Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)


hawa watu wanatia aibu mno
mimi niliposikia Mwakyembe kapata ajali mwanzo na maelezo hayafanani
nilishangaa sana,sasa unasikia kalishwa polonium na wao wapo tu.....

wao pekee ndo wenye 'license to assassinate' hapa nchini....

sasa wanatokaje watu nje kuja 'kuinngilia territory' yao tena twice na wao wasi react?????

Huwezi ingia Marekani ukajaribu 'kumshughulikia mtu' twice na pasiwepo na reaction ya vyombo vya usalama

hata kama huyo mtu 'hapendwi' na watawala.......
 
Vitendo na matukio yanayomhusu yakiunganishwa na "ukitaka uanaacha" yanaleta jibu kuwa tuendako ni hatari kwelikweli, sijui nani ataweza kusimama mbele ya mtandao huu na kuuzuia kuleta madhara kwa taifa letu. Lo mbona tumekwisha!!!
 


Hata mimi tokea part 1 nilishasema haya ni mazingaombwe................... kuna jamaa walinijia juu. Nafikikiri umetumia neno zuri thamthilia. Ujaribu kuunganisha dots, utagundua kuwa hizi ni story za mtaani jamaa kajaribu kuziungaunga na diyo sababu hazina mtiririko mzuri. Kwa upande mwingine ukiangalia maandiko yake ya part 1, part 2 na hiyo uliyoileta ya Membe, utaona kuwa jamaa anajicontradict mwenyewe. So far, it does not make much sense............ atleast to me!!
 
Mkuu Mtazamo huyu Rais wetu hata akijua hayo yote ni mbishi, labda anabuy time muda uishe au anakubaliana iwe hivyo sijui ni kwa maslahi ya nani???????????? Bali si kwa maslahi ya Tanzania niipendayo!!!!!!!!!!!

 

Uwa naumia sana na upata shida sana kujiuliza hivi zama za Mwalimu Intellectuals ambao ndio Intellegency Unity ya wakati huo mbona walikuwa waelevu kiasi kuwa inaonekana Marekani na ubabe wake walituheshimu sana na hata kuna yule agent wao wakati fulani aliweka makazi yake Zanzibar, Mwalimu aliwaagiza wakubwa zake huko USA wamtoe haraka.Na kwa ombi lile la Mwalimu walijua dhahili atolewe vinginevyo watamkuta kwenye makolongo ya Mbuga za Wanyama gari lake limegongwa na faru akitizama wanyama.

Hiyo ni moja ya heshima ya Watanzania kuwa chombo chako cha ulinzi kinaheshimika na watu wa mataifa.Ni sawa na kuwa na baba Mwenye Bastora nyumbani kidogo mama na watoto wanalala na amani kuwa baba anae msaidizi wa ulinzi.Na hakika enzi ya Mwalimu Usalama ule ulikuwa ni Baba analinda familia yake kwa Rocket Ranger.

Hakika wapo wapo tena mbaya mtaaluma,kiongozi, anapeendwa na umma,japo viongozi awampendi, alipaswa kulindwa kwa gharama yoyote hapo ndipo ikibidi watu kufa kuonyesha uzarendo kwa Taifa basi ilibidi hayo yafanyike.Lakini leo watu wanamcheki jamaa wanaingia Nchini wanapiga mission zao wahusika wanatimiza yao ya kumdhuru, walinzi nao kimya mitaani tunasema yanageuzwa kivyake ilikuwa kiherere chake mhusika.

Kiherere mtu anajaribu kuangalia reality jamani dhidi ya maisha yetu.Hata watetezi wa mwisho Usalama ambao ndio kimbilio nao wanamtosa jamani hata kwa Mungu na Mizimu ya Mababu wa Kiafrika hiyo sio sawa hata kidogo.Ila kanuni kubwa ya usaliti ya What goes around comes around itwaludi tu wale wote waliokuwa na dhamana ya kumlinda mpewa sumu na hawakufanya hivyo wakawaacha jamaa wapige mission yao ndani ya ardhi ya mtoto wa Nchi, Mungu hana likizo, japo nae alishiriki kuifadhi vitu ambavyo angevisema wakati huo historia ingekuwa nyingine."

