Wajameni,
Nilikua sijamsikiliza Kikwete kwenye kampeni leo nikasema ngoja nibuy time nimsikilize. Jamaaa ni mweupe hakuna mfano. Hata hayo machache aliyofanya kashindwa kuyaelezea pamoja na kuulizwa guided questions. Sijaona cha kuvutia kutoka kwake hata kidogo. sioni kwa nini TV na Radio leo jioni kupoteza Valuable time kuendesha mahojiono kwenye vyombo hivyo wakati hana jipya la kutuelezea. Nasema ni bora hata zile hotuba zake za mwezi walau alikua anagusia jambo liliotokea mwezi huo.
Nenda kapumzike kaka yetu, umechoka saaana, umesahau watu wako, umeisahau nchi yako, umeshau wapiga kura wako, hata kule kwako kiwangwa, chalinze, yombo, Ubena, fukayosi, bagamoyo, vigwaza wamekuchoka, hivyo kwa nini usiende ukajipange tena uje 2015? kwa sababu hujamaliza 10 years unaweza kuja kugombea tena 2015, Pumzika kwa sasa mpatie Dr. Slaa,
Hakuna mtu anaheshimika kama kiongozi anayesikia na kutenda yale anaowangoza wanataka.
Hatutaki ufisadi hujasema utalishughulikia vipi,maradhi hatuoni jinsi gani ushugulikia
Elimu hatuoni...... nk
Nenda kapumzike ukipata nguvu za kutosha kuja kuwatumikia kwa kasi na nguvu mpya kama ulivyosema
njoo uje utuombe ridhaa tena tunaweza kukufikiria vinginevyo kapumzike ulee familia yako vema.
Sisi wananchi tutakuenzi kwa kukuita Rais mstaafu nenda kapumzike.
Unatumia rasimali za nchi vibaya na sasa hadi vyombo vya habari unavitumia vibaya
kwa sababu umeshindwa kutimiza wajibu wako sasa unatumia vyombo vya habari kuwafanya watu
waamini umefanya mengi, kweli umefanya mengi (ufisadi na mengine) lakini sio hayo tunayoyataka sisi.
tunataka maendeleo ya nchi pamoja na mtu mmoja moja, umeshindwa kutimiza hilo watanzania tunasema
tunashukuru kwa kutupotezea muda hivyo nenda kapumzike mstaafu wetu tuko tayari tuingie hasara ya kukulipa10million kila mwezi pension lakini ukapumzike kuliko kututia hasara ya mabilion ukiendelea kuwa rais. Tunasema nenda kapumzike