Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Kamnanga tena mzee baba[emoji23]Rais mstaafu Kikwete amesema jambo ambalo wengi hawalijui ni kwamba mwaka 1988 yeye alipelekwa wilaya ya Masasi kuwa Katibu wa CCM na alimkuta mzee Mkapa akiwa ni mbunge.
Kikwete anasema walikuwa marafiki wa kweli hata mwaka 1995 yeye ( Kikwete) alipoburutwa kugombea urais bado alikuwa anamuunga mkono mzee Mkapa kama chaguo sahihi la wakati huo.
Kikwete anasema anamshukuru mzee Mkapa pamoja na ukweli kuwa walishindana kwenye urais lakini hakutaka kumpoteza kisiasa bali alimteua kushika wizara nyeti ya Mambo ya nje kwa kipindi cha miaka 10 na kumuwezesha kutimiza ndoto yake ya kuwa Rais katika muda muafaka yaani 2005.
Chanzo: BBC Dira ya Dunia!