Wana JF, hakuna haja ya kuwa na hofu yoyote juu ya CIA na RA, kwani hata wao CIA wana heshimu sana UMMA. CIA huwa wanakuwa na jeuri pale tu wanapopata vibaraka wa kuwapandikiza kwenye their strategic interest areas, haswa pale vibaraka hao wanapofanikiwa kuufanya UMMA ufyate kwa hofu. Vinginevyo, kwa miaka mingi sana, CIA walimlinda Mubarak pale Misri kwa sababu ya strategic interest ya Israel, lakini UMMA wa Misri ulipoamka, CIA ikamshauri Mubarak angatuke. Pia huko Afganistan, ni juzi tu CIA wamemshauri Kazai kumaliza tofauti zao na Taliban, huku Marekani ikisaidia kufanikisha hilo, baada ya CIA kugundua kwamba UMMA wa Taliban will only retreat, but will never surrender. MIfano ipo mingi sana.
Vijana, sisi tunaondoka. Lakini natoa wito kwa vijana kama nyie mliokuwa na upeo kuliko wenzenu wa mitaani na vijijini, waongozeni wenzenu kupigania nchi yenu. Lakini hadi sasa, ni wao huko Mbeya, Arusha, ndio wanaowangoza nyie, na kuwapa fikra kwamba kumbe inawezekana, wakati suala hili lilitakiwa liwe kinyume, kwa nyie kuwaongoza. Ebu jaribuni kuwaza iwapo vijana hawa wa Mbeya, Arusha na kwingineko watapata mwongozo na ushirikiano kidogo tu kutoka miongoni mwenu, si tutakuwa tunaongea majina ya RA, EL , kama ni historia? Lakini mjiandae kupoteza maisha ya baadhi miongoni mwenu, lakini hilo lisiwe kikwazo na lisiwatie hofu, kwani hiyo nayo ni sehemu ya mapambano. Vinginevyo, pamoja na ukweli kwamba JF inatikisa mpaka chumbani ikulu, na ina watu waliopewa kazi maalum kuifuatilia kila siku, na wapo kwenye pay roll za Ikulu kwa Salva Rweyemamu, TISS, na Ofisi ndogo ya CCM Lumumba kwa kazi hiyo tu. Vinginevyo furaha kubwa ya watawala wetu ni pale JF na nguvu yake kubwa, itakapoendelea kubakia kuwa ni kijiwe cha Soga, na sio jukwaa la vitendo vyenye lengo la kuleta mabadiliko.