Kikwete wa Kenya na Kikwete wa Tanzania ni watu wawili tofauti

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
1,492
Reaction score
2,361
Rais mstaafu JK naona anasifia tume huru ya Kenya, wagombea binafsi na uwazi wa uchaguzi na anasema Africa ijifunze Kenya.

Binafsi maswali ni mengi kuliko majibu, alipokuwa Rais alifanya nini kuhakikisha hayo yanatokea? Si, ni yeye aliyeusambaratisha rasimu ya Warioba kwa hotuba yake pale bungeni iliyopangwa mwisho kinyume na utaratibu?
 
Huu utetezi wa kusema maigizo anayofanya JK kule Kenya eti ndio "siasa" hapo ndipo ujinga wetu watanzania unapoanzia na ndio maana tunaendelea kutawaliwa na CCM, na umasikini juu.

Siasa ni maisha ya watu, na siasa inapohusishwa na mfumo wa maisha ya watu haitakiwi kuletewa maigizo, lazima patengenezwe mazingira bora yatakayofanya washindani waheshimiwe na washindi kuaminika, pasiwepo na malalamiko.

Kenya wana tume huru ya uchaguzi, JK ameenda kule anaisifia kwa kazi nzuri inayofanya, transparency; anafanya hivyo akijua fika hii tume yetu hapa Tanzania ni tume iliyopo kwa maslahi ya CCM.

Alituanzishia mchakato wa Katiba Mpya ili tuwe kama wakenya anaowasifia kwa ile Rasimu ya Warioba, badala yake akakubali itupwe na kuletwa Katiba Pendekezwa kwa manufaa ya CCM.

Huyu anatakiwa aambiwe ukweli, amechezea pesa za walipakodi, na amepiga teke maoni ya watanzania yaliyokuwepo kwenye ile Rasimu ya Warioba kwa manufaa ya CCM, ni msaliti.

Lakini sio asifiwe kwamba alichokifanya ndio siasa, huo ni ujinga, ambao wakenya waliukataa ndio maana leo JK ameenda kule anawasifia kwa walichofanya.
 
Rais mstaafu JK naona anasifia tume huru ya Kenya, wagombea binafsi na uwazi wa uchaguzi na anasema Africa ijifunze Kenya.

Binafsi maswali ni mengi kuliko majibu, alipokuwa Rais alifanya nini kuhakikisha hayo yanatokea? Si, ni yeye aliyeusambaratisha rasimu ya Warioba kwa hotuba yake pale bungeni iliyopangwa mwisho kinyume na utaratibu?
WAKENYA wanapiga Kura na kuchagua WATANGANYIKA Tunapiga Kura ila tunachaguliwa
 
Siasa unaijua? Tuanzie hapo kwanza!
Siasa ni muhimu sana kwa sababu inahusika na maamuzi ya msingi kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla. Wapumbavu hutafsiri siasa kama udanganyifu, ghiliba na yanayofanana na hayo, kitu ambacho ni makosa makubwa.
 
Huu utetezi wa kusema maigizo anayofanya JK kule Kenya eti ndio "siasa" hapo ndipo ujinga wetu watanzania unapoanzia na ndio maana tunaendelea kutawaliwa na CCM.

Siasa ni maisha ya watu, na siasa inapohusishwa na mfumo wa maisha ya watu haitakiwi kuletewa maigizo, lazima patengenezwe mazingira bora yatakayofanya washindani waheshimiwe na washindi kuaminika, pasiwepo na malalamiko.

Kenya wana tume huru ya uchaguzi, JK ameenda kule anaisifia kwa kazi nzuri inayofanya, transparency; anafanya hivyo akijua fika hii tume yetu hapa Tanzania ni tume iliyopo kwa maslahi ya CCM.

Alituanzishia mchakato wa Katiba Mpya ili tuwe kama wakenya anaowasifia kwa ile Rasimu ya Warioba, badala yake akakubali itupwe na kuletwa Katiba Pendekezwa kwa manufaa ya CCM.

Huyu anatakiwa aambiwe ukweli, amechezea pesa za walipakodi, na amepiga teke maoni ya watanzania yaliyokuwepo kwenye ile Rasimu ya Warioba kwa manufaa ya CCM, ni msaliti.

Lakini sio asifiwe kwamba alichokifanya ndio siasa, huo ni ujinga, ambao wakenya waliukataa ndio maana leo JK ameenda kule anawasifia kwa walichofanya.
Sasa tufanyeje mkuu? Maana tuliwategemea kwamba wangefanya kitu, nao wameufyata. Yaani ni mwendo wa kubwia asali na maziwa.

