Kila mauaji hushuhudiwa na macho matano

Wata weza kweli kumpata muuwaji wa Huyo mkuu washule kweli mbona kama ni ana PhD ya uuwaji
Uzuri ni kwamba, kwa maelezo ya mtoa mada, kuna macho mengi sana ambayo husaidia kufanikisha kukamatwa kwa muaji/wauaji, rpc muroto ametuambia jana kwamba eti marehemu alifariki baada ya moyo kushindwa kufanya kazi, anasahau kwamba mtu akikabwa koo moyo utakosa hewa na utasimama, kwa hiyo moyo kushindwa kufanya kazi haimaanishi kwamba mtu huyo amekufa mwenyewe kama ambavyo rpc alijaribu kutudanganya, kuna possibility kubwa kwamba aliuawa na wasiojulikana ambao sasa tumeanza kuwajua, maswali ya mtoa mada hapa juu ni ya muhimu sana kujibiwa
 
Hata kama nitaombwa kufanya hivyo hutojua

Jr[emoji769]
Mkuu wengine sio unajisumbua kuwajibu, watu wamezoea mada za kina diamond na alikiba, wakikuta mada za namna hii, yaani za kufikirisha wanaanza kuleta utani na mizaha, sio lazima kila mada u comment, sometime unapita unaenda zako vijiweni
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji109][emoji123][emoji109][emoji116]
Mkuu wengine sio unajisumbua kuwajibu, watu wamezoea mada za kina diamond na alikiba, wakikuta mada za namna hii, yaani za kufikirisha wanaanza kuleta utani na mizaha, sio lazima kila mada u comment, sometime unapita unaenda zako vijiweni

Jr[emoji769]
 
Mkuu kuna inshu ya evidence
Admissible na non admissible kwani hao wataalam wanaweza fanya uchunguz lakini evidence ikawa non admissible
Mfano dying declaration au ali bi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani iwe ndugu zangu wa Jamii Forum.

Nimeisikiliza kwa Makini taarifa ya RPC wa Dodoma Ndugu Muroto juu ya Kifo cha Ndugu yetu Mpendwa Marehemu Sheikh Rashid Bura ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa The Dalai Islamic Centre.

Awali ya yote napenda Jamii ifahamu kuwa;

a/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Rafiki yake na Kamanda Muroto.

b/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Mmiliki wa ZAMZAM PRE & PRIMARY SCHOOL.

c/ Sheikh Rashid Bura alikuwa akijishughulisha na shughuli nyingine pia (Naiweka kapuni kwa Sasa) licha ya kuwa ni Mmiliki wa Shule.

Kamanda Muroto ameficha mengi juu ya Kifo cha Sheikh Rashid Bura. Hapa naomba nielezee utata uliopo juu ya Kifo chake.

UTATA.

1. SAFARI,
a/ Marehemu Sheikh Rashid Bura alisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam siku ya Ijumaa Tarehe 20/12/2019 na siyo Tarehe 21/12/2019 kama alivyosema Kamanda Muroto. Tarehe 21/12/2019 ilikuwa ndiyo siku ya Kongamano / Mkutano huo wa Kidini. Katika Safari hiyo waliondoka watu wawili katika chombo kimoja cha usafiri.

b/ Tarehe 22 Marehemu alirudi Dodoma lakini akiwa amemuacha aliyeenda naye Safari huko Dar es salaam. Alipofika Dodoma alienda Kuswali katika MSIKITI wa NUNGE na baadae kuelekea Ofisini kwake.

NB: KWENYE TAREHE YA SAFARI KUNA JAMBO HALIPO SAWA.

2. MAWASILIANO,
Marehemu Sheikh Bura, aliwasiliana na Ndugu zake kwa njia ya Maongezi kwa mara ya Mwisho Jumamosi Usiku akiwa Dar es salaam. Baada ya hapo Simu za Ndugu zake hazikupokelewa tena na Meseji hazikujibiwa pia. Siku ya Jumapili Mawasiliano yaliyopatikana Pekee ni UJUMBE wa WHATSAPP ambao uliwapa taarifa Ndugu kuwa Amewasili Dodoma. Baada ya hapo hakukuwa na Mawasiliano tena.

NB: SHEIKH BURA HAKUWAHI KUTOPOKEA SIMU AU KUKOSEKANA HEWANI SIKU ZOTE AMBAZO AMEKUWA AKISAFIRI. KUTOPOKEA SIMU NA KUKOSEKANA KWAKE HEWANI KUMELETA MKANGANYIKO MKUBWA.

