Kuna mambo mawili au zaidi lazima uyaangalie sio tu hizo statistic
1) Unaangalia kukua kwa uchumi kwa kulinganisha Tanzania na nchi zengine lazima uangalie kama hizo nchi zengine chumi zake zimekuaa pia au zilikua zime stop kukua na hata kama zimekuaa ni kwa rate gani?
Mimi naamini hizo nchi zilizo linganishwa na Tanzania chumi zake zimekuaa kwa niwango kidogo sana au hazijakuaa kabisa
2)Kikwete haja fanya lolote la kukuza uchumi wewe mkuu just tutajie mawili tu aliyofanya ambayo yana result to the long term economic growth,
3)Fahamu ya kuua mambo yote unayoyaona sasa YA KIMAENDELEO hapa Tanzania yanatufuta machozi ni mikakati ya Mkapa
kikwete hajafanya kitu na hatafanya hata moja sio kwamba hataki kufanya HAJUI afanye nini
Hilo swala No 1, ungelijibu wewe kwa kuangalia Nigeria, Kenya na Uganda zilikuwaje huko nyuma. Mimi nimelinganisha Tanzania 2005(alipokabidhiwa Urais Kikwete) mpaka 2008. Msipende kulishwa kwa vijiko, wakati ule wa ujamaa umekwisha sasa ni wakati wa kutumia akili yako usisubiri Zawadi Ngoda akuandikie kila kitu. Kifupi nchi zote hizo uchumi wake umekua lakini si kwa mwendokasi wa Bongo. Umekua kwa ongezeko gani, nawe fanya kazi na chemsha bongo.
Swali No 2 umeomba nikutajia mambo 2 aliyofanya JK kukuza uchumi.
1. Leo tunakutana hapa nakutoa mawazo yetu waziwazi kama alivyoeleza mtoa hoja # Lole Gwakisa. Sikudanganyi, nisingethubutu kuwa muwazi kiasi hiki toka awamu ya 1 mpaka ya 3. Kama Tanzania imepata ufunguo ndio huu, maana hata bubu leo aweza kusema.
Tumeanza kuzijua wapi skendo za EPA, Richmond, Rada na mikataba mbalimbali. Haya yote yalianza kutoka kwenye magazeti na mitandao. Hata Dr Slaa akitoboa ubadhilifu na kunuu habari za kwenye mtandao. Uhuru wa habari ndio uliowapa kufahamu watanzania wote kuwa kumbe Serikalini kuna mambo.
Mikataba iliwekwa wakati wa Mkapa sasa nyie wenye magazeti mlikuwa wapi kusema toka kuanza mazungumzo ya mikataba mpaka inasainiwa? Mlinyimwa haki ya kupata habari, na hata mkipata basi muandishi atakiona kama akiandika habari hiyo. Haya yalikuwa jana tu, eti mnataka kusema kuwa mmeshasahau? Acheni kuwa wepesi wa kusahau.
Nakumbuka wakati wa Nyerere, alilifungia gazeti la New African, eti kwa sababu liliandika 1/4 ukurasa habara juu ya mali zake. Leo hii gazeti la kitanzania linajaza kurasa mbili kuelezea ubadhilifu wa Rais japo ni wa kutunga tu. Lakini Rais anawaachia tu akijua hawa ndio kwanza wanaanza kuutumia uhuru wa kusema.
Sasa usijeukaniuliza, hivi uhuru wa kusema unakuzaje uchumi? Hapo utanivunja mbavu!!
2.Kutokomeza ujambazi. Huwezi kufanya biashara na kukimbia huku na kule kita wawekezaji kama usalama wao na mali zao ziko hatarini. Mabenki ndio yalikuwa kichumo No 1 cha majambazi. Muulize mwanauchumi yeyote yule umuhimu wa mabenki katika kukuza uchumi. Na omba Takwimu ujue kiasi gani cha pesa kilichukuliwa na majambazi wakati wa Mkapa? Ukilijua hilo utakua mjinga kama hukumsifu Kikwete.
Leo watu tunalala kwa amani, jamani tulikuwa hatupati usingizi kama una kajumba kadogo kazuri na vitu viwili vitatu ndani. Mlinzi hata wa bunduki alikuwa hafai, maana wale walikuwa profesionals wakija na silaha nzito. Wenyewe tulikuwa tukiwaita kama watoto wa "Mahita" waliopata baraka za Mkapa. Pengine wenzetu mnaandika toka Ughaibuni ambako mmeshasahau neno majambazi
Samahani uliniomba sababu 2 tu lakini niruhusu nikupe hii ya 3.
3. Kudumisha imani kwa nchi jirani kwetu. Amini usiamini wakatia wa Mkapa kidogo tuingie vitani kati yetu na Rwanda. Kagame alishasogeza majeshi yake mpakani. Mkapa akataka kuonyesha kuwa Tanzania ni super power wa Afrika Mashariki. Kama si umoja wa mataifa basi yale ya 1979 yangetufika. Si kama hayo hayatoshi, uhusiano wetu na Kenya ulikuwa mbovu kama wakati wa Nyerere. Wakati huo Tanzania ikaishutumu Kenya kwa kuwasaidia eti waasi wa Pemba kuleta vurugu Pemba na eti kutaka kuanzisha vita huko. Dhambi kubwa ya Kenya ilikuwa ni kupokea wakimbizi wa Kitanzania, tulisahau kuwa sisi wenyewe ndio wasaidiaji wakubwa wa wakimbnizi toka nchi jirani zenye vita. Kwa mara nyingine tena tukasuluhishwa na Umoja wa mataifa.
Uhusiano na nchi jirani ni muhimu sana katika kukuza uchumi endelevu, na ninafikiri hakuta kuja mwendawazimu mwingine asiyeelewa hili.
Hoja yako ya 3. Eti yote yamefanywa na Mkapa. Ngoja nikupe semi mbili zikusaidie katika maisha yako: Ni ngumu sana kujenga, lakini ni rahisi sana kubomoa. Mwingine: Watu maarufu husema, ni rahisi zaidi kujitahidi mpaka kufika kileleni, lakini kubaki huko kileleni ndio ngumu zaidi.
Semi hizo zote zina lengo la kukueleza kuwa, hebu tukubali kuwa Mkapa ndio aliyofanya kazi. Amini na kwambia kama Hata Mkapa alitengeneza, kwa miaka mitatu ingetosha kwa Kikwete kuharibu kabisa uchumi. Na kama ameweza kubaki huko juu alikokuacha Mkapa na kuongeza basi Kikwete ni shujaa.
Usipoamini maneno yangu, Muulize Clinton alichofanya na kusifiwa na Kile alichofanya Bush. Utasema si kosa lake, ndio majibu yenu pindi umpendaye anapoboronga.