GE2025 Kikwete: Wanaodai utaratibu wa kumpata mgombea CCM haukufuatwa labda wanajifanya hamnazo

GE2025 Kikwete: Wanaodai utaratibu wa kumpata mgombea CCM haukufuatwa labda wanajifanya hamnazo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho amesema, "Najua kulikuwa na maneno eti utaratibu umekiukwa na mimi nililaumiwa kwa jinsi nilivyosema kwenye Mkutano Mkuu, lakini waliokuwa wanasema hayo ama hawafahamu utaratibu wa chama chetu, au labda wamesahau, au wanajifanya hamnazo"


Ni muhuni tu.

Yeye mbona alikuwa mpinzani, Shibuda mpaka wakamfanyia zengwe wakamtimua Chama.

Magufuli alikuwa na mpinzani pia ambaye ni Membe. Wakampiga zengwe wakamtimua chama.

Yeye ndiye atakuwa amesahau au hamnazo.
 
Mbona hajafafanua kuhusu ,je oil ilitakiwa imwagwe ,mama muda wake vipi? Mbona waziri mkuu na makamu wameachia ngazi?
 
Wengi walisahau kuuliza na kuelewa zile zinazoitwa AWAMU. Ilivyoitwa tu awamu ya 6 wenye kubisha hapo wangebisha ili ibaki kuitwa awamu ya 5. Ikishabadirika tu kutoka awamu ya 5 kwenda awamu ya 6, Mgombea kipindi cha PILI hawezi kuwa na wagombea wengine kwenye ulingo maana anamalizia awamu yake.
Wanaofahamu sasa watutueleza, ni lini mhula wa urais hauwezi kubadirika kuitwa awamu nyingine baada ya kufariki kwa rais akiwa madarakani. Rais aliyoko madarakani je akifa bado awamu yake imebakiza mwaka moja au miwili, au miezi michache, je hiyo awamu itabadirika au inabaki hiyo hiyo???
Kwani aliruhusu maswali?
 
Ila huyu mzee 😹
Bora angenyamaza tu..!!
Wacha tumsubiri Polepole amjibu.
Polepole ndio alivyotaka kuwa mtu mzito wa ccm aingie anga zake ili ajibizane nae ;
Sasa Huyu mzee wa kikwere kajitumbuliza tuone jinsi Mheshimiwa Balozi atakavyomjibu!
 
Back
Top Bottom