Uchaguzi 2020 Kikwete, Mizengo Pinda na Kassim Majaliwa hamna ushawishi wowote kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, huko kwenye kampeni mlikojiingiza mnachorwa tu

Uchaguzi 2020 Kikwete, Mizengo Pinda na Kassim Majaliwa hamna ushawishi wowote kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, huko kwenye kampeni mlikojiingiza mnachorwa tu

Sasa wewe unahangaika nini? Hao wazee wote uliowataja kwa taarifa yako ni viongozi wenye heshima kubwa Sana kwenye taifa hili msifikiri watu wote Wana akili ndogo za kudanganywa na vimaneno vya hovyo hivi watu wenye akili timamu wanawaangalia tu mnayoweweseka
 
Sasa wewe unahangaika nini? Hao wazee wote uliowataja kwa taarifa yako ni viongozi wenye heshima kubwa Sana kwenye taifa hili msifikiri watu wote Wana akili ndogo za kudanganywa na vimaneno vya hovyo hivi watu wenye akili timamu wanawaangalia tu mnayoweweseka.
Kwanza heshima maana yake nini?
 
Erythrocyte,

Wivu tu! Nanyinyi si muwatume kina mbowe wakamfanyie kampeni lissu. Salum Mwalimu nae aende sehemu yake, Mnyika aende kwake, tuone kama hata nzi atasogea. Kila sehemu inabidi Lissu aende mwenyewe na bado maeneo mengine hana ushawishi.
 
Wivu tu! Nanyinyi si muwatume kina mbowe wakamfanyie kampeni lissu. Salum mwalimu nae aende sehemu yake, mnyika aende kwake, tuone kama hata nzi atasogea. Kila sehemu inabidi Lissu aende mwenyewe na bado maeneo mengine hana ushawishi.
Tunawaonya hao wazee wasije wakamlilia mtu
 
Wanajidhalilisha bure. Jitu limejimilisha chama kimekuwa Cha kihutu, wao ndio walimtuma asiongeze mishahara, asipandishe madaraja, aongeze makato bodi ya mikopo true wanajicholesha tu.
 
Nikianza na Kikwete, huyu mambo yote yalimvurugikia mwaka 2015 kutokana na kutokujiamini na uoga wake dhidi ya Lowassa, akaboronga na kupeleka nchi kushoto kwa kucheza kamari ya hatari sana na kumpa nchi mtu asiyestahili, katili na mwenye visasi vya hovyo sana ambavyo havijawahi kutokea kwenye nchi hii. Matokeo yake nchi yetu imerudi utumwani huku watu wakitekwa na kupotea katika mazingira ya hovyo sana yenye kuiletea nchi aibu duniani. Hata hivyo Kikwete hajawahi kukemea unyama huu wa kishamba, na tangu hapo wananchi wamemdharau sana, japo ameonekana Lindi kwenye mkutano wa kampeni wa CCM, wengi hawakuguswa na uwepo wake na wanaamini alikuja mahususi kumpigia kampeni mkewe, ambaye alifikia kuwa first lady lakini sasa anaomba tena ubunge. Maajabu! Kwa kifupi Kikwete ndio aliyesababisha nchi hii kuwa hivi, wananchi hawatamsamehe.

Mizengo Pinda, huyu hana uwezo wa kumshawishi yeyote kuhusu siasa za Tanzania , hana uwezo na wala hajawahi kukemea maovu popote Tanzania, wananchi siyo Wajinga na wanazo kumbukumbu na akili timamu. Pinda alipokuwa Waziri Mkuu alimzuia Magufuli aliyekuwa Waziri wa Ujenzi kubomoa jengo la Tanesco Ubungo kwa kisingizio kwamba liko kwenye hifadhi ya barabara. Hata hivyo, baada ya Magufuli kuwa Rais akarudi tena Ubungo na kulibomoa jengo lile kiroho mbaya bila huruma na wala bila faida yoyote, Pinda aliona lakini akaufyata, mtu kama huyu anaweza kumshawishi mwananchi gani kuichagua CCM?

Kasimu Majaliwa, huyu ndio funga kazi kabisa! Hana ubunifu na wala hajawahi kuwa nao. Katika kipindi chake chote cha miaka mitano alichofanya ni kupandisha ligi kuu kimagumashi timu ya kwao inayoitwa Namungo na kutumia pesa ya umma kujenga uwanja wa soka kwao. Hana alilolifanya zaidi ya kusoma hotuba za kufunga ama kufungua bunge. Aliufyata alipoambiwa mashangazi zake watatandikwa makofi kwenye sakata la korosho, ndugu zake wakazama kwenye mafuriko huku yeye akijificha DSM. Kwa kumbukumbu zangu huyu ndio Waziri Mkuu wa kiwango cha chini kabisa kuwahi kuwepo nchi hii, hana ubunifu wowote na kuna taarifa kwamba kwao hatakiwi kabisa na wananchi. Hii ndio sababu ya Wagombea ubunge Ruangwa wa vyama vingine kutekwa na kunyimwa fomu ili apitishwe bila kupingwa. Huyu hana uwezo wa kumshawishi mtu yeyote kuichagua CCM. Kampeni anazozifanya ni sawa na kupoteza muda tu.

Itaendelea...
Umepaniki
 
Unaanzaje kumuogopa mtu ambaye hata kukutana ulingoni ili mzipige uso kwa uso anaogopa anataka mwenzake aenguliwe ili apate ushindi wa mezani wa viti maalumu???
Akirudi tena nistue
 
....ambaye alifikia kuwa first lady lakini sasa anaomba tena ubunge! Maajabu....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna kitu huyu former First Lady anakosa nyumbani kwao hivyo anatafuta njia ya kutokuwepo nyumbani kwa kisingizio cha Bunge!!! She does not have the competence to be a useful member of parliament!!
 
Back
Top Bottom