Elections 2010 Kikwete Live on Power Breakfast (Clouds FM)

Elections 2010 Kikwete Live on Power Breakfast (Clouds FM)

Kuwa mpole jethro

Mkuu

Ntawezaje kuwa mpole huku Rais wangu huyo anayoyaongea ni kama vile huwa hawana watu wa mipango miji na mgawanyo wa Funds huko mikoani jamani ukiangalia rasilimali nyingi za Taifa zatokea Kanda ya ziwa ambako huko ndiko kulitakiwa kuwe baraaaa kupita mikoa mingine ukicheki Shinyanga utalia, nenda Kahama ndio usiseme, Rudi Nyamongo - Tarime wacha bwana maendeleo ni zero tuu neda Arusha nako ndiko kila siku kukicha leo wanaambiwa JIJI mara kesho wanaambiwa vigezo havijitoshelezi sasa ni nini seriklai imejipanga,

Serikali inapo kuza maendeleo inatakiwa ijipange na kuangali future ya wananchi na vizazi vilivyopo na vijavyo itakuwaje. na ndio maana nikasema au kushauri sera ya Majimbo irudi muone kama Dar watu watakaaa watu wote utawaona Arusha au Mwanza

 
Clouds fm, imechakachuliwa na thithiem unadhani watauliza ki2 gani muhimu cha kitaifa wakati maDJ na MaCM ni wale wale vihiyo, wamepita pita vyuo vya ghorofa ya 3 wakaambulia hamna.

Bora wafunge kiredio chao wakacheze mdako, kibonde na wenzake wabwatukaji tu kama jamaa yao makamba......
 
Ama kweli simba akizidiwa hula majani....! Mdahalo huu kwa CCM na JK sio kama majani kwa simba? Kwani mmeshasahau kauli na msimamo wa CCM kuhusu mdahalo? Kuwa lazima makubaliano juu ya maswali ya kuuliza na watu wa kuuliza yawekwe mapema....! Mmesahau hata tabia yao ya uchakachuaji? Mimi naamini lazima mdahalo huo uchakachuliwe kwa kuwaandaa watu na maswali ya kuulizwa...! Bado pia nashangaa kuwa iweje leo wanataka kuwasikiliza wananchi wakati walisema wao wanajua wananchi wanahitaji nini? Vinginevyo, mimi nawashauri wana CCM wasidhubutu hata kuingia kwenye mdahalo huo maana watazidi kujimaliza...! Wasijilinganishe na Dr. Slaa na CHADEMA au Prof. Lipumba na CUF....!

Halafu nahisi haikuwa live imekuwa record
 
Yaani waandishi wetu wanashindwa kuuliza maswali ya msingi,rushwa,ufisadi,wanauliza mambo ya barabara za dar,mambo ya kumuliza diwani,nimeuzunika sana.

mbona Slaa aliulizwa maswali mengi ya kiuchumi, tatizo hao jamaa walikuwa wako kimaslahi zaid leo
 
Eboo--ukishagawa nchi kwenye majimbo, that means they are divided kikabila (geographically). Swali ni kwamba, how can you maintain uTanzania katika mazingira haya? Ukiangalia sana katika resources allocation kutoka central government, and distribution of resources from the haves to the have nots.

Mpiganaji wenu hakufikiria suala la umoja na mshikamano katika majimbo. If you can figure that one out without having disgruntled majimbo--then go ahead.
Mkuu ukiipanua sana hoja hii utakuja kugundua kuwa hata shukle za sekondari za kata nazo zinaligawa taifa kwa misingi ya ukabila na mtu atokako kwa sababu mtu anaweza kusoma mpaka form four (na wanataka kuongeza mpaka form six) katika kijiji chake. Huyo hatawafahamu wananchi hata wa kijiji jirani.
 
Mmesikia hiyo? Magari ni maendeleo

.... na majumba makubwa makubwa yanayoonekana ni indicators of a rising n thriving middle class! PHEW!!!
Nilitarajia angesungumsia indiketa moja kutetea maendeleo hayo .....decline in destitution matched with actual, not fictitious growth in GDP, real growth that can be seen kwa maskini wa nchi hii .... yaani, in bold and clear language, kuanzia na yule wa chini kabisaaa, AONE maisha sio msululu tu wa taabu za ajabu, pawepo na MATUMAINI ya kweli kwamba PAMOJA na juhudi zao wenyewe kuondokana na UMASKINI, mfumo uliopo unawajali na waweza kuwavusha upande wa pili.

