Kwa ustawi wa nchi yetu tunatakiwa kushughulika na wahalifu mmojammoja sio chama, dini wala kabila.
Yanayoongelewa na yaliyotokea kwa chadema yametokea kwa CCM na vyama vingine pia ila kikubwa ni kutoa ushirikiano kwa vyombo husika kumaliza matatizo hayo
Tumeona wana CCM wengi wakiuwawa na atujasikia ccm wakikituhumu chama cha chadema bali tumeona viongozi wakisema waliofanya hayo matukio watashughulikiwa.
Ukomavu wa kisiasa ni pamoja na kubeba mambo hatari kama haya kwa style ambayo tutajenga amani yetu zaidi ya kuibomoa
Kibiti. Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani hapa, Alife Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
www.mwananchi.co.tz
mtanzania.co.tz
MTU mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa ambao wanadaiwa kuwa ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kutokea vurugu za kisiasa katika mji wa Tunduma mkoani Songwe.
www.ippmedia.com
Mauaji Kada wa CCM Njombe, JPM Aagiza… September 28, 2020 by Global Publishers RAIS wa Tanzania na mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),&nb
theworldnews.net
Tukianza kunyoosheana vidole kwa vyama tutagundua kila chama kina maumivu ya kupoteza mtu wao na haitasaidia wala haitajenga utaifa wetu
Bado ya kunusurika kwa Mwakyembe, Magufuli, kifo cha Prof Mwaikusa, Dr Sengondo Mvungi na wengine
Tufike mahala tupunguze kuchocheana chuki tukifikiria itasaidia kufanikisha tunachokita. Tunaweza kujiona kwa sasa tunajenga kumbe tunazidi kubomoa.