Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Nimesoma part 1 na II, mkuu wewe mwenye hii thread unachofanya ni hiki:-

a. Kutengeneza story za kufikirika kwamba RA ni hatari kuliko mtu yeyote mwingine ambaye ametuibia Tanzania; ni hatari kuliko Mkapa, EL, Mramba, Mwanyika, Chenge, Werema..kwanini umeamua kumchagua huyo tu hakuna zaidi ya chuki kwa wananchi wa Tanzania waislam..unataka ku-protray wrong concept kwamba in fact hawa wengine (wakristo) ni nafuu aliye mbaya zaidi RA..hatudanganyika kama ni wabaya ni wote on equal scale OK

b. Umetengeneza story kwamba nchi hii inaongozwa na wanamtandao na kwamba wana nguvu sana kupita serikali yenyewe; fine lakini ukweli ni kwamba story yako ni illusion tupu..ili kuonyesha kwamba serikali haina nguvu kupita hicho kikundi; hapa una taka ku-potray kwamba JK hawawezi hao watu wako above the law; na kama anaweza embu awachukulie hatua wrong perception; si kwamba watu hao hawana hatia kisheria vile vile ni kumtafutia ugomvi watu kwa umbea usio na maana

Nakusifu kwakuandika story ya kama ile iliypo kwenye bible ya cruci-fiction nzuri sana..
 
Hoja zako zina mkanganyiko ndugu yangu. Kuwa Agent wa CIA hakuhusiani na nguvu zako kwenye jamii iliyokuzunguka. Ukitaka kuijua CIA vizuri jiulize ni kwa nini inakusanya taarifa za chumi za nchi mbali mbali duniani, leo hii CIA wana taarifa zaidi za Tanzania kuliko hata idara yetu ya takwimu. Zakhia siyo tu RA hata Msaidizi wa Jakaya Omary Luwhavi alishawahi kumlamba. lakini Zakhia ana Impact gani kwenye maslahi ya RA, alisema ndiyo ndani ya CC, tangu aseme alichosema KIMETOKEA nini hadi sasa baada ya yeye kusema?
tatizo lako wewe mama unakurupuka sana ..
 
unataka kusema hutaki unaacha ndiye mtoa habari?

hawa watu hawafanani kimaandishi ila naweza sema wanafahamiana sana na wamejipanga kuwa wewe lipuka hivi then mtoa habari anakuja kufafanua, mtoa habari anaoneka zaidi km mzalendo flani hivi na anayewatia vijana nguvu badala yakutishika.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
kwa jinsi anavyoandika hasa ukiwa ulianza kuisoma ile thadhari aliyoileta hapa kumpa membe awe careful,huyu ni msomali wa nzega!najua aina ya uandishi na maneno anayopenda kuyatumia!

CIA kama wangetaka kumtumia mtu atleast siyo huyo hawana akili za kihivyo huwezi kutumia visible kufanya invisible things atleast hii ni common sense tu! Hao watu wako kwenye denial situation hawajui wafanye nini maana wako kwenye moto ambao waliuwasha kwaajili ya wengine kuungua bila kujua wao wenyewe ndiyo watakao kuwa roasted!
 
Tanzania is the 3rd leading recipient of development AID in the world behind Afghanistan and Iraq. T Tanzania is also 3rd leading Gold producer in the world, yet remains poor.

Although your points hit home well (very well indeed), there are some few corrections that are worth mentioning.

Tanzania is not the third leading World producer of Gold, but third leading in Africa, behind South Africa and Ghana. China, Australia and South Africa have been dominating the top three spots, while the other seven gold producing counties have been exchanging positions, every now and then, in the top ten league. Otherwise, top ten gold producing countries are:

1. China*
2. Australia*
3. South Africa*
4. USA*
5. Russia*
6. Peru*
7. Canada *
8. Indonesia*
9. Ghana
10. Uzbekistan

The top 8 (highlighted in RED) account for almost 70% of world's total gold production. Ghana, Uzbekistan, Tanzania, Argentina, Bolivia, Brazil, Chile, Colombia, Ghana Kazakhstan, Mali, Morocco, Mexico, Papua, Philippines and about 70 other gold producing countries – these countries combined, produce just over half of the production of the top eight countries (combined), in the list above.

