Asante sana JF, hizi kumbukumbu zidumu ili vizazi vijavyo angalau vielewe kuwa pamoja na utawala wa kidhalimu wa viongozi kama Jakaya Mrisho Kikwete, kuna wazalendo wachache ambao hawakusita kuita koleo kwa jina lake, hawakutetereka katika kutetea maslahi ya taifa, hawakurudi nyuma hata walipokabiliana na nguvu za dola zikisimamiwa na mafisadi na wala hawakumung'unya maneno katika kuwaanika maadui wa taifa bila kujali nguvu na nyadhifa zao.
Wataelewa kuwa ingawaje nchi iliendeshwa na genge la wahuni, wezi na wauaji kwa kivuli cha chama tawala, CCM, wapo wananchi waliosimama kidete kupambana nao hata ikibidi kupoteza maisha. Kwa kifupi watafahamu umasikini uliowatafuna babu zao kwa miaka hamsini ulisababishwa na nani kwa uroho wa kubaki madarakani. Kwamba kulikuwa na wachache waliojitolea kukabiliana na hawa mafisi na manyang'au, bila shaka kutawapa faraja na kuwapunguzia machungu.