa haraka sana. Nimekwambia kwamba, Muungano waweza kuvunjwa na baada ya muda ukarudi tena nakuwa serikali moja. Jiulize ni kwanini Mwamunyange anakudharau kiasi hicho?. Hicho kiburi anakitoa wapi?. Mr President, usikurupuke, cheza karata vizuri!

WAPENDWA WANA JF, MNIVUMILIE KWA MPANGILIO MBOVU. NITAENDELEA NA ROSTAM KWA UPANA ZAIDI, THEN APSON, MKAPA, EDWARD NA OTHMAN
 
mkuu basi hata uni pm kama huwezi taja watu hapa
Subiri kidogo Boss. Hapa tunajitahidi watu wajue kwamba tunachokiongea hata kama kinatutisha kiasi gani lazima kina UKWELI fulani. Bilal alikuwa yuko karibu sana Mohamed Zahor ambaye alikuwa ni Katibu wa UVCCM, lakini huyu jamaa alishughulikiwa na Jakaya bila ya Bilal kuwa na uwezo wa kuingilia. Lakini sasa Bilal yuko na Mahmud Mnyimage ambaye hapo kabla alikuwa yuko na kina Jakaya kosa lake unalijua?

Huyu jamaa alikabidhiwa Brificase yenye milioni 200 kwa ajili ya kufanya kampeni za Jakaya ndani ya CCM, jamaa akasepa nalo.Akaenda kuimarisha Gereji yake pale sinza na kununua shamba Mbodole ikumbukwe kwamba huyu jamaa anamiliki nyumba pale Sinza madukani na ndiye aliyekuwa afisa usalama wa Mrema mwaka 1995 wakati Mrema alipokuwa anagombea Urais. Jakaya alipokuwa Rais Mnyimage aliwahi kufikishwa mahakamani kwa kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Unajua ilikuwaje?
 
unadhani ukitaja majina ya viongozi wakubwa ndo utatutsha sana tuseme unajua sana mambo ee!huna lolote wewe,story yako feki tu hii.uguza majeraha yako taratibu utapona.

Busara za hivi hata ubalozi wa nyumba kumi hupewi. Siku nyingine ukipinga pia toa hoja....kutumia nguvu tu hapa sio sehemu yake.
 
Hutaki unaacha! We do not want to listen to your handbag tantrums here, please madam!

'WE' wewe na shemeji yako? We hutaki acha...tuachie wenyewe tuunganishe dots....
 
Ukifikiria sana waweza kuwa chizi; nashangaa watu kama Mwanakijiji bado wako SANE. Mambo yanatisha, yanachanganya, yanachefua na mbaya zaidi yanakatisha tamaa.
 
Cha kufahamu nikwamba hawa jamaa CIA wako another level za intelijensia compared to TISS.Alafu, mipango ya CIA ni ya long run (e.g. 20 and above). Afu tukumbuke TISS, kimfumo wamechelewa kubadilika sana. Nchi yetu ilipoanza kuingia kwenye ubepari (kipindi cha mwinyi), TISS walikua wanashangaa shangaa tu. Hivi inawezekana vipi nchi inaingia kwenye mfumo wa soko huria afu mali zote zinakwapuliwa na wageni afu TISS wapo tu wanatoa macho?

Pia, mfumo wan chi unapokosewa (unapokua wrong), inachukua muda mrefu kuurekebisha, and it needs real expertsto do it with perfection, sio hawa watoto wa mafisadi waliojaa pale oyesterbayna dodoma. Afu tufahamu kuwa tupo kwenye imperialist world, kwa hiyo instrumentkama CIA ipo everywhere penye interest ya US.

Kimuundo hawa TISS bado wako nyuma. Afu usikute hata hizo computer zao plus servers walizopewa msaada kutoka kwa watu wa Marekani ziko monitored na hao CIA.
My friend don't ask the obvious, system ya maana kama mitambo ya intelligence wataacha kumonit wachekwe!!! Kama waliwafungia mitambo lazima kuna system ya kupata feed back!!!!!! Vile vile kuna employees wa hao wakubwa kwenye kilinge hicho!!!!

 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hussein Bashe katika style nyingine ya kumsafisha Rostam na kundi lake. TISS na serikali kamateni huyu achana na maneno haya ya mtaani CIA watamkuta gerezani. haingii akilini ni mpango wa vitisho vilivyotengenezwa kwa akili ya hali ya juu ili kumpa kinga RA.
Bashe hana lolote wa kukamata ni Boss wake Rostam Azizi atueleze habari za KAGODA, hao wakubwa zake wamkute kule Segerea lupango wamtoe huko, wacha kutubabaisha na matisho yasiyo na miguu!!!!!!!!!!!

 
huyu mtoto ni Imara kuliko viongozi wa pale Magogoni
398450_249130138493527_100001896272261_619405_319793181_n.jpg
 
Na mimi nakubali kwamba hili ni kundi la Hussein Bashe na Rostam Aziz baada ya kutumia magazeti yao wameona bado RA ni mchafu wameingia huku kujaribu kutupa karata ya mwisho. sitakubali kuingia kwenye kundi la abunwasi kukubali hadithi za kipofu kabahatika kuona.
Kweli ni hao hao kwanza watueleze fedha za KAGODA na EPA wamerudisha ngapi, au wamejigeuza SYMBION waendelee kutuibia kiaina? JK usitishwe na vibaka kamata wakileta za kuleta weka ndani wacha vitisho hapa!
 
Back
Top Bottom