Anzisha labda chama kingine, au hata harakati inayoeleweka???
 
Hata Mkapa wa Tz na yule msuluhishi wa majirani walikuwa tofauti.

Ccm waanarudishiwaga akili wakistaafu
 
Rais mstaafu JK naona anasifia tume huru ya Kenya, wagombea binafsi na uwazi wa uchaguzi na anasema Africa ijifunze Kenya.

Binafsi maswali ni mengi kuliko majibu, alipokuwa Rais alifanya nini kuhakikisha hayo yanatokea? Si, ni yeye aliyeusambaratisha rasimu ya Warioba kwa hotuba yake pale bungeni iliyopangwa mwisho kinyume na utaratibu?
Yaani huyu mzee ni mtu wa hovyo, familia yake imejaa bungeni unadhani atafnaya nini?
 
Rais mstaafu JK naona anasifia tume huru ya Kenya, wagombea binafsi na uwazi wa uchaguzi na anasema Africa ijifunze Kenya.

Binafsi maswali ni mengi kuliko majibu, alipokuwa Rais alifanya nini kuhakikisha hayo yanatokea? Si, ni yeye aliyeusambaratisha rasimu ya Warioba kwa hotuba yake pale bungeni iliyopangwa mwisho kinyume na utaratibu?
Uzuri ni kwamba Wakenya wamemstukia
 
Ukitaka kujua performance ya Jakaya katika demokrasia mlinganishe na Magufuli. Ndio utajua alichosema anamaanisha au la.

Uchaguzi ni kipengele kimojawapo tu kati ya vingi katika demokrasia. Mara fulani sio kila kitu ni kukosoa. Tutoe pongezi hata katika hatua ndogo ya mafanikio.

Katiba? Tunapima mtu kwa takwa la wakati huo la Mwenykiti wa chama pinzani? Nani aliyekwamisha? Kikwete au UKAWA/Vyama vya upinzani? Jakaya aliona ubovu wa katiba! Akatengeneza mazingira ya kuibadili. Wakaja wajuvi wa kupinga. Wakabutua....madhara yake wakayaona,wanadai upya!
 
Mchango wa hawa waangalizi huwa ni nini hasa maana uchaguzi unaisha changamoto kibao wao ni kutoa maoni kila siku miaka na miaka
 
Rais mstaafu JK naona anasifia tume huru ya Kenya, wagombea binafsi na uwazi wa uchaguzi na anasema Africa ijifunze Kenya.

Binafsi maswali ni mengi kuliko majibu, alipokuwa Rais alifanya nini kuhakikisha hayo yanatokea? Si, ni yeye aliyeusambaratisha rasimu ya Warioba kwa hotuba yake pale bungeni iliyopangwa mwisho kinyume na utaratibu?
Kikwete amekwepa kusema Tanganyika ijifunze badala yake ameitaka Afrika ijifunze! Hawa wanaccm ndivyo walivyo, kengine kale kako Malawi kajifunze huko siasa za kistaarabu za kuvumiliana na kuacha kupenda kuwa watawala. Mwingereza angekuwa kama CCM walivyo Tanganyika isingepata uhuru, mwingereza hakuwahi kuwa na mfungwa wa kisiasa na aliondoka bila rabsha akaahidi kuja kuitembelea Tanganyika baada ya miaka 10 na alifanya hivyo, ila la hakuamini alichokiona, maduka ya bidhaa muhimu na foleni za yanga.
CCM ni walewale hata wakiwa nje ya nchi usiwaamini kwani uongo kwao ni jadi.
 
Rais mstaafu JK naona anasifia tume huru ya Kenya, wagombea binafsi na uwazi wa uchaguzi na anasema Africa ijifunze Kenya.

Binafsi maswali ni mengi kuliko majibu, alipokuwa Rais alifanya nini kuhakikisha hayo yanatokea? Si, ni yeye aliyeusambaratisha rasimu ya Warioba kwa hotuba yake pale bungeni iliyopangwa mwisho kinyume na utaratibu?
Kikwete+kikwete=??
 
WAKENYA wanapiga Kura na kuchagua WATANGANYIKA Tunapiga Kura ila tunachaguliwa
Kenya wamefika hapo baada ya Wananchi kujitambua,kumbuka 2007 Mwai Kibaki alichokifanya,Wanacho wakachukua hatua iliyopelekea kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi mnayoisifia leo,sisi wa Tz hatujitambui.
 
Back
Top Bottom