Wakuu,
Mdahalo wa JK kupitia Clounds umemmaliza badala ya kumjenga! Anapiga porojo, uelewa mdogo, vicheko visivyo na msingi, anazungukazungukaa wee hajibu swali. Anaulizwa maswali mazuri sana ambayo kama angekuwa mtu mwenye uwezo na upeo angejibu kwa umahiri kabisa na angegeuza mtazamo uliopo sasa hivi kwamba uwezo wake wa akili ni mdodo na hana uwezo wa kuleta mabadiliko.
Kwa maoni yangu, hii ina maana watu ambao wamemsikiliza hata kama bado walikuwa na imani naye basi amewakatisha tamaa. Ameshindwa kuonesha uwezo wake wa kuelewa mambo, kujibu maswali, na kukabiliana na changamoto tulizo nazo sasa hivi. Amethibitisha kwamba yeye hana uwezo wa kutuongoza.