And on the Development AID front, Tanzania is also not in the top three, but in the top ten. The the correct list is as follows:

1. Iraq
2. Afghanistan
3. Ethiopia
4. Occupied Palestinian territory
5. Viet Nam
6. Sudan
7. Tanzania
8. India
9. Bangladesh
10. Turkey

Notwithstanding, your point stands very well.
 
Atayeikomboa hii Nchi ni mwananchi,yaani mimi na wewe la tukikubali na kubweteka kwa ushawishi ama kutishwa kwa namna moja au nyingine ni kukiki dhahiri kwa hatuwezi kupambana na kupigania utaifa wetu kwa ujumla wake,basi na tuichukulie na kuifanya taarifa ya Ndugu HU kuwa chachu ya mapambano yetu juu ya udhalimu unaofanywa na serikali hii ya CCM na mashoga zake bila woga wala kutishwa na matendo yao kwani ni dhahiri hata wao wana hofu juu ya maisha yao na mali zao na ndio maana wengine miongoni mwao wanahamisha taratibu mitaji yako nje ya nchi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hoja zako zina mkanganyiko ndugu yangu. Kuwa Agent wa CIA hakuhusiani na nguvu zako kwenye jamii iliyokuzunguka. Ukitaka kuijua CIA vizuri jiulize ni kwa nini inakusanya taarifa za chumi za nchi mbali mbali duniani, leo hii CIA wana taarifa zaidi za Tanzania kuliko hata idara yetu ya takwimu. Zakhia siyo tu RA hata Msaidizi wa Jakaya Omary Luwhavi alishawahi kumlamba. lakini Zakhia ana Impact gani kwenye maslahi ya RA, alisema ndiyo ndani ya CC, tangu aseme alichosema KIMETOKEA nini hadi sasa baada ya yeye kusema?

unajikanganya mwenyewe kwa sababu umeshaingizwa kichwani vitu vya bwana HUTAKI UNAACHA,na ni ngumu kuvitoa au mtu kukubadilisha!nilichokuwa naki challenge ni upotoshaji wa kutaka kuonyesha kwamba eti rostam analolitaka huyo bwana mkubwa rostam liwe kwenye political arena ya nchi yetu linakua,ndio nikatoa huo mfano wa jimbo "lake" la igunga.

Kuhusu nini kimefanyika toka da zakhia amvae rostam kwenye cc(kitu ambacho hakikuwahi kutokea abadan kabla ya siku ile)ni Rostam kutoswa nec(zakhia bado yumo),na baadae Rostam kujivua gamba japo siku ile alimfuata zakia na kumtishia kwamba sijui atamfanya nini na nini,lakini hakuna hata kimoja kilichotokea!kama yote hayo huyatazami kama impact basi kuna kuna tatizo hapo!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Zakhia mwanzoni kabisa alionekana atakuja kuwa Iron Lady wa Tanzania kumbuka jinsi alivyodili na mafuriko ya Moshi (akiwa mkuu wa Wilaya) lakini kuna wakati huyu mama wakubwa "walimchezea" sana hadi ikawa hakuna jinsi bali kumwacha 'afunzwe' na dunia. Na maisha yake pale Chuo cha Ushirika Moshi hayakuwapendeza baadhi ya watu!!

hilo ndilo "faili" lake!!!aisee
 
mkuu basi hata uni pm kama huwezi taja watu hapa

Hamjui hata mmoja alikua anajisemea tu kutokana na habari labda aliyowahi kuisoma kwenye gazeti fulani akaiingiza kichwani kuitoa humo kichwani ndio issue!
 
