Mkuu wangu hao watu wa chuo, si ndio waliotuambia kwenye polls kuwa Muungwana, anakubalika kuliko wote, na ata-make a good president, kweli mkuu untaka tuongozwe na kina Prof. Mkandalla?
Urais siku zote ni learning on the job, unless uwe kwenye nchi kama USA, ambako kuna CIA, State Department, FBI, Congress, Judicial, ambao kazi yao ni pmaoja na kuiangalaia executive branch inafanya nini kila siku, lakini bongo inabidi wakampigie magoti Kigoda, ndio maana Muungwana majuzi alikuwa mklai kweli aliposikia kuwa Makamba, alikuwa akimpiga vita Kigoda kwa jina lake,
Kwenye kampeni za urais uliyopita, tuliambiwa na wananchi wengi kuwa tunataka vijana, haya vijana ndio wanaoongoza sasa hivi, sasa tukubali tu kuwa tulikosea, maana ukweli ni kwamba hatujawahi kuwa na serikali ya wasomi kama this time na vijana pia, lakini angalia yaliyotukuta, maana yake ni moja tu nayo ni kwamba kuanzia wananchi wa Tanzania, yaani sisi hatuelewi cha kufanya inapokuja kwenye uongozi, sasa wote turudi tujipange upya tuangalie tulikosea wapi, badala ya kuwalaumu tu walioko, maana kama ni Mlimani, Prof. Mbilinyi aliyekula hela za minofu ya samaki alitoke wapi Mkuu? Prof. Malima alitokea wapi?
Mkuu wangu Invicible,
Heshima mbele, unayosema ni kweli kabisaa, lakini bado hatuja-address matatizo yetu ya character, kutokana na kutokuwa na maadili ya uongozi, ambayo yataanzia kwenye level ya sisi wananchi pia kuwa na maadili ya kijamii, otherwise sisi wananchi haya mabadiliko hayatatusaidia kitu, bali viongozi wachache, maana hata kuanzishwa kwa vyma vingi walionufaika ni kina Mreema na Mtei, sio sisi wananchi, bila wanachi kuamshwa tutaishia kama Visiwani, wananchi wanamuaminia Seif tuu, mpaka sasa amenunuliwa hawaelewi cha kufanya maana kila kitu kilikuwa Seif tu,
Kama tusipokazana kuwaamsha wananchi, hata yanayoendelea sasa yataishia kuwanufaisha wachache tu, na sisi tutaendelea kupiga kelele tu hapa!
Lakini heshima kwa maneno yako mazito mkuu!