Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Karume na Jussa ni wamoja na wanafahamiana vizuri sana kuliko wewe unavyofikiri. Kundi hili linao uwezo wa kuvunja Muungano muda wowote linaoutaka na kuanzisha serikali tatu na baada ya malengo kutimia likaanzisha serikali moja!. Ni vigumu kuelewa ni yapi majukumu ya Karume ndani ya hili kundi na nani kampa majukumu hayo na wapi kiburi cha Karume kimeegemea. Ni swala la historia ndefu sana ambayo nitaiunganisha vizuri baada ya kumchambua Rostam ambaye nitachukua muda mrefu kumchambua kuliko mwingine yeyote katika kundi hili.

Nafikiri urafiki wako na Karume waweza kuwa umeingia doa kipindi cha 2007 hivi wakati umeletewa zile briefcase zilizojaa dola na kumhukumu Karume kabla hujaenda uarabuni!. Hivi zile dola zilienda wapi Mh Rais?. Zilikuwa nyingi kwelikweli. Hata hivyo Karume anaweza kweli kusahau mchezo mliotaka kumfanyia wewe na Nahodha kuhusiana na mwafaka kabla ya kipindi chake kuisha na kupelekea kumtishia Nahodha nafasi yake ya Waziri Kiongozi? Nahodha akabaki analia wakati wewe umemruka tayari baada ya kuona umezidiwa nguvu?. Mr President, unawafahamu waliokuwa nyuma ya mchezo huu? Basi hao hao kwa miaka mingi wangekwishakumaliza lakini Edward alionekana "kukupenda'" zaidi na yeye amekuwa akiwawekea ngumu yaani kukulinda lakini kwa bahati mbaya sana, amewakubalia hivyo kufanya '‘game'' kuwa kali. Edward anaweza kukulinda baadaye. Lakini hutaweza kufanya biashara yeyote ile na waweza kubaki na "njaa" kali sana baada ya kustaafu. '‘Game'' hii ni hatari kwasababu lazima imuweke Karume kwenye nafasi za juu za uongozi wa taifa hili 2015. Mh Rais naomba umuulize Mama Maria Nyerere akwambie vitisho alivyopewa na Karume na Mkapa kuhusiana na mwanaye makongoro wakati wewe unaendesha kikao cha NEC. Hata hivyo ni vizuri ukajiuliza swali la kitoto kama hili: Je ni kwanini Karume na wenzake walikushinikiza sana umteue Tom Apson kuwa mbunge wao wakikudanganya kwamba Tom amefanya kazi nzuri ya kuiba siri za Apson na malecela na wengine? Think twice Jakaya!.

Mjomba mimi naona unajichanganya na kushindwa hata kujuwa kipi unakizungumza ili tujuwe? Ikiwa Amani na Jussa wanaweza kuvunja Muungano ?basi itakuwa hakuna tena Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Sikweli kuwa wakivunja Muungano kutakuwa na Serekali tatu ,itakuwa Muungano umevunjika na Jussa na Amani itakuwa wanaingia Tanganyika kwavisa kwa vile itakuwa ni nchi tafauti kama vile kabla ya Muungano wa Tanganyikana Zanzibar.

Hebu rekebisha sentesi yako ili tukufahamu?
 
WAPENDWA WANA JF, MNIVUMILIE KWA MPANGILIO MBOVU. NITAENDELEA NA ROSTAM KWA UPANA ZAIDI, THEN APSON, MKAPA, EDWARD NA OTHMAN
Sema usiogope sema......
 
RA kaanza kuchipua enzi za mkapa,akaota mapembe enzi za jk..
 
Duu!! Kwa maelezo hayo, idara ya usalama wa taifa ina kazi gani? Kama hii mijitu inajiingiza hapa nchini hakuna mtu wa kuwagusa... inaunda mitandao ndani ya ccm na serikali hakuwa wa kuwagusa... Sasa nchi hii inakuwaje chini ya nyang'au hawa ccm?

Idara ya usalama wa Taifa inaangalia chadema na kuongeza kura za CCM. FULL STOP
 
Acheni wasiwasi, hakuna ambacho kinasemwa hapa ambacho hakijulikani in the corridors of power za Tanzania.
Mwanakijiji, kama unayosema ni ya kweli, what is been done to solve these problem. Kwa jinsi nchi ilivyo hovyo, we are tempted to belive haya yote...
 
Siku Bush alotia mguu Tanzania ndio nilijua kiasi gani CIA wameingia TZ na nguvu ya Marekani kwetu.. Tuna ubalozi mkubwa wa Marekani Dar kuliko sehemu yoyote Afrika, wametujengea jengo la Usalama wa Taifa (eagle), Kigamboni mji mpya, Mbeya wana project ya Uranium na kadhalika haya yote hatuna sababu ya kujiuliza tuko upande gani wala kulalamika ati CIA wameingia. CIA agents wapo kabla na toka wakati wa Nyerere..

Jambo moja tu ambalo linanipa shaka ni RA kutumiwa na CIA kama agent wao.. Hili sidhani ila ukinambia RA ni agent wa Iran pengine yawezekana ila nashindwa ku connect dots za Iran na USA kuwa pamoja!. Kwa nini nasema hivyi, sii rahisi kabisa kumjua agent wa CIA na akijulikana humwondoa mapema sana na kumweka mwingine ama wengine maana sio mtu mmoja.