Unayosema Boss tunatatizo kubwa sana na la msingi kwa kuwa the Court Break became the Court Breaker.Tunaitaji mageuzi makubwa na ya kutisha sana ndani ya taasisi hiyo muhimu na nyeti kwa Taifa.Nina hakika pamoja na kuwa CIA Kitaasisi ni wazuri lakini Watanzania kwa kila mmoja mmoja kwenye usalama wetu kwa sasa ni Best.

Ni jukumu la kupata mtu makini akashughurika kurestructure Instutional nzima na kufanya reform ya aina yake na kuakikisha wale wote best wanaform instutitional mpya tena isiyoegemea upande wowote.Na kufrash uchafu wote unahusiana na mapandikizi ndani ya mfumo huo wa usalama.

Hakika Tanzania ya Neema ya Maziwa na Asari wataiona kwa kuwa cake yao kwa sasa inaliwa na wageni, chini ya kivuli cha wanasiasa wasiojua ama wanajua kinachoendelea na baadhi ya Mapandikizi uchwara.
 
mimi hawa TISS ndo wananishangaza kupita kiasi; ni sawa wewe uwe refa wa mechi, halafu aje mtu uwanjani na filimbi apige filimbi na kutoa penati, na wewe bado unajiita refa.....hiyo ni kukubali dharau ya kiasi gani...

Watu wanaingia ndani ya nchi kufanya shughuli ambazo ni TISS tu wenye 'vibali halali' vya kufanya....na still wanaweza kusema wako 'in charge'?
 
Sasa kama chadema watachukua nchi 2015 hali itakuwaje? Hawa jamaa wataenda wapi?

Watasepa au wajinyonge kukimbia mkono wa sheria! Lakini la ukweli hawa jamaa wa USA and allies wanatabia ya kusoma vizuri alama za nyakati wataanza kunyumbulika kama Camilion ili waendane na wakati. Watawatosa wote watakao kuwa threat kwa maslahi ya nchi zao, American interest come first above anything alisema Presida Obama wakati fulani!
 
kuna siku mshikaji mmoja wa mwalimu airport alinidokeza kuwa, kwa siku raia wanaofanya safari zao za kuingia na kutoka 60% ni wamarekani, yaan hata watz hatuon ndan, sasa mnasubiri nini, bora mie nijitafutie uraia wa msumbiji, Huku serikali inajali wananchi wake sana zaidi ya sisi, kwa mfano ukitaka mikopo iko Nje Nje kwa raia wao, sema shule ndo hawana
 
Leo mnatuambia eti fisadi Rostam Azizi ni CIA kwa maana ya agent kwa hiyo siku hizi CIA wanakumbatia mafisadi?
Hivi kuna ujabu gani kwa CIA kukumbatia mafisadi? Hivi wewe unazungumzia "Central Intelligence Agency" ya marekani au unazungumzia kitu kingine? Hawa jamaa si ndiyo walikuw wanawasaidia Makaburu wa Afrika Kusini dhidi ya wazalendo. Siyo hawa waliokuwa wanamshabikia na kumpa misaada ya Kijeshi Savimbi. Hao wengine ukiwalinganisha matendo yao na RA si RA ataibuka "mtakatifu"?
 
Ukiona part II haina kile ambacho nilitarajia kwamba ingeziba mianya ya mapungufu ya part I ulitakiwa kumpelekea mtaalam wa uchambuzi kufanya editing na kukushauri.

Hivi maana ya kuwa GT ni nini? Kwa nini usifanye hiyo uchambuzi ww mwenyewe?
 
ndo maana serikali ilwaambia kuna mafisadi wengine hawakamatiki, wakikamatwa nchi ita tetereka. Mia

Kidogo sasa hili inaingia akilini. But kwani Tz ni ya wamarekani?. Tutawakamata tu one day,no matter how, hata kama wana back up ya CIA yao
 
Hoja zako zina mkanganyiko ndugu yangu. Kuwa Agent wa CIA hakuhusiani na nguvu zako kwenye jamii iliyokuzunguka. Ukitaka kuijua CIA vizuri jiulize ni kwa nini inakusanya taarifa za chumi za nchi mbali mbali duniani, leo hii CIA wana taarifa zaidi za Tanzania kuliko hata idara yetu ya takwimu. Zakhia siyo tu RA hata Msaidizi wa Jakaya Omary Luwhavi alishawahi kumlamba. lakini Zakhia ana Impact gani kwenye maslahi ya RA, alisema ndiyo ndani ya CC, tangu aseme alichosema KIMETOKEA nini hadi sasa baada ya yeye kusema?
 