Nimesikiliza throughout mahojiano yale. Najiuliza maswali bado. Ni Watanzania wangapi wenye pato la halali nikimaanisha kwanza kwenye upatikanaji wa pato hilo na baadae WALIVYOLIPIA kodi pato hilo ambao wana uwezo wa kujenga MIJENGO anayozungumzia Dr JK? Changanya hapo na Wabenzi nikimaanisha wenye uwezo wa kununua na kuimudu ile migari ambayo ktk nchi kama UK ni ya mijamaa ilosheheni fedha kwelikweli tangu enzi za mababu.

Kamfano kadogo tu....wale waloweza ku-airlift magari to Dar si mnawajua? I am not contradicting myself na vigari vya USD 7000 landed cost ingawa hata hapo unakuta jamaa huyo huyo ana ka-mshahara wa 180,000, jumba la USD 200,000 plus ukiacha nyumba ndogo.

Eti hayo ni maendeleo!!! DUH. Kazi kwelikweli.
 
Duuuuuh huyu jamaa ataenda mpaka kwenye Leo Tena na Part ile ya HEKAHEKA.:rip: CCM

Tonge bana, mwenzako anakusanya idadi ya kura sasa atafanye wazungu wanasema with hooks and crooks usije ukamshangaa kaingia hadi kwenye XXL
 
ndo maana ogopa saana kiongozi anaeahidi maji, barabara, ni vitu vya msingi, ni haki ya kila raia, Rais anaeahidi kukuletea umeme, wapuuzi hawa.
 
mwache acheke bwana kwanini alie!

Wengi hamjui kuwa JK hacheki kwa hisia. Yeye anaugonjwa wa chekachekamania.

Kuna siku alikuwa akielezea jambo analodai lililomtia uchungu..akasema...''jamani watu wanaua albino ha ha ha...wengine wanabaka mpaka vikongwe ha ha ha ha..tehe tehe tehe jamani mimi naona uchungu sana watanzania he he he he..oh ho ho ho" yaani alicheka mpaka machozi yakamtoka sasa wewe unashangaa jamaa akicheka??

JK siku hizi akienda msibani, Ikulu kuna dawa wanampa ambayo inagandisha viungo vyake na uso wake unakuwa kama sanamu la 'Boutique' ili asionekane kucheka msibani...ndio maana anakuwa amenuna kuliko kawaida ya binadamu anapokuwa msibani.

Vinginevyo angeenda msibani na kuhutubia...''Jamani nasikitika sana kuondokewa na Waziri wangu huyu mchapakazi ha ha ha ha, oh hoho ho ho ho ho ho ...ha ha ha ha ha ha ha ha ha hah ...''

Wenu mtiifu.
 
Jamani hii radio ctamani hata kuickia tena haina usawa hta kdg but km wao wanaukumbatia mbuyu cc 2nauzunguka ngoja waone trh31
 
Mpiganaji alisema yeye akipewa nchi atagawanya katika majimbo, lakini alipingwa vibaya mno na akachomekewa kwamba anataka kuwagawa watanzania ki-kabila, ,

JK ndiye aliyetaka kuiweka nchi kwenye majimbo?? na Nani aliyempinga CCM au MAFISADI wa SIASA??? Kwani MAJIMBO si Muunganiko wa mikoa kadhaaa na sio kila mkoa peke yake? Majimbo kwangu mie yange kuwa ki kanda,? au wewe nawe wasemaje? Naamini kuwepo kwa majimbo kungekuewepo na mgawanyiko mzuri wa kiuchumi na maendeleo bila shida

 
Wengi hamjui kuwa JK hacheki kwa hisia. Yeye anaugonjwa wa chekachekamania.

Kuna siku alikuwa akielezea jambo analodai lililomtia uchungu..akasema...''jamani watu wanaua albino ha ha ha...wengine wanabaka mpaka vikongwe ha ha ha ha..tehe tehe tehe jamani mimi naona uchungu sana watanzania he he he he..oh ho ho ho" yaani alicheka mpaka machozi yakamtoka sasa wewe unashangaa jamaa akicheka??

JK siku hizi akienda msibani, Ikulu kuna dawa wanampa ambayo inagandisha viungo vyake na uso wake unakuwa kama sanamu la 'Boutique' ili asionekane kucheka msibani...ndio maana anakuwa amenuna kuliko kawaida ya binadamu anapokuwa msibani.

Vinginevyo angeenda msibani na kuhutubia...''Jamani nasikitika sana kuondokewa na Waziri wangu huyu mchapakazi ha ha ha ha, oh hoho ho ho ho ho ho ...ha ha ha ha ha ha ha ha ha hah ...''