RA anaweza kuwa pandikizi la uongozi kwa maana yeye ndiye kashika mpini kutokana na kwamba Mfumo wa Utawala wa Tanzania ni tofauti sana na nchi nyingine ambazo Mwanasiasa (mwenye itikadi) ndiye mtawala wa nchi wakati Tanzania hatuna itikadi tena - hiyo imeisha wakati wa Nyerere bali mwenye fedha na umaarufu ndiye mshindi. CIA wanalijua hili na ndio maana wanatumia wafanya biashara zaidi kumbukeni list ya members wa Skull.. Siri ya CIA huwa hawajali kutambuliwa kwa pandikizi hata kidogo lakini sio agent..

Kitu kimoja tu nawaomba mkitilie maanani sana kwamba Afrika sasa hivi ni uwanja wa vita kubwa ya kiuchumi baina ya Marekani na China, (Americans hawataki China iwe supperpower based on economic muscle) hofu ya Marekani ni China hivyo hata ujio wa Mama Clinton umetokana na kutembelewa na viongozi wa China pamoja na ile Meli ya Kijeshi ilotia nanga kwetu..Kenda hadi zambia na lugha ni ile ile tujihadhari na Ukoloni maboleo wa China, kesi ya Ngedele mshtaka ni Nyani!..

Na kikubwa zaidi tunachotakiwa kufikiria na kupima ni kwamba hawa fahari wawili wanapambana uwanja ni Afrika watakao umia kina nani? - NYASI -
 
jamani ee nyie mnaompinga mwanzisha thread... jamaa kawaambia "hutaki unaacha", so why all the fuss? piga mbizi!

having said that however....panapofuka moto, moshi unawaka....right?
 
Story za huyu jamaa ni za kwenda kupigia soga kwenye vijiwe vya kahawa labda, zimejaa uzushi na exaggeration za hali ya juu lakini bahati mbaya sana ndio style ya maisha yetu wabongo toka huu mtandao wa kina kikwete uingie madarakani, Rostam na wenzake waliposhika hatamu za uongozi walinunua vyombo vyote vya habari na kuanzisha style ya kuongoza nchi kwa makala za dizaini hii kwenye magazeti, wakafanikiwa kutulemaza na sasa tumelemaa ndio mana watu kama hawa wanaoutumia mwanya huo kutuingizia mabo vichwani mwetu huku wakielewa mtanzania ukimuingizia jambo kichwani na akaliamini kulitoa ni kazi ngumu sana,jamaa anaonekana kufanikiwa kuwapata baadhi yetu humu lakini naamini hatawapata wote kwa wakati wote bali wachache kwa wakati wote au wote (kasoro mimi) kwa wakati fulani!Naelewa CIA wanavyoendesha operation zao,siwezi kuingizwa choo cha stendi kirahisi namna hii aisee!

mi sitaki na nimeamua kuuacha uongo na uzushi huu ulioandaliwa kwa utaalamu wa hali ya juu na mtu anaeijua kazi yake!tumsubiri yule jamaa yake "mtoa tetesi" nae aje na makala yake!


Swala ni hilo? What is the issue here? kwa nini watu wanfikiria kaundika makala za hivi na wetu wengi wanazikubali?
Jibu hiyo hoja, usiseme tu unajua CA wanavyofanya kazi. wanaanzia kwenye nchi isiyo na mwelekeo
 
Tom Apson si mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa haingii akilini kwamba angejua mambo ya msingi kupitia kwa baba yake eti tu kwa sababu ni mtoto wa aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Idara hiyo ndugu Apson. Tuwe makini na maneno ya mitaani

The ideas of the ruling class are the ruling ideas...

Watu huwa wanatawala na familia zao.
 
mkuu aliyekwambia rostam ni mtanzania ni nani?mtanzania hana guts za kucheza diliza kuuza nchi namna hiyo..huyu mtu sijui kama anashikika since USA are backing him...obama go to hell..

Not Obama my brother... he has less influence. Just remember, USA has institutions which are functioning properly.. Raisi ni symbol tu... the opposite is true.
 
Aiseee!.... Umerejea tena na pumba zako, Unachonishangaza ni kwamba huna point wala mpangilio katika uandishi wako. Hata hivyo unatimiza wajibu kama unavyotumwa.

What is your side of the story? We would like to read the other side of the coin...
 
kama ingekuwa movie ungepata mapato kidogo kazi yako haina mtiririko tangu part I. kuna kipindi umewahusisha baadhi ya wachezaji wa movie yako lakini hatujawaona wakiwa sehemu ya wachezaji kwenye DVD uliotuwekea kutazama mwishowe ukarukia wachezaji wapya ambao mwanzo hukuwataja na ndio umewapa maelezo marefu. shit

It is better than nothing. Final the puzzle will be opened....
By the way, why sorry?
 
Ukiona part II haina kile ambacho nilitarajia kwamba ingeziba mianya ya mapungufu ya part I ulitakiwa kumpelekea mtaalam wa uchambuzi kufanya editing na kukushauri.

Why you all the time? kwa nini hii story hunts you> Ipotezee... kama ni oumba just leave it, fanya ya maana zaidii
 
Tom apson mwenyewe alikuwa mwanamtandao hakuteuliwa kwa sababu ya nguvu ya baba yake hapo pia umekosea. Taarifa kama hizi uwe unaandika kwa makini kwa sababu tupo humu pia tunaofahamu ukweli kwa upande mwingine.

asante kwa kutujuza lakini epuka kuweka uwongo kwenye taarifa muhimu kama hii.

Interesting... but could not influence the game......
 
Back
Top Bottom