Kikwete kainua uchumi wa Tanzania

Kikwete kainua uchumi wa Tanzania

Kuna mambo mawili au zaidi lazima uyaangalie sio tu hizo statistic

1) Unaangalia kukua kwa uchumi kwa kulinganisha Tanzania na nchi zengine lazima uangalie kama hizo nchi zengine chumi zake zimekuaa pia au zilikua zime stop kukua na hata kama zimekuaa ni kwa rate gani?
Mimi naamini hizo nchi zilizo linganishwa na Tanzania chumi zake zimekuaa kwa niwango kidogo sana au hazijakuaa kabisa

2)Kikwete haja fanya lolote la kukuza uchumi wewe mkuu just tutajie mawili tu aliyofanya ambayo yana result to the long term economic growth,

3)Fahamu ya kuua mambo yote unayoyaona sasa YA KIMAENDELEO hapa Tanzania yanatufuta machozi ni mikakati ya Mkapa

kikwete hajafanya kitu na hatafanya hata moja sio kwamba hataki kufanya HAJUI afanye nini
 
Mmesahau tulivyopanga mawe asubuhi na mapema kutafuta unga kipindi cha Nyerere, magari ya National Milling au kutupiganisha vita ya Field Marshal Amini Dadaa kama sehemu ya kurusedi Afrika Mashariki na sasa kanisa linamzawadia eti mwenye heri wakati alituachia shari. Kanisa linatoa miongozo kila uchaguzi namna ya kumpata kiongozi anayekubalika nalo. Acheni udini jadilini mada.Msiwe Sauli.
 
Ni kweli uchumi umekuwa mbona hiyo ni dhahiri. Ona ma-vogue yalivyojaa bongo na makesi ya vibaka kujichotea mabilioni kila siku utafikiri njugu. Alishasema Lowassa siku nyingi hamkumsikia "uchumi umepaa!" Wamepaa nao hao mafisadi....
 
Pamoja na matatizo, matatizo ambayo ni ya mtoto kukua-kama anaota meno, JK anastahili pongezi kwa mambo mengi tu.Mojawapo ni uweza mkubwa wa watanzania kuongea kwa uhuru kabisa na kufanya mambo bila kuvunja sheria.Wengi wetu tunajua tulikotoka.
Sasa hivi inabidi uwe mwerevu kujua pumba ipi na mchele ni upi kwa maendeleo yako.
 
Kuna mambo mawili au zaidi lazima uyaangalie sio tu hizo statistic

1) Unaangalia kukua kwa uchumi kwa kulinganisha Tanzania na nchi zengine lazima uangalie kama hizo nchi zengine chumi zake zimekuaa pia au zilikua zime stop kukua na hata kama zimekuaa ni kwa rate gani?
Mimi naamini hizo nchi zilizo linganishwa na Tanzania chumi zake zimekuaa kwa niwango kidogo sana au hazijakuaa kabisa

2)Kikwete haja fanya lolote la kukuza uchumi wewe mkuu just tutajie mawili tu aliyofanya ambayo yana result to the long term economic growth,

3)Fahamu ya kuua mambo yote unayoyaona sasa YA KIMAENDELEO hapa Tanzania yanatufuta machozi ni mikakati ya Mkapa

kikwete hajafanya kitu na hatafanya hata moja sio kwamba hataki kufanya HAJUI afanye nini
Hilo swala No 1, ungelijibu wewe kwa kuangalia Nigeria, Kenya na Uganda zilikuwaje huko nyuma. Mimi nimelinganisha Tanzania 2005(alipokabidhiwa Urais Kikwete) mpaka 2008. Msipende kulishwa kwa vijiko, wakati ule wa ujamaa umekwisha sasa ni wakati wa kutumia akili yako usisubiri Zawadi Ngoda akuandikie kila kitu. Kifupi nchi zote hizo uchumi wake umekua lakini si kwa mwendokasi wa Bongo. Umekua kwa ongezeko gani, nawe fanya kazi na chemsha bongo.

Swali No 2 umeomba nikutajia mambo 2 aliyofanya JK kukuza uchumi.

1. Leo tunakutana hapa nakutoa mawazo yetu waziwazi kama alivyoeleza mtoa hoja # Lole Gwakisa. Sikudanganyi, nisingethubutu kuwa muwazi kiasi hiki toka awamu ya 1 mpaka ya 3. Kama Tanzania imepata ufunguo ndio huu, maana hata bubu leo aweza kusema.