I got my data from Visual Economics. An American organization unraveling complexities in financial data.


...."The top recipient of developmental aid is Iraq, with $9.115 billion in donations. Number two is Afghanistan, with $3.951 billion in donations received. Number three is Tanzania, with $2.811 billion received in donations"

The top DONOR of development AID to Tanzania according to this organization is the USA.

As for Tanzania being the 3rd leading gold producer in africa, true will correct that.
But wanted to mention Barrick gold as the TOP gold producer in the world.
 
Ed manake Edson na HU manake Hutaki Unaacha.Vipi umeona maadishi ya kichina.

ulichemka jamaa ndio akawa anakua alert kiaina kwamba sio HU bali ujumbe wako ulitaka kuuelekeza kwa mtoa tetesi/habari ambae ndio ulikua umemnukuu kwenye maandishi yako sio Hutaki unaacha ambae ni mleta thread,tukubali kukosolewa tunapokosea!
 
unajikanganya mwenyewe kwa sababu umeshaingizwa kichwani vitu vya bwana HUTAKI UNAACHA,na ni ngumu kuvitoa au mtu kukubadilisha!nilichokuwa naki challenge ni upotoshaji wa kutaka kuonyesha kwamba eti rostam analolitaka huyo bwana mkubwa rostam liwe kwenye political arena ya nchi yetu linakua,ndio nikatoa huo mfano wa jimbo "lake" la igunga.

Kuhusu nini kimefanyika toka da zakhia amvae rostam kwenye cc(kitu ambacho hakikuwahi kutokea abadan kabla ya siku ile)ni Rostam kutoswa nec(zakhia bado yumo),na baadae Rostam kujivua gamba japo siku ile alimfuata zakia na kumtishia kwamba sijui atamfanya nini na nini,lakini hakuna hata kimoja kilichotokea!kama yote hayo huyatazami kama impact basi kuna kuna tatizo hapo!
Mmhhh yangu macho...nashuhudia makubwa ya dunia hii..
 
Swala ni hilo? What is the issue here? kwa nini watu wanfikiria kaundika makala za hivi na wetu wengi wanazikubali?
Jibu hiyo hoja, usiseme tu unajua CA wanavyofanya kazi. wanaanzia kwenye nchi isiyo na mwelekeo

Je na KIKWETE nae ni Agent wa CIA????????????????hebu soma hapo habari hiyo hapo chini kwa makini then "upime" kabla ya "kupiga mbizi"!!

Ni taarifa za WikiLeaks JK Adaiwa na wamarekani kumuogopa CDF waitara..