3. MAZINGIRA YA KUPATIKANA KWAKE,
Mazingira ya kupatikana kwa Sheikh Bura yana utata mwingi Sana,

a/ Sheikh Bura alipatikana Ofisini kwake siku ya tatu baada ya Mauti yake tena Mwili ukiwa umeanza kuharibika. Maswali ya kujiuliza,

i/ Je Ofisi yake haina Msaidizi wa Kazi ambaye angeweza kugundua kifo chake?

ii/ Je Ofisi za Jirani hawakuweza kusikia hata harufu ya kitu kinachotoa harufu kutoka Ofisini kwake?

b/ Polisi na Ndugu walipofika Ofisini kwake walikuta Mlango umefungwa na walipo uvunja na kuingia ndani walikuta mwili wa Marehemu LAKINI UFUNGUO HAUKUWEPO MLANGONI NA HATA NDANI PIA. Swali la kujiuliza, NI NANI ALIMFUNGIA SHEIKH BURA KWA NJE?

c/ Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulikutwa na Vazi lake la Kanzu lakini likiwa na Damu. Swali la kujiuliza, JE DAMU HII KWENYE KANZU YA MAREHEMU ILITOKA WAPI?

4. SIKU YA MAZISHI,
Siku ya Mazishi 26/12/2019 Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulitolewa Mochwari na kupelekwa Nyumbani kwake na Gari la Polisi na hata kutoka Nyumbani kwenda eneo la Mazishi (MAKABURI YA CHAMWINO / CHINANGALI) Mwili wake ulipelekwa na Gari la Polisi. Polisi pia walitoa basi lao kwa ajili ya kubeba wafiwa. Basi hili lilikwama Kwenye eneo karibu kabisa Ofisi ya Serikali ya Mtaa. Maswali ya Kujiuliza,

i/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Magari ya Jeshi la Polisi kubeba Mwili wa Marehemu mpaka Nyumbani na Eneo la Maziko?

ii/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Basi la Jeshi la Polisi kubeba wafiwa?

iii/ Uwepo wa Jeshi la Polisi kwenye eneo la tukio kulimaanisha nini?

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr[emoji769]
 
[emoji45][emoji45][emoji26][emoji26][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamechoka wanaona mtawasumbua tu wakati mishahara yenyewe haipandishwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukiamua kufuata weledi na kutumia wataalam kwenye fani husika... All unsolved murders will be solved

Jr[emoji769]
Mshanna hatuna clues zilizokusanywa, of is now IPO sawa KWA matumiz, muda umepita, Assad hataki kusema, doctor amepindishs taarifa, familia imezubaishwa

Watagundua nn zaid ya kusema huwenda aliuawa kupitia ushahid wa masimuliz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wauaji hawajawahi fahamika hadi leo tokea zama za mawe[emoji16]

Struggle For Success!
 
Na mimi niliamka leo na wazo la kujiuliza je wakati wanavunja mlango ufunguo ulikutwa wapi ndani au la, ila hapa umetupa jibu ndugu mshana na inaonyesha wazi kabisa aliuwawa kama ni kweli haukukutwa ufunguo. Ila wataalamu watusaidie kwani hawawezi kuchunguza alama za mikono kwenye kitasa pengine wanaweza kupata chochote.
Hilo la gari za polisi kubeba mwili huku kwetu kijijini ni kawaida naona mara kwa mara wanafanya hivyo sijajuaga sababu ni nini hasa, especially kama kuna utata wa kifo mf.mtu aliyejiua au kujinyonga.

Mshana Jr
 
Nieleweshe kwenye udongo hapo tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Udongo unatumika kwenye tasnia ya upelelezi ili kung'amua muhusika.

Nikupe mfano huu.

Muuaji ametoka Los Angeles kuja Miami Beach kufanya mauaji,

Akaja na Gari hadi eneo la tukio ambapo ni fukwe, alipomaliza Kuua akaondoka eneo la tukio moja kwa moja hadi Los Angeles.

Hapo, police wakija wataona alama za Tyres zilizoachwa na Gari ya yule jamaa,

Watachota sample ya udongo kutoka kwenye Tyres za gari na kuupeleka maabara ya kiupelelezi, baadae itakulikana muuaji alitokea Los Angeles mpaka Miami kwasababu udongo unatabia ya kutofautiana eneo na eneo.

Kiasi utakuwa umenielewa, Ahsante!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr kibongo bongo hao wataalam tunao? na kama wapo huchunguza mauaji yote au mpka auliwe mtu mweny jina na nafasi
 
unafaaa kuwa Mpelelezi kaka mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leta Uzi mwingine
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…