Tumeanza kuzijua wapi skendo za EPA, Richmond, Rada na mikataba mbalimbali. Haya yote yalianza kutoka kwenye magazeti na mitandao. Hata Dr Slaa akitoboa ubadhilifu na kunuu habari za kwenye mtandao. Uhuru wa habari ndio uliowapa kufahamu watanzania wote kuwa kumbe Serikalini kuna mambo.

Mikataba iliwekwa wakati wa Mkapa sasa nyie wenye magazeti mlikuwa wapi kusema toka kuanza mazungumzo ya mikataba mpaka inasainiwa? Mlinyimwa haki ya kupata habari, na hata mkipata basi muandishi atakiona kama akiandika habari hiyo. Haya yalikuwa jana tu, eti mnataka kusema kuwa mmeshasahau? Acheni kuwa wepesi wa kusahau.

Nakumbuka wakati wa Nyerere, alilifungia gazeti la New African, eti kwa sababu liliandika 1/4 ukurasa habara juu ya mali zake. Leo hii gazeti la kitanzania linajaza kurasa mbili kuelezea ubadhilifu wa Rais japo ni wa kutunga tu. Lakini Rais anawaachia tu akijua hawa ndio kwanza wanaanza kuutumia uhuru wa kusema.

Sasa usijeukaniuliza, hivi uhuru wa kusema unakuzaje uchumi? Hapo utanivunja mbavu!!

2.Kutokomeza ujambazi. Huwezi kufanya biashara na kukimbia huku na kule kita wawekezaji kama usalama wao na mali zao ziko hatarini. Mabenki ndio yalikuwa kichumo No 1 cha majambazi. Muulize mwanauchumi yeyote yule umuhimu wa mabenki katika kukuza uchumi. Na omba Takwimu ujue kiasi gani cha pesa kilichukuliwa na majambazi wakati wa Mkapa? Ukilijua hilo utakua mjinga kama hukumsifu Kikwete.

Leo watu tunalala kwa amani, jamani tulikuwa hatupati usingizi kama una kajumba kadogo kazuri na vitu viwili vitatu ndani. Mlinzi hata wa bunduki alikuwa hafai, maana wale walikuwa profesionals wakija na silaha nzito. Wenyewe tulikuwa tukiwaita kama watoto wa "Mahita" waliopata baraka za Mkapa. Pengine wenzetu mnaandika toka Ughaibuni ambako mmeshasahau neno majambazi

Samahani uliniomba sababu 2 tu lakini niruhusu nikupe hii ya 3.
3. Kudumisha imani kwa nchi jirani kwetu. Amini usiamini wakatia wa Mkapa kidogo tuingie vitani kati yetu na Rwanda. Kagame alishasogeza majeshi yake mpakani. Mkapa akataka kuonyesha kuwa Tanzania ni super power wa Afrika Mashariki. Kama si umoja wa mataifa basi yale ya 1979 yangetufika. Si kama hayo hayatoshi, uhusiano wetu na Kenya ulikuwa mbovu kama wakati wa Nyerere. Wakati huo Tanzania ikaishutumu Kenya kwa kuwasaidia eti waasi wa Pemba kuleta vurugu Pemba na eti kutaka kuanzisha vita huko. Dhambi kubwa ya Kenya ilikuwa ni kupokea wakimbizi wa Kitanzania, tulisahau kuwa sisi wenyewe ndio wasaidiaji wakubwa wa wakimbnizi toka nchi jirani zenye vita. Kwa mara nyingine tena tukasuluhishwa na Umoja wa mataifa.

Uhusiano na nchi jirani ni muhimu sana katika kukuza uchumi endelevu, na ninafikiri hakuta kuja mwendawazimu mwingine asiyeelewa hili.

Hoja yako ya 3. Eti yote yamefanywa na Mkapa. Ngoja nikupe semi mbili zikusaidie katika maisha yako: Ni ngumu sana kujenga, lakini ni rahisi sana kubomoa. Mwingine: Watu maarufu husema, ni rahisi zaidi kujitahidi mpaka kufika kileleni, lakini kubaki huko kileleni ndio ngumu zaidi.

Semi hizo zote zina lengo la kukueleza kuwa, hebu tukubali kuwa Mkapa ndio aliyofanya kazi. Amini na kwambia kama Hata Mkapa alitengeneza, kwa miaka mitatu ingetosha kwa Kikwete kuharibu kabisa uchumi. Na kama ameweza kubaki huko juu alikokuacha Mkapa na kuongeza basi Kikwete ni shujaa.