jk7.jpg




RAIS Jakaya Kikwete amezidi kuandamwa. Sasa anaitwa “dhaifu na anayetishwa na wasaidizi wake.”
Mtandao wa WikiLeaks unaoibua taarifa za siri za kibalozi duniani, umeandika kuwa Rais Kikwete aliwahi kumwogopa mkuu wake wa majeshi, Jenerali Mwita Waitara.
Kinachoitwa udhaifu wake ni hatua ya kukatalia Marekani kuweka nchini kituo cha majeshi ya ushirikiano – Africa Contingency Operations Training Assistance (ACOTA).
Taarifa zinasema Kikwete alighairi ahadi yake ya kuwa na mradi huo kwa kuwa ulikuwa ukipingwa na Jenerali Waitara.
Rais Kikwete anaelezwa kuwa alikuwa amekubali, mara baada ya kuingia madarakani Desemba 2005, mpango huo wa Marekani unaodaiwa ungesaidia wanajeshi wa Tanzania kupata mafunzo ya kulinda amani katika ukanda wa Afrika na serikali kunufaika kwa misaada kifedha.
WikiLeaks inamnukuu aliyekuwa balozi wa Marekani nchini, Michael Retzer akisema kukwama kwa mpango huo kulitokana na Jenerali Waitara “kuuwekea ngumu.”
Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja baada ya Balozi Retzer kunukuliwa na mtandao huo akisema Rais Kikwete, alilipiwa na Ali Albwardy, raia wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) nauli ya kwenda Uingereza na kurudi.
Alinukuliwa akisema pia kuwa Rais Kikwete “aliwezeshwa” kiasi cha dola milioni moja za Kimarekani (sawa na Sh. 1.6 bilioni), kwa ajili ya shughuli za kutafuta urais mwaka 2005.
Ali Albawardy, ambaye ni mmiliki wa hoteli maarufu jijini Dar es Salaam, Kilimanjaro-Kempinski.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu alikana madai hayo akisema, “Rais Kikwete hakuwa akikusanya fedha” za chama chake.
Ikulu ilimwita Balozi Rezter mzushi, muongo na ikasema Rais Kikwete hajawahi kufadhiliwa na bilionea mmiliki wa Kilimanjaro-Kempinski.
Taarifa zinamnukuu Balozi Retzer akisema utawala wa Kikwete ulikuwa unapitia katika wakati mgumu kati ya raia na jeshi, kutokana na hatua ya mkuu wa majeshi “kuzuia” rais na waziri wa ulinzi kuchukua hatua ya kuanzishwa kwa mafunzo hayo.
Hata hivyo, Balozi Retzer anasema, “Lakini hatukukata tamaa kwa kuwa mkuu wa majeshi alikuwa anakaribia kustaafu, 31 Julai 2006 na Rais Kikwete aliahidi kuanzishwa mafunzo hayo baada ya Waitara kuondoka.”
WikiLeaks inasema tarehe 2 Mei 2006, aliyekuwa waziri wa ulinzi, Profesa Juma Kapuya aliomba kukutana na balozi ambapo aliomba radhi kwa kucheleweshwa mafunzo hayo.
Profesa Kapuya amenukuliwa akimhakikishia Balozi Retzer kwamba mafunzo ya ACOTA yangeanza muda wowote baada ya Waitara kustaafu.
“Kama ilivyodhaniwa, utawala wa Kikwete unakumbana na mvutano wa kiraia na kijeshi. Mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania anazuia rais na waziri wa ulinzi kuchukua hatua ya kuanzisha mafunzo ya kulinda amani chini ya (ACOTA),” linaeleza WikiLeaks, likinukuu Balozi Retzer.
Balozi ananukuliwa akisema mafunzo hayo yalilenga “kufundisha vikosi vitatu vya kulinda amani ifikapo 2008, mafunzo ya kwanza yakiwa yamepangwa kufanyika Machi 2007.”
Hadi Mei 2007, mafunzo hayo yalikuwa bado hayajaanza na Balozi Rezter ananukuliwa akisema, “…ni muhimu kuelewa kwamba Jenerali Waitara anakumbatia sera za ulinzi za kijamaa na amekuwa akizuia uhusiano wa karibu wa kijeshi na Marekani kwa kupendelea Uchina na nchi nyingine za kijamaa.”
Kwa upande wake, Profesa Kapuya ananukuliwa akieleza Balozi Retzer, jinsi Rais Kikwete alivyoweka msimamo wake katika suala hilo, tangu 3 Machi 2006 wakati wa ziara ya Naibu Kamanda wa Marekani katika Muungano wa Ulaya, Jenerali William Ward.
“Kikwete alisisitiza nia yake ya dhati ya kuunga mkono shughuli za mafunzo hayo…mbele ya wakuu wake wa jeshi. Lakini sasa kuna mkanganyiko kuhusiana na ucheleweshaji huu,” Kapuya ananukuliwa akisema.
Anasema, “Tunajaribu kuzuia mgongano na CDF (Mkuu wa Majeshi) na kuvuta muda wa kama miezi miwili hadi mitatu – ili tuzuie mgongano huo usiweze kutokea."
Kwa shabaha ya kueleweka vema, Kapuya anamwambia balozi, “…tunajaribu kueleza hali halisi ilivyo ili utuelewe. Tupo katika hali mbaya sana. Tunaomba msamaha kwa ucheleweshaji huo na tunakuomba utusaidie kutoa maelezo haya nchini kwako.”
