Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Achaneni na kilaza jamani...Ni mtapeli huyu!
hahaha yuu noo obama hahaha owa kentri haha izi veri pua pipo ara noti no skuli hahaha aha ha puuuliizi hehehe teki machi hahaha konsidaresheni teteh teeh yuu noo hihihi wora amu tokini..Du huyu jamaa huwa inakuwaje akikaa na akina Obama!
yaani waandishi wetu wanashindwa kuuliza maswali ya msingi,rushwa,ufisadi,wanauliza mambo ya barabara za dar,mambo ya kumuliza diwani,nimeuzunika sana.
Maendeleo kwa mujibu wa Dr. Slaa ni Elimu bora kwa kila mtanzania, Afya bora kwa kila mtanzania, Makazi bora, Fursa sawa, Haki kwa jamii, Ongezeko la pato la taifa likiambatana na uwekezaji bora na matumizi bora ya rasilimali za Taifa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Maendeleo kwa mujibu wa Jakaya Kikwete ni ongezeko la foleni Dar es Salaam, Ongezeko la nyumba mbovu na zilizo nje ya mpangilio wa mipango miji ambazo siku za usoni zitakuja kubomolewa tu na wananchi watakosa mahali pa kuishi kama ilivyotokea kurasini, tabata dampo na kwingineko. Pia kupunguza daladala ''kuchomekeana''
Gonga link hiyo hapo juu umsikilize JK na sera zake leo Clouds FM
Mkuu, mbona mazungumzo yenyewe hayapo?
Mhhhh!!! hata kuiba mke wa mtu ameweza kuiga???Hana jipya huyo msanii tu, kwelia ameamua kuiga kila kitu anachokifanya dr wa ukweli, si aige mbinu za kupambana na ufisadi. Oh sorry kumbe muda wake wa uongozi ndo umefikia mwisho!
Unauliza majibu?.Kama anaweza sema hajui kwa nini waTz ni maskini unategemea nini?Yaani baada ya kumsikiliza leo nasikia uchungu sana kwamba ilikuwaje akapata urahisi 2005. Hawezi kueleza kitu chochote chenye mantiki na mvuto. Huwa anaongeaje na marais wenzake anapokwenda nje ya nchi?si ametutia aibu miaka yote hiyo mitano aliyokuwa anasafiri hovyo hovyo?
Wakuu,
Mdahalo wa JK kupitia Clounds umemmaliza badala ya kumjenga! Anapiga porojo, uelewa mdogo, vicheko visivyo na msingi, anazungukazungukaa wee hajibu swali. Anaulizwa maswali mazuri sana ambayo kama angekuwa mtu mwenye uwezo na upeo angejibu kwa umahiri kabisa na angegeuza mtazamo uliopo sasa hivi kwamba uwezo wake wa akili ni mdodo na hana uwezo wa kuleta mabadiliko.
Kwa maoni yangu, hii ina maana watu ambao wamemsikiliza hata kama bado walikuwa na imani naye basi amewakatisha tamaa. Ameshindwa kuonesha uwezo wake wa kuelewa mambo, kujibu maswali, na kukabiliana na changamoto tulizo nazo sasa hivi. Amethibitisha kwamba yeye hana uwezo wa kutuongoza.