Usipoamini maneno yangu, Muulize Clinton alichofanya na kusifiwa na Kile alichofanya Bush. Utasema si kosa lake, ndio majibu yenu pindi umpendaye anapoboronga.
 
LO! Takwimu ni nzuri na zinavutia mno lakini suala sio kukua kwa uchumi,suala ni je hali za wananchi zinaimarika? huo ukuaji wa uchumi unamsaidiajae mtanzania wa hali ya chini?
 
Zawadi nadhani unapiga propaganda za siasa hapa, mimi nimetoka huko vijijini watu ni maskini wakutupwa, Wazee wale hawana hata kiberiti!

Mazao sasa hivi ebu niambie ni zao gani linaingiza pesa serikalini na kumkomboa mkulima? (Pamba, Kahawa, katani) yote hiyo sasa hivi ni historia! Enzi za Nyerere hayo mazao ndo yalikuwa mkombozi kwa mkulima kwa kusomesha watoto,kujenga nyumba bora n.k.

Hapa Dsm ebu angalia mfumuko wa bei na maisha yalivyopanda kwa kasi ya ajabu (bei za vyakula, Petrol, umeme n.k.)

Angalia mishahara ya Wafanyakazi, madai ya walimu n.k.

Sasa huo uchumi alioinua ni upi? mimi sitatumia percent danganya toto natoa mifano ninayokumbana nayo kwenye maisha kwa kulinganisha Nyerere/Mwinyi/Mkapa
/JK.

Unaweza kuwa sahihi jinsi unavyotumia dtazako za Nyerere/Minyi/Mkapa/JK. Lakni swali hivi umeweza kkuwa Kipalapala (Tabora) Ulyankuru na Matemanga(Tunduru) Nyakati hizo zote. Sijui kama una wakala.

Na utawafundishaje wanafunzi wa Vo vyaa biashara na wale wa B.Com wa Mlimani. Sijui kama watakuelewa!!

Sasa burudika na ripoti ifuatayo. Isome kwa makini, nimeiiba katika vyanzo vilivyoandikwa. Kama haikurudhishi sema kwanini. Iangalie Tanzania kwa karibu!!!!

"The Nairobi newspaper, The East African, this week reports that a London based think tank, known as the Institute of Public Policy's Research (IPPR), has placed Kenya and Uganda> among the 20 weakest and failing states of Africa together with Somalia, Rwanda, Burundi and Zimbabwe while Tanzania has been praised.

The same newspaper also reports that Kenya and Uganda have been again kicked out of any prospects for Millenium Challenge assistance while Tanzania continues to enjoy the disbursement of $698 million, which is the highest ever. As usual, Kenya scored poorly in rule of law, immunisation rates, health expenditures and fiscal policy.. In the corruption perception index prepared by Transparency International (TI), Kenya ranks 147th while Tanzania ranks
102nd among 180 countries. The World Bank Institute (WBI) groups Kenya together with Afghanistan and Somalia on criteria such as control of corruption, rule of law, and political stability."
 
Yaani sasa ndio unajijibu mwenyewe kuwa nchi unazojaribu kuzilinganisha na Tanzania zinaporomoka na sio kuwa Tanzania inazipita.

Pamoja na kuwa tuna kiwango cha dhahabu kikubwa kabisa na cha kutosha, na pamoja na kuwa bei ya dhahabu imekuwa inachezea karibu dola 1000 kwa aunsi, lakini bado Tanzania ni ya 102 kati ya nchi 180 zilizopimwa kwenye hiyo ripoti?

NO wonder Kikwete alimtuma Karamagi akasaini mkataba wa Buzwagi hotelini .... ten percent wanayokula hapo sio kidogo.
 
Pamoja na matatizo, matatizo ambayo ni ya mtoto kukua-kama anaota meno, JK anastahili pongezi kwa mambo mengi tu.Mojawapo ni uweza mkubwa wa watanzania kuongea kwa uhuru kabisa na kufanya mambo bila kuvunja sheria.Wengi wetu tunajua tulikotoka.
Sasa hivi inabidi uwe mwerevu kujua pumba ipi na mchele ni upi kwa maendeleo yako.