“Kwa dhati tupo tayari kuunga mkono jitahada za mafunzo haya ya kulinda amani nchini, na hatupendi kuona ucheleweshaji huu unaharibu uhusiano wetu mzuri uliopo,” anaeleza Profesa Kapuya katika hali ya kubembeleza.
Mtandao unamnukuu Balozi Retzer akimhakikishia Profesa Kapuya kuwa wanaelewa madhumuni ya serikali ya kuunga mkono mafunzo hayo pamoja na changamoto zinazomkumba rais na waziri wake wa ulinzi.
Balozi Retzer alisema anautambua mkanganyiko huo ulioanzishwa na Jenerali Waitara, na hivyo akamshauri Profesa kuruhusu mafunzo hayo kuanza kabla ya makubaliano kufungwa.
Mpaka sasa, ubalozi wa Marekani nchini haujakana maelezo ya Balozi Retzer, jambo ambalo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, linathibitisha kilichoandikwa na WikiLeaks.
“Hizi tuhuma dhidi ya Kikwete, bila shaka zina ukweli. Vinginevyo ubalozi wa Marekani ungekuwa tayari umetoa taarifa ya kujitetea kwa sababu anayelipua jipu hili bichi ni aliyekuwa balozi wake hapa nchini, na hii ni tuhuma kati ya nchi na nchi na siyo Balozi Rezter na Kikwete,” anaeleza kiongozi mmoja mwandamizi serikalini kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.
WikiLeaks inamnukuu balozi akisema, Profesa Kapuya, akikubaliana naye kuhusu kuanza mafunzo kabla ya makubaliano, alitikisa kichwa na kisha kusema, "Tunaelewa hayo. Kila mmoja wetu anaelewa haya, kwamba hatukuhitaji makubaliano ili tuendelee na ACOTA. Lakini ni salama kusema, tunaweza kuanza mafunzo haya ifikapo Agosti 2007."
Akijibu maelezo hayo, Balozi Retzer alisema, “Rais Kikwete alitamka hadharani msimamo wake huu wa kuunga mkono mafunzo haya ya ACOTA. Lakini hivi sasa, anaangushwa na wakuu wa jeshi.
“Najua Rais Kikwete amepiga hesabu zake za haraka ambazo hata sisi tunakubaliana nazo. Lakini wasiwasi wangu, ni jinsi anavyoshindwa kusimamia ahadi zake,” mtandao unamnukuu balozi akisema.
Mchakato huu ulianza wakati Dk. Asha-Rose Migiro akiwa waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa. Balozi pia alirejea kukumbusha ahadi ya Kikwete wakati alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa sasa, Bernard Membe.
Katika hatua nyingine, WikiLeaks linasema, mara baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani, alimuomba Balozi Rezter kumsaidai kupeleka wasaidizi wake wawili wa karibu kupata mafunzo nchini Marekani.
Katika ombi hilo, Kikwete aliwataja wasaidizi wake hao wawili kuwa ni January Makamba, ambaye sasa ni mbunge wa Bumbuli na David Jairo ambaye ni katibu mkuu Nishati na Madini aliyesimamishwa kazi.
Balozi Rezter alikubali na kumuahidi rais kuwa atafanya mawasiliano na serikali yake na hatimaye kuanza utaratibu ya mafunzo hayo kwa Januari na Jairo nchini humo.
Gazeti hili halikufanikiwa juzi kuthibitisha iwapo Makamba na Jairo walipata mafunzo hayo nchini Marekani.
Aidha, taarifa ya ikulu wiki iliyopita, ilisema Rais Kikwete alikataa ujenzi wa hoteli katika mbuga za wanyama za Ngorongoro, ikiwa na maana ya kuonyesha kutokuwepo uhusiano kati yake na Ali Albawardy.
Lakini taarifa haikusema lolote juu ya hoteli katika mbuga za Serengeti ambayo ilifunguliwa rasmi na Rais Kikwete. Hoteli hiyo inaitwa Bilila Lodge Kempinski. Ilifunguliwa tarehe 10 Julai 2009.
Katika hutuba yake ya ufunguzi, Kikwete alisema, “Najisikia kupewa heshima kubwa na upendeleo katika kushuhudia tendo hili la kihistoria la ufunguzi wa Bilila Lodge ambayo ni mojawapo ya hoteli za Kempinski.
“Nakushukuru Bw. Reto Witter, rais na mtendaji mkuu wa hoteli za Kempinski, Bw. Ali Albawardy, mwenyekiti wa ASB Tanzania Limited na Bw. Hasu Masrani mkurugenzi wa ASB Tanzania Limited kwa mwaliko huu.
“Nina mapenzi ya dhati kwa Serengeti, lakini Bilila Lodge imekamilisha uhondo na starehe pamoja na uzuri wa Serengeti. Nakushukuru sana Bw. Ali Albawardy kwa uamuzi wako wa kujenga hoteli hii ya kifahari hapa Serengeti na katika ardhi ya Tanzania,” alieleza Rais Kikwete.
https://www.jamiiforums.com/toleo/259
 