Wenu mtiifu.

Haki ya nani umedata!!!
 
Walijipangia maswali rahisix2 ya kurahisisha mdahalo ili wananchi waone ni poa tu, lakini waelewa wanaelewa nini cha kufanya hapo 31.
 
Clouds haina waandishi ina maMC njaa(Kibonde) na maDJ wa kipaimara,kitchen parties(Hando)

Sijui ni kwa nini wenzetu hawa hawataki kutafuta elimu. Au ni mazoea ya kuchekesha watu ktk sherehe sasa wanadhani kila sehemu ni vichekesho. Leo wametoa simu ya uongo na hiyo ndo ingewasaidia kupata maswali ya maana.

Lakini pia mkuu wa Clouds, lazima ajifunze kupanga watu wake. Huwezi ukampa kijana wa miaka 30 kumuhoji mkuu wa nchi wa miaka 60. Labda kama kaona Rais ana tabia za umri huo.

Ni jambo la kuiga tu. waangalie wazoefu BBC, VOA ili waone umri na elimu ya wanaowahoji ma-Rais wa nchi.

MC anamuhoji Rais juu ya mambo ya kisiasa!!!!!!!!!!!!!!
 
Mnatupotosha tu humu ndani na subjective interpretation of the interview. Kwenye macho na masikio yenu JK can't do any better. Hamko open minded.

One more day. And all this hypocrisy will end!!
agree sele... kikwete nact do any better... but knowing you... you can do better than him,
 
Jamani Hando aliuliza maswali mazuri sana siku ile alimhoji dk.Slaa. Hii show ya leo nahisi jamaa alikuwa kashaandaliwa maswali ya kuuliza.
Tofauti na interview na Slaa, ambayo clouds waliomba kumwoji Slaa nyumbani kwake, hii ya leo Clous ndo waliitwa wakamuhoji prezidaa ikulu na sharti kubwa ilikuwa lazima waulize maswali kama yalivyo kwenye paper...very low Mr. President. nazidi kuelewa ni kwa nini huju jamaa hata wamshikie bunduki hawezi tia timu akaojiwe na waandishi makini.
 
Eboo--ukishagawa nchi kwenye majimbo, that means they are divided kikabila (geographically). Swali ni kwamba, how can you maintain uTanzania katika mazingira haya? Ukiangalia sana katika resources allocation kutoka central government, and distribution of resources from the haves to the have nots.

Mpiganaji wenu hakufikiria suala la umoja na mshikamano katika majimbo. If you can figure that one out without having disgruntled majimbo--then go ahead.

Again... kama ni kuwagawa watanzania, basi shule za kata ndio namba moja... mrangi hawezi tena kusoma mwanza... mnalocalise hawa watu na kibaya zaidi kuna makabila yataishia kuwa wasusi tu maana hawana shule za maana

KUhusu majimbo... Hivi marekani ukiwa jimbo fulani hurusiwi kwenda kwingne??
Hivi kweli jimbo na mkoa kioperesheni kuna tofauti yoyote???
unataka kusema ukiwa jimbo moja lazma uombe viza ya kwenda kwingine?
wewe sele wewe.... yani ndio uelewa wako kuhusu majimbo huo???

Sera ya majimbo ni kugawa watu wkeli au ku-decentralise administration and specify on development strategies?? yesu wangu!!! :doh:

Dont let me lose you, i rate you very highly mkuu

tumedecentralise nchi kwenye huduma za jamii kwenda wilaya, ni ukweli usiopingika kwamba tunapoteza pesa nyingi kwani efficiency na accuntsbility iko chini sana... tumeanza sasa kukgundua nafasi ya mkoa... ukiniuliza mimi, ntasema weka majimbo... kanda ya ziwa weka majimbo mawili unganisha na magharibi halafu niambie kama hiyo mikoa itadoda ten

kanda ya kati weka... wana natural resoruces zao na waisha yao... develop (sorry copy paste) system iliyokua proven nje ya tanzania... impelement uone

dah
 
Msiwalaumu sana hao vijan, wenyewe wameelekezwa na mabosi wao kufanya yale waliyofanya kwa Kikwete.

Hata wengine humu jamvini wangekaa nafasi yao wangefanya hivyo hivyo. Ni waajiriwa tu, pengine kura zao watampa Slaa. Pale wanabangaiza mkate wao tu wa kila siku.
 
Back
Top Bottom