Hakuna mtu anastahili kupongezwa kwa kutoa ruhusa ya kuongea. Kikwete huyu huyu ndiye alikuwa raisi wakati waanzilishi wa hii forum wamewekwa ndani - umesahau?

Bila kelele za watu hapa unadhani wangeachiwa. Kikwete huyu ndiye raisi wakati waandishi wanamwagiwa tindikali usoni. Umesahau?

Hayo mengine ni juu yako. Kikwete hana uwezo wa kuminya uhuru wa kuongea maana ni mtu anayependa kusafiri kwenda nchi za nje. Anajua kabisa kuwa akianza upuuzi huo ndio utakuwa mwisho wa uvasco dagama wake.
 
Miongoni mwa hao waliosaini mikataba mibovu wakati wa enzi za Mkapa na Mwinyi Kikwete ni mmojawao. Naye ameshiriki kikamilifu kuuza nchi.
 
Hakuna mtu anastahili kupongezwa kwa kutoa ruhusa ya kuongea. Kikwete huyu huyu ndiye alikuwa raisi wakati waanzilishi wa hii forum wamewekwa ndani - umesahau?

Bila kelele za watu hapa unadhani wangeachiwa. Kikwete huyu ndiye raisi wakati waandishi wanamwagiwa tindikali usoni. Umesahau?

Hayo mengine ni juu yako. Kikwete hana uwezo wa kuminya uhuru wa kuongea maana ni mtu anayependa kusafiri kwenda nchi za nje. Anajua kabisa kuwa akianza upuuzi huo ndio utakuwa mwisho wa uvasco dagama wake.

Yule aliemwagiwa tindikali ni kwa uzinzi wake au hujafatilia habari zake?

Na hao walioshikwa humu ndani si kwa sababu ni waandishi! sababu wanazijuwa lakini kwa nini hawajazisema?

Magazeti tumeona yakifungiwa wakati wa Nyerere na Nkapa. nkapa mpaka alifikia kuwaponda waandishi wa Tanzania na kumsifu Riz Khan. Au ulikuwa wapi?

Nyerere ndio duh, hata kuongea na mkeo nyumbani kuhusu Tanzania inavyodidimia na kuwa masikini mpaka ikafikia kuletewa unga wa Yanga ilikuwa huwezi. Au ulikuwa wapi?
 
Hilo swala No 1, ungelijibu wewe kwa kuangalia Nigeria, Kenya na Uganda zilikuwaje huko nyuma. Mimi nimelinganisha Tanzania 2005(alipokabidhiwa Urais Kikwete) mpaka 2008. Msipende kulishwa kwa vijiko, wakati ule wa ujamaa umekwisha sasa ni wakati wa kutumia akili yako usisubiri Zawadi Ngoda akuandikie kila kitu. Kifupi nchi zote hizo uchumi wake umekua lakini si kwa mwendokasi wa Bongo. Umekua kwa ongezeko gani, nawe fanya kazi na chemsha bongo.

Swali No 2 umeomba nikutajia mambo 2 aliyofanya JK kukuza uchumi.

1. Leo tunakutana hapa nakutoa mawazo yetu waziwazi kama alivyoeleza mtoa hoja # Lole Gwakisa. Sikudanganyi, nisingethubutu kuwa muwazi kiasi hiki toka awamu ya 1 mpaka ya 3. Kama Tanzania imepata ufunguo ndio huu, maana hata bubu leo aweza kusema.

Tumeanza kuzijua wapi skendo za EPA, Richmond, Rada na mikataba mbalimbali. Haya yote yalianza kutoka kwenye magazeti na mitandao. Hata Dr Slaa akitoboa ubadhilifu na kunuu habari za kwenye mtandao. Uhuru wa habari ndio uliowapa kufahamu watanzania wote kuwa kumbe Serikalini kuna mambo.

Mikataba iliwekwa wakati wa Mkapa sasa nyie wenye magazeti mlikuwa wapi kusema toka kuanza mazungumzo ya mikataba mpaka inasainiwa? Mlinyimwa haki ya kupata habari, na hata mkipata basi muandishi atakiona kama akiandika habari hiyo. Haya yalikuwa jana tu, eti mnataka kusema kuwa mmeshasahau? Acheni kuwa wepesi wa kusahau.