Nakumbuka kwenye issue ya Mwakyembe humu ndani wengine tulisema hivi TISS inajiskiaje pale wananchi wapowashilikisha kuwa ni wauaji.Mbaya sana watuwenyewe maskini hawakushiriki kwenye matendo hayo, japo wana lesni hiyo.

Ni aibu kweli kwa taasisi yetu hiyo ni sawa na Mwanaume mwingine anakuja nyumbani kuzengea mkeo nae unamwangalia japo hata kama ni wale vidume mabouncer wanyanyua chuma, na wewe ni mbavu za mbwa kachoka,utamvizia njiania anatoka clabu usiku kwenye kazi zake za ubouncer basi unajipanga na vitofa na nondo zako kaza unamtangulizia vitofa vya mbavuni kisha unamtuliza na nondo za Mabegani uku ukitoa ujumbe kuwa ukimuona kwa mkeo unammaliza.

Jamani wapewa sumu ndani ya ardhi yetu ni ndugu zetu jamaa zetu, viongozi wetu, marafiki zetu na hata kama wameingia maslahi ya baadhi ya wenzetu bado hiyo sio haki kupewa sumu.Kuna baadhi ya vigogo kibao sana wamekoswa koswa na kwenda kwa sumu hizo lakini hawasemi tunayasikia mitaani.Please TISS haya mambo yako mikononi mwao wanauwezo mkubwa tu wa kuyavunja tufike mwisho wananchi wajadiliane maendeleo sio hizi sarakasi tunazochezeshwa na third part.
 
Kidogo sasa hili inaingia akilini. But kwani Tz ni ya wamarekani?. Tutawakamata tu one day,no matter how, hata kama wana back up ya CIA yao
Unajua ni kwa nini Ufaransa ilitoa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kuwezesha shule zinazomilikiwa na Jeshi zifundishe Kifaransa kama somo la ziada? Usiiangalie Tanzania kama nchi iangalie Tanzania kama nchi iliyo kwenye eneo la Kimkakati kwenye nchi za Maziwa makuu. Watu hawajiulizi kwa nini Museveni walikuwa hawaivi na Kagame lakini mwishoni mwa mwaka jana Kagame alikuwa Uganda kwa mapumziko.

Kwa nini Odinga ana uhusiano wa karibu na Magufuli na kwa nini Nyalandu ndiyo Kete ya USA kwenye Urais wa Tanzania? Gharib Bilal alikuwa hana mahusiano mzuri na Jakaya kwa nini Jakaya alikubali kumteua Gharib wakati 2005 Bilal aliondoka Dodoma usiku kurudi Zanzibar baada ya kutemwa na CC ya CCM bila ya Msaada wa Jakaya na kundi lake?
 
Changanya kidogo na akili yako...sio kuingiza kichwani kila kitu,2015 toka sasa ni mbali sana,utakiover work kichwa chako kakaangu maana yataletwa mengi humu
Dossier ndogo namna hii ndiyo ita - over work akili ya mtu. watu tunasoma kurasa zaidi ya 500 na bado tupo tupo!!
 
Jamani kuwa great thinker ni pamoja na kuokota mauza uza na kuyageuza kuwa bidhaa yenye bei sokoni. Sasa kuna watu wanataka kila kitu kiwe "rahisi" tu kueleweka. Tuunganishe na thread zingine zilizowahi kutoka humu ndani na kisha unachambua na unaachana na makapi unatoka na kitu kamili!
 
Gen Davis Mwamunyange JKT ilikuwa kazi kama kazi zingine za kijeshi, yeye Davis ni wa JWTZ toka kitengo nyeti, na jeshini hakuna dharau kwa mkubwa mengine ni uzushi tuu!!!!!!!!!!

 

na huyo Zakhia
faili lake likoje?
nasikia sikia tu
sijui kipi ukweli kipi uwongo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…