Amani iwe ndugu zangu wa Jamii Forum.
Nimeisikiliza kwa Makini taarifa ya RPC wa Dodoma Ndugu Muroto juu ya Kifo cha Ndugu yetu Mpendwa Marehemu Sheikh Rashid Bura ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa The Dalai Islamic Centre.
Awali ya yote napenda Jamii ifahamu kuwa;
a/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Rafiki yake na Kamanda Muroto.
b/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Mmiliki wa ZAMZAM PRE & PRIMARY SCHOOL.
c/ Sheikh Rashid Bura alikuwa akijishughulisha na shughuli nyingine pia (Naiweka kapuni kwa Sasa) licha ya kuwa ni Mmiliki wa Shule.
Kamanda Muroto ameficha mengi juu ya Kifo cha Sheikh Rashid Bura. Hapa naomba nielezee utata uliopo juu ya Kifo chake.
UTATA.
1. SAFARI,
a/ Marehemu Sheikh Rashid Bura alisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam siku ya Ijumaa Tarehe 20/12/2019 na siyo Tarehe 21/12/2019 kama alivyosema Kamanda Muroto. Tarehe 21/12/2019 ilikuwa ndiyo siku ya Kongamano / Mkutano huo wa Kidini. Katika Safari hiyo waliondoka watu wawili katika chombo kimoja cha usafiri.
b/ Tarehe 22 Marehemu alirudi Dodoma lakini akiwa amemuacha aliyeenda naye Safari huko Dar es salaam. Alipofika Dodoma alienda Kuswali katika MSIKITI wa NUNGE na baadae kuelekea Ofisini kwake.
NB: KWENYE TAREHE YA SAFARI KUNA JAMBO HALIPO SAWA.
2. MAWASILIANO,
Marehemu Sheikh Bura, aliwasiliana na Ndugu zake kwa njia ya Maongezi kwa mara ya Mwisho Jumamosi Usiku akiwa Dar es salaam. Baada ya hapo Simu za Ndugu zake hazikupokelewa tena na Meseji hazikujibiwa pia. Siku ya Jumapili Mawasiliano yaliyopatikana Pekee ni UJUMBE wa WHATSAPP ambao uliwapa taarifa Ndugu kuwa Amewasili Dodoma. Baada ya hapo hakukuwa na Mawasiliano tena.
NB: SHEIKH BURA HAKUWAHI KUTOPOKEA SIMU AU KUKOSEKANA HEWANI SIKU ZOTE AMBAZO AMEKUWA AKISAFIRI. KUTOPOKEA SIMU NA KUKOSEKANA KWAKE HEWANI KUMELETA MKANGANYIKO MKUBWA.
3. MAZINGIRA YA KUPATIKANA KWAKE,
Mazingira ya kupatikana kwa Sheikh Bura yana utata mwingi Sana,
a/ Sheikh Bura alipatikana Ofisini kwake siku ya tatu baada ya Mauti yake tena Mwili ukiwa umeanza kuharibika. Maswali ya kujiuliza,
i/ Je Ofisi yake haina Msaidizi wa Kazi ambaye angeweza kugundua kifo chake?
ii/ Je Ofisi za Jirani hawakuweza kusikia hata harufu ya kitu kinachotoa harufu kutoka Ofisini kwake?
b/ Polisi na Ndugu walipofika Ofisini kwake walikuta Mlango umefungwa na walipo uvunja na kuingia ndani walikuta mwili wa Marehemu LAKINI UFUNGUO HAUKUWEPO MLANGONI NA HATA NDANI PIA. Swali la kujiuliza, NI NANI ALIMFUNGIA SHEIKH BURA KWA NJE?
c/ Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulikutwa na Vazi lake la Kanzu lakini likiwa na Damu. Swali la kujiuliza, JE DAMU HII KWENYE KANZU YA MAREHEMU ILITOKA WAPI?
4. SIKU YA MAZISHI,
Siku ya Mazishi 26/12/2019 Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulitolewa Mochwari na kupelekwa Nyumbani kwake na Gari la Polisi na hata kutoka Nyumbani kwenda eneo la Mazishi (MAKABURI YA CHAMWINO / CHINANGALI) Mwili wake ulipelekwa na Gari la Polisi. Polisi pia walitoa basi lao kwa ajili ya kubeba wafiwa. Basi hili lilikwama Kwenye eneo karibu kabisa Ofisi ya Serikali ya Mtaa. Maswali ya Kujiuliza,
i/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Magari ya Jeshi la Polisi kubeba Mwili wa Marehemu mpaka Nyumbani na Eneo la Maziko?
ii/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Basi la Jeshi la Polisi kubeba wafiwa?
iii/ Uwepo wa Jeshi la Polisi kwenye eneo la tukio kulimaanisha nini?
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Jr[emoji769]