Nakumbuka wakati wa Nyerere, alilifungia gazeti la New African, eti kwa sababu liliandika 1/4 ukurasa habara juu ya mali zake. Leo hii gazeti la kitanzania linajaza kurasa mbili kuelezea ubadhilifu wa Rais japo ni wa kutunga tu. Lakini Rais anawaachia tu akijua hawa ndio kwanza wanaanza kuutumia uhuru wa kusema.

Sasa usijeukaniuliza, hivi uhuru wa kusema unakuzaje uchumi? Hapo utanivunja mbavu!!

2.Kutokomeza ujambazi. Huwezi kufanya biashara na kukimbia huku na kule kita wawekezaji kama usalama wao na mali zao ziko hatarini. Mabenki ndio yalikuwa kichumo No 1 cha majambazi. Muulize mwanauchumi yeyote yule umuhimu wa mabenki katika kukuza uchumi. Na omba Takwimu ujue kiasi gani cha pesa kilichukuliwa na majambazi wakati wa Mkapa? Ukilijua hilo utakua mjinga kama hukumsifu Kikwete.

Leo watu tunalala kwa amani, jamani tulikuwa hatupati usingizi kama una kajumba kadogo kazuri na vitu viwili vitatu ndani. Mlinzi hata wa bunduki alikuwa hafai, maana wale walikuwa profesionals wakija na silaha nzito. Wenyewe tulikuwa tukiwaita kama watoto wa "Mahita" waliopata baraka za Mkapa. Pengine wenzetu mnaandika toka Ughaibuni ambako mmeshasahau neno majambazi

Samahani uliniomba sababu 2 tu lakini niruhusu nikupe hii ya 3.
3. Kudumisha imani kwa nchi jirani kwetu. Amini usiamini wakatia wa Mkapa kidogo tuingie vitani kati yetu na Rwanda. Kagame alishasogeza majeshi yake mpakani. Mkapa akataka kuonyesha kuwa Tanzania ni super power wa Afrika Mashariki. Kama si umoja wa mataifa basi yale ya 1979 yangetufika. Si kama hayo hayatoshi, uhusiano wetu na Kenya ulikuwa mbovu kama wakati wa Nyerere. Wakati huo Tanzania ikaishutumu Kenya kwa kuwasaidia eti waasi wa Pemba kuleta vurugu Pemba na eti kutaka kuanzisha vita huko. Dhambi kubwa ya Kenya ilikuwa ni kupokea wakimbizi wa Kitanzania, tulisahau kuwa sisi wenyewe ndio wasaidiaji wakubwa wa wakimbnizi toka nchi jirani zenye vita. Kwa mara nyingine tena tukasuluhishwa na Umoja wa mataifa.

Uhusiano na nchi jirani ni muhimu sana katika kukuza uchumi endelevu, na ninafikiri hakuta kuja mwendawazimu mwingine asiyeelewa hili.

Hoja yako ya 3. Eti yote yamefanywa na Mkapa. Ngoja nikupe semi mbili zikusaidie katika maisha yako: Ni ngumu sana kujenga, lakini ni rahisi sana kubomoa. Mwingine: Watu maarufu husema, ni rahisi zaidi kujitahidi mpaka kufika kileleni, lakini kubaki huko kileleni ndio ngumu zaidi.

Semi hizo zote zina lengo la kukueleza kuwa, hebu tukubali kuwa Mkapa ndio aliyofanya kazi. Amini na kwambia kama Hata Mkapa alitengeneza, kwa miaka mitatu ingetosha kwa Kikwete kuharibu kabisa uchumi. Na kama ameweza kubaki huko juu alikokuacha Mkapa na kuongeza basi Kikwete ni shujaa.

Usipoamini maneno yangu, Muulize Clinton alichofanya na kusifiwa na Kile alichofanya Bush. Utasema si kosa lake, ndio majibu yenu pindi umpendaye anapoboronga.

Huna hoja na uache longongo zako wee Zawadi Ngudu! Kulikoni ulete takwimu za CIA, ambao kwa Waislamu walio wengi wanafahamika kuwa ni ADUI NAMBARI WANI WA ISLAMU, na ambao bila shaka, Ansar al Sunna/Shura ya Maimamu wanapinga kwa nguvu zao zote (ikiwamo mabomu ya atomiki na nyuklia kama ikiwezekana) chochote kile kinachohusiana na CIA/Wazungu/Wakristo/Makuruseda/Makafiri?

Afterall, if Muslims really do make up 50% of the population in Tanzania, then chances are, one or another Muslim intellectual would have come up with figures that side with your side of the story about the unprecedented, phenomenal successes of Kikwete's economic policies.