Hii nasikia ni kweli na wakati ule SHIMBO alipokutwa na TRILIONI KADHAA nasikia alipoona KIKWETE hataki kumchukulia hatua SHEMEJI yake jamaa alienda kwao na alisusa kila kitu na amini usiamini NCHI hali ilikuwa tete na ni mwezi uliopita tu STAND BY imeisha kwani jamaa haeleweki na wana JERSHI wana muunga mkono na ku mkubali sana MWAMUNYANGE.

Duu!kwa hiyo alisusa?!!!kama hiyo ni kweli basi mwamunyange atakua ndio mkuu wamajeshi "muoga" kuliko wote kupata kutokea hapa tanzania!tulipata kusikia simulizi za wakuu wa majeshi kipindi cha mwinyi na hata kipindi cha mkapa mwishoni wakiwadindishia ma amiri jeshi wakuu hao,sasa huyu kukimbilia kijijini inatuonesha nini?ana muogopa kikwete si ndio?
 
Umesema vyema mkuu,Jeshini hakuna dharau kwa mkubwa ni heshima kwenda mbele hata kama umemzidi elimu.Haya mambo tuyachambue kwa umakini.Tuchuje pumba na kuziweka pembeni ili tubaki na ngano safi itakayotusaidia kusonga mbele.

Lakini kusema ukweli kwa miaka ya hivi karibuni TISS imeonyesha udhaifu mkubwa tangu kuondoka kwa marehemu Imran Kombe.At least alionyesha umahiri wa kuiongoza idara hii muhimu kwa usalama wa Taifa letu.Waliofuata baadae ni kama JK wameonyesha udhaifu mkubwa wa Uongozi mpaka sasa tunaingiliwa na maajent wengine mpaka jikoni.

Ufike wakati tuseme imetosha na tuiboreshe Idara hii kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.RA na EL na genge lao ni watu wa chache sana kusumbua akili zetu.
.........ndugu yangu bongo hii kila mtu siku hizi ni mganga njaa, hebu jiulize uzalendo tuiliokuwa nao kama taifa umepotelea wapi!!! katika mabadiliko ya uzamadamu, pengine hapa tulipo ni hatua mbaya zaidi na tuombe tubadilike haraka kwenda hatua ya mbele pengine yaweza kuwa productive, vinginevyo tumekuwa kama mizinja-thropus matendo ya akili zetu
 
Yaelekea CIA inawatu wengi ndani ya sirikali ya TZ. Ni hatari!
 
Back
Top Bottom