GE2025 Kikwete: Wanaodai utaratibu wa kumpata mgombea CCM haukufuatwa labda wanajifanya hamnazo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Okay, fine. Tumeelewa. Ndiio utaratibu. Na hauna exception huo utaratibu.

Kwa nini mlifanya kimchakato cha uongo na kweli, na kura za mdomo za uongo na ukweli, kama utaratibu rasmi upo, na sio wa kura, za mdomo wala karatasi, na unajulikana, na unatumika ?

Kwa nini CCM inaruhusiwa na Tume kufuata taratibu ambazo hajizaandikwa kwenye katiba yao, au zinapingana kabisa na katiba yao ?


Nini maana ya kupeleka katiba yako kwa msajili wa vyama, na Tume ya Uchaguzi, na msajili wa nyaraka kama utakachofuata hakiko kwenye hiyo katiba ?

Kwa nini basi isitangazwe tu na chama, kwamba Samia ndio mgombea wetu kwa mujibu wa utaratibu wetu wa siku zote wa miaka kumi kumi ?

Na kwa nini Kikwete aliagiza, na Amos Makalla akatangaza, kwamba wajumbe wa kamati sijui ya kanuni tokeni nje, nendeni chemba mkaweke mambo sawa.
Walienda pembeni kuweka mambo gani ya kikanuni sawa ? Kanuni gani ilijitaji marekebisho ?

Madai kwamba Mkutano Mkuu una nguvu, unaweza kubadili kanuni, katiba, taratibu. Unawezaje kubadili katiba yako halafu ukaanza kutumia taratibu mpya kabla hujamwambia msajili kwamba tumebadili taratibu, mpya hizi hapa ?

Kwa nini mnatukuchulia Watanzania kama wapika gongo, hohe hahe vichwani, ambao hatujasoma kabisa kabisa kabisa ?
 
Tanzania hakuna Tume ya uchaguzi, kuna Tume ya ccm ya uchaguzi wa maigizo
 
ONa jinga hili.
 
Vijinenoneno-jk

Vidomodomo-karume

Uswahili kazi sana
 
Hata Mimi ningejizima tu data kama huyo Mzee!

Mke na mtoto wamepitishwa ubunge huku Mzee Pinda na Yusuph wa kwao wameliwa vichwa!!
Yule ma rope hana kifua cha uvumilivu kuna code alisema na figisu zake ikabidi wa muweke pembeni ! Ni jamaa yao lakini amepumzishwa kwanza.
 
Ukiona umefanya maamuzi ya jambo fulani na linapigiwa kelele, na mmejaribu kutoa ufafanuzi kila iitwatwapo leo, na ufafanunuzi huo bado haueleweiki, hauwezi kujisimamia wenyewe, hakika hapo mlichemka. Period

Mzee wangu JK, utafafanua sana lakini ukweli utabaki mlichemka vibaya sana kutokufuata utaratibu wa chama. Nakumbuka PM Majaliwa alikuwa anasema kwenye chama fomu ni moja tu, lakini hata yenyewe hatukiona mpaka kesho
 
Ujamuelewa Mchungaji Malisa pia, achana na Polepole labda ukumuelewa kabisa.

Hao watu kuwaelewa unatakiwa timamu kiakili, ukikurupuka uwezi kuwaelewa.
 
Polepole ndio alivyotaka kuwa mtu mzito wa ccm aingie anga zake ili ajibizane nae ;
Sasa Huyu mzee wa kikwere kajitumbuliza tuone jinsi Mheshimiwa Balozi atakavyomjibu!
Acha tuone atakamvyomjibu..!!
 
Ujamuelewa Mchungaji Malisa pia, achana na Polepole labda ukumuelewa kabisa.

Hao watu kuwaelewa unatakiwa timamu kiakili, ukikurupuka uwezi kuwaelewa.
Iko hivi Mkuu kwa kifupi kabisa ngoja nikufahamishe -:
Kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ya sasa yaani iliyopo imempa madaraka makubwa sana tena sana Mkuu wa Nchi ambaye huyo huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Chama cha CCM ambaye waoga wanasema huku wengine wamejificha kwamba amevunja kanuni na desturi za Chama !

πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜„πŸ˜‚ !

Nyerere mwenyewe alishaonyesha kuiogopa hiyo Katiba mpaka akasema hii Katiba akipatikana Rais atakayetaka kuyatumia madaraka yake kikamilifu watu watashangaa na Roho zao !

Kidogo kidogo akina Fulani wanaanza kumuelewa Mwalimu Nyerere !
Wasiomuelewa Mwalimu hao watakuwa ni akina Hamnazo. !
Usiangalie ulipoangukia bali angalia ulijikwaa wapi ndipo ukaanguka πŸ€£πŸ˜…πŸ˜„πŸ€·πŸΏβ€β™‚οΈ !
 
Yule ma rope hana kifua cha uvumilivu kuna code alisema na figisu zake ikabidi wa muweke pembeni ! Ni jamaa yao lakini amepumzishwa kwanza.
Marope ana ule ubitozi wa sekondari yeye mwenyewe anadhani ndio ujanja wenye kutosha kuutumia katika siasa za kuendeshea nchi!.

Alimkejeli kwa kibonzo JPM na marehemu akamsemehe tu. Karudia tena ujinga wa kumteta Samia yeye na Ummy Mwalimu matokeo yake wote wawili wamepigwa chini!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…