Wewe unachotakiwa kufanya hapa, Ms. Zawadi Ngedere, ni kutumwagia takwimu zilizotayarishwa na hao milioni 20 (au 50%) ya Watanzania unaodai ni Waislamu.
 
Tanzania is in the bottom ten percent of the world's economies in terms of per capita income. The economy depends heavily on agriculture, which accounts for more than 40% of GDP, provides 85% of exports, and employs 80% of the work force. Topography and climatic conditions, however, limit cultivated crops to only 4% of the land area. Industry traditionally featured the processing of agricultural products and light consumer goods. The World Bank, the IMF, and bilateral donors have provided funds to rehabilitate Tanzania's out-of-date economic infrastructure and to alleviate poverty. Long-term growth through 2005 featured a pickup in industrial production and a substantial increase in output of minerals led by gold. Recent banking reforms have helped increase private-sector growth and investment. Continued donor assistance and solid macroeconomic policies supported real
GDP growth of 7.1% in 2008.

Source: CIA world fact boook.

kumbe kubadilika kwa hayo ma namba yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na dhahabu wanayoiba hapa na kutuachia vumbi?!
yaani sisi sijui tukoje? aliyetulaani ametuweza kweli...mwizi anakuja nyumbani kwako na familia yako Zawadi, unamkaribisha.... ana kupa peremende ya Tsh 200 ili ummkabidhi fanicha zako mpya na pesa..unamkabidhi tena mpaka zile ulizoweka benki, ..anaenda mtaani anapiga kelele "Zawadi ana maendeleo siku hiziiii, ana furniture mpyaaa na pesaaa!!" na wewe unafurahi na kujigamba tena kwa maringo kwamba uchumi wa nyumbani kwako umeongezeka, tena una nukuu maneno ya mwizi huyohuyo kama ushahidi...

We have a looong way to go LOL!
 
huna hoja na uache longongo zako wee zawadi ngudu! Kulikoni ulete takwimu za cia, ambao kwa waislamu walio wengi wanafahamika kuwa ni adui nambari wani wa islamu, na ambao bila shaka, ansar al sunna/shura ya maimamu wanapinga kwa nguvu zao zote (ikiwamo mabomu ya atomiki na nyuklia kama ikiwezekana) chochote kile kinachohusiana na cia/wazungu/wakristo/makuruseda/makafiri?

Afterall, if muslims really do make up 50% of the population in tanzania, then chances are, one or another muslim intellectual would have come up with figures that side with your side of the story about the unprecedented, phenomenal successes of kikwete's economic policies.

Wewe unachotakiwa kufanya hapa, ms. Zawadi ngedere, ni kutumwagia takwimu zilizotayarishwa na hao milioni 20 (au 50%) ya watanzania unaodai ni waislamu.

umekunywa au kuvuta nini leo ??? Mbona hufahamiki

akili ikirudi , soma tena alichokiandika zawadi ,

kwani huko mwanzo ulimwomba afanye nini ????

hebu ikirudi akili soma tena

Ukiziamini takwimu za CIA kupitia website yao(www.aneki.com), basi hutakuwa na ubavu wa kukipinga kichwa cha habari hapo juu. CIA ni shirika lnaloaminika sana duniani, na lipo up to date katika takwimu zao.

Miaka miwili iliyopita nilitembelea mtandao wao na nikapata aibu, pale nilipoiona Tanzania katika bora 10 masikini duniani. Kwa wasomaji wazuri wa mtandao wa wakati ule T/Daima wanaweza kukumbuka jinsi nilivyokuwa naleta takwimu hizi kwa masikitiko. Mara leo hii upepo umegeuka na naweza kuandika kwa majigambo jinsi uchumi ulivyopanda kama ndege, mig 21. Leo hii Tanzania ipo nafasi ya 28, ikipanda toka nafasi ya 8 mwaka 2007. Ifuatayo ni orodha ya nchi 33, ikianzia Zimbawe msikini sana ikiwa na GDP $200, na ya 33 ni Chad ikiwa na GDP $1600
Top 100 countries with the lowest GDP per capita
Samahani; nilijaribu kuziweka hapa hizo nchi lakini hazijatokea. Hivyo tembelea www.aneki.com. Na angalia katika Top 100 countries.........kama hapo juu.

