Kikwete mbona Magufuli alipofariki dunia hukumuelezea kirefu kama kwa Membe?

Unapaswa kushangaa kwamba JPM hakuwa rafiki wa JK lakini JK alimpa u waziri na baadaye kuruhusu hata awe rais! Kama Kikwete ana chuki na JPM basi kosa ni la JPM sio la JK. Unaelewa?
Watu wangemshangaa kama asingempa uwaziri, pia kwenye urais hakuwa na namna maana hali haikuwa hali, hata yeye mwenyewe alisema , walikuwa wanasema sisiem itanifia mkononi ikowapi hata yeye alishukuru, mtafute Shibuda

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kwani nasema uongo jamani? --- in Magu's voice
Mufti ni kati ya watu wachache waliopata nafasi ya kwenda kuongea nae hospital akiwa mgonjwa siku za mwisho wa uhai wake.
Habari ya msikiti wa Kinondoni unaijua bila shaka.
Na ule alioitaga harambee tena kanisani na pesa ikachangwa

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Ni rahisi kumuelezea mstaarabu kuliko mdhalimu.nimemaliza
 
Damu ni nzito kuliko maji, ujue!
 

..tungekuwa na KATIBA BORA huyo bwana na watu wake wasingetupa shida.

..Katiba yetu imeandikwa kwa ajili ya CCM na si nchi au wananchi.

..Kwa hiyo atakayekamata CCM ameikamata nchi.
 
Ndugu yangu uwezo wangu mkubwa najielewa
O level Tabora boys one 7
A-level mzumbe one 4
Bachelor degree civil engineering UDSM
Masters Highway udsm

Usijifananishe na mimi wewe tahira
Wewe unajiona wa pekee sana. Hujui wapo wengi zaidi yako. Kama ni masuala ya academic performance, upo mbali sana toka kwangu, japo nafahamu kuwa hata mimi wapo wengi wa kunizidi. Mimi nilitoka ni 3As PCM, hraduate degree second best science student, postgraduate degree best MSc student (Geological sciences) University of British Columbia.

Lakini la muhimu zaidi ni kwamba performance ya darasani si chochote, kama haiwezi kuakisiwa na maisha yako ya kila siku. Kama unabaki unatukana tukana watu hovyo, hata hizo degree zako zinakuwa hazina maana yeyote kwa yeyote kwa sababu zimeshindwa kukusaidia hata wewe mwenyewe binafsi kjstaarabika na angalao kuweza kuwa hata na hekima ile ya kawaida ambayo hata mtu asiyeenda shule anastahili kuwa nayo. Unaweza kuwa umesoma lakini hujaelimika.
 
Wengi wamejitwika upofu wa akili.

Magu alifanya aliyoweza kuyafanya, lakini ukweli ni machache sana ukilinganisha na ambayo tayari yalikuwa yamefanyika. Mema yale aliyoyafanya hayabezwi lakini si kweli kwamba alifanya maajabu.

Vyuo vikuu
Nyerere - UDSM, SOKOINE, MZUMBE
Mwinyi - 0
Mkapa - 0
Kikwete - UDOM
JPM - 0

Hospitals Kubwa
Nyerere - Muhimbili
Mwinyi - 0
Mkapa - 0
Kikwete - Taasisi ya Moyo, Mloganzila, Mkapa hospital
JPM - 0

Mabwawa ya Umeme
Nyerere - Kidatu, Mtera
Mwinyi - Kihansi
Mkapa - 0
Kikwete - 0
JPM/Samia - Nyerere

Barabara Ndefu za lami
Nyerere - Dar to Kaprimposhi
Mwinyi - 0
Mkapa - Dar to Kibiti
Kikwete - Dar to Mafinga, Chalinze to Arusha, Moro to Mwanza, Mwanza to Bukoba, Dodoma to Iringa, Kahama to Nyakanazi, Songea to Masasi, Kibiti to Mtwara, Tunduma to Sumbawanga
JPM - nyingi barabara fupi na za mijini.

Reli
Nyerere - Uhuru
Mwinyi - 0
Mkapa - 0
Kikwete - 0
JPM/Samia - SGR

Ndege
Nyerere - 13 brand new jet engine
Mwinyi - 0
Mkapa - 0
Kikwete - 0
JPM -8, 3 jet engines, 5 pangaboi

Madaraja makubwa
Nyerere - 0
Mwinyi - 0
Mkapa - Umoja
Kikwete - Tanzanite
JPM/Samia - Busisi

Viwanda
Nyerere - vingi sana
Mwinyi - 0
Mkapa - 0
Kikwete - 0
JPM - 0

Lakini Mkapa ndiye aliyejenga uchumi wa kisasa na kutengeneza mifumo mbalimbali ya kiuchumi, hata kuwa ndiye Rais pekee Tanzania kuiacha hazina ikiwa imenona wakati yeye aliingia ikulu, hazina ikiwa haina chochote, ikiwa na madeni lundo, kiasi cha nchi kutokopesheka. Mengi aliyoyafanya Kikwete msjngi wake uliachwa na Mkapa.
 
Kama elimu ingekuwa haijanisaidia nisengekuwa na kampuni nje ya nchi
Wewe kazi yako kulipwa vijisenti kumtukana Magufuli.
Kwa hiyo wewe elimu imekusaidia kumtukana Magufuli

Kipindi cha Magufuli Tanzania ilikuwa inaheshimika sana huku 🇳🇴 ata ukiulizwa unatoka nchi gani unajivunia unasema bila uoga Tanzania but nowadays inafikia hatua hadi tunaukana uraia wetu but tunaipenda Tanzania ndio maana tunatamani tupate viongozi kama Magufuli wenye uchungu na nchi sio wenye tamaa na familia zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…