Huyu mzee alikuwa anakuja nyumbani kuongea na mshua wangu. Zamani sana kabla ya haya mambo ya Escrow. Miaka ya mwanzo ya 1990s.
Sasa, ikafika wakati nikawa simuoni.
Nikamuuliza mshua. Mbona yule rafiki yako Mzee Rugemalira simuoni kuja nyumbani siku hizi?
Mshua akaniambia, mwanangu, unajua dunia hii kuna marafiki wengine wanakuwa marafiki kwa kutaka kitu fulani kwako, wakikikosa, na urafiki wao unaisha.
Basi kwa miaka mingi jibu lile lilikuwa kitendawili kwangu, nilikuwa sijalielewa vizuri.
Baadaye sasa kwenye hii issue ya Rugemalira kugawa pesa kama hana akili nzuri, ndiyo nikajumlisha moja na moja kupata mbili, kwamba huyu mzee alitaka kumhonga mshua wangu apate favors fulani, mshua akamkatalia.