Mwaka 2007 Tanzania ilikuwa na GDP kama Somalia leo hii, $600 (sh 780000) na tulishika nafasi ya 8. Ninafura kusema kuwa leo hii tuna GDP ya $1400 ( sh 1820000). na kuzibwaga nchi kadhaa na kushika nafasi ya 28. Kiwango hicho cha pesa kinafanya tofauti ya sh 1040000 kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa hesabu rahisi ukuaji wa GDP kwa kipindi cha miaka miwili ni wastani wa sh 520000 kwa mwaka.

Ikiwa kama Kikwete atachaguliwa tena, katika uchaguzi wa 2010 na kuwa madarakani mpaka 2015, na kwa mwendo kasi huu ina maanisha kuwa GDP ya Tanzania mwaka 2015 itakuwa sh 1820000 +(520000*6)= 4940000 = $3800. Hii inamaanisha kwamba kama ilivyo leo hii, basi Tanzania itakuwa katika nafasi ya 67, sawa na Djibouti yenye kiwango hicho leo hii.

Watanzania tutakuwa wendawazimu kama hatutaridhika na kufurahia maendeleo hayo kiuchumi. Kwa maendeleo hayo, tunaweza vile vile tukasema bye bye misaada, sasa wenyewe tutajiendesha, kama vile warusi walivyofanya mwaka 2004 kwa IMF na World Bank. Na hii ndio ndoto yangu kubwa na nafikiri ndio ndoto ya Serikali na watanzania wote kwa jumla.

Tabasam la Kikwete lina bahati, ngekewa na linazivuta nchi zote duniani kuiona Tanzania kama Tumaini la uwekezaji. Kusema kuwa Kikwete anaweza, sio tu propaganda bali Takwimu zinajionyesha. Pamoja tutashinda, safari ni ndefu na uvumilivu ndio dawa.

ukitaka kujua kama uchumi wa tz unakua au la,huitaji madata ya CIA wala usiangalie hizo mbwembwe zinazoendelea hapo Dar es salaam...angalia maisha ya watanzania walio wengi kule kijijini ukilinganisha na miaka mitano iliyopita
 
umekunywa au kuvuta nini leo ??? Mbona hufahamiki

akili ikirudi , soma tena alichokiandika zawadi ,

kwani huko mwanzo ulimwomba afanye nini ????

hebu ikirudi akili soma tena

Na hawa watoto ombaomba hapa chini (nadhani wawili au watatu wana miaka si zaidi ya 4) wanasubiri peremende za Kikwete. Hebu mwaga hizo data za Ansaar al Sunna, halafu ndiyo tuanze kujadili mada ya uchumi kupaa ...

09_09_1vgz1q.jpg

Watoto wanaoomba katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam wakiwa wanazurura katika barabara ya Lumumba leo. (Picha na Mroki Mroki)
 
uchumi umekuwa lakini mbona sisi wananchi tulio na hali ya chini ndio tunazidi kudidimia ,sipati sence kabisa
 
Zawadi nadhani wewe ni Mwanasiasa na hapa umekuja kisiasa. Hapa kuna maswali magumu lakini umekuwa unapiga chenga chenga zinakuwa nyingi hatupati majibu mpaka hata watu wanashikwa hasira.

Wewe utamwambiaje Mtanzania wa kawaida uchumi umeinuka na huku nyumbani Mtanzania huyo huyo hakuacha hata robo ya unga na maharage?? au wewe ni fisadi??

Zawadi acha utani! ukumbuki yule Rais wa Walimu pale Diamond Hall walimfanya nini??

Kajipange upya na hizo takwimu sisi wengine hatukuelewi!
 
Naona sasa kampeni za JK 2010 zimeanzia JF! Unapoona post ya mtu unayeweza kumhisi kama kada wa SISIEM, watch out! Just ignore them!

JF kama community ya great thinkers, sio watu wakudanganywa kirahisi na watu wachache wenye lengo la kutimiza malengo yao ya KIBINAFSI. Nashukuru kwa kuwa wengi wetu tunaelewa ni nini cha kufanya ili kuikomboa nchi yetu. Tubaki na msimamo wetu na kujenga hoja zisizo na mitazamo binafsi kama ile ya wachache waliovamia JF wakijaribu kuendelea kuipotosha jamii yetu ya watanzania.

Tanzania tunaipenda wengi, ila wachache wenye nguvu ndio wanaoiharibu. MUNGU atusaidie.
 
Back
Top Bottom