Kila Mtanzania anadaiwa takriban Tshs. Milioni 1.66 kutokana na deni la Taifa

"Mama hana deni" kwa hiyo sisi ndo tuna deni?. Hizi hela zinazokopwa na kuambiwa sisi Wananchi ndo tunadaiwa huwa zinaenda wapi jamani, mkeka wa matumizi ya fedha kwenye miradi hauwekwi wazi tunaambiwa tu kuna miradi imefanyika. Tunataka kujua ni shing ngapi zimetumika?

View attachment 3365872

Kufikia Machi 2025, deni la Taifa la Tanzania limeongezeka hadi Shilingi trilioni 107.7 kutoka Shilingi trilioni 91.7 Machi 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.9.

Kwa mujibu wa takwimu za idadi ya watu, kila Mtanzania sasa anadaiwa takribani Shilingi 1,668, 176.80.
Hii inatokana na ongezeko la idadi ya watu nchini kutoka 61,718,700 mwaka 2023 hadi kufikia watu 64,241,822 mwaka 2024, kwa mujibu wa makadirio ya Serikali.

Akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 bungeni jijini Dodoma leo, Alhamisi Juni 12, 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema ongezeko hilo la deni limetokana na Serikali kuendelea kupata mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ya kimkakati.
"Ongezeko la deni limetokana na Serikali kuendelea kupokea mikopo kutoka vyanzo mbalimbali ili kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, nishati na maji," amesema Prof.
Mkumbo.

Aidha, Prof. Mkumbo amebainisha kuwa licha ya kuongezeka kwa deni, hali ya uchumi wa Taifa inaendelea kuimarika. Pato la Taifa kwa mtu (per capita) limeongezeka hadi wastani wa Shilingi milioni 3.2 mwaka 2024, kutoka Shilingi milioni 3.05 mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 4.8.
Hata hivyo, katika thamani ya Dola za Marekani, pato hilo limepungua kidogo kutoka USD 1,276.8 mwaka 2023 hadi USD 1,227.4 mwaka 2024, hali inayoweza kuhusishwa na mabadiliko ya viwango vya ubadilishaji wa fedha au mwenendo wa soko la kimataifa.
Mimi silipi hata iweje, watu wanakopa pesa wakidai ni deni la taifa lakini wakizipata ni zao binafsi.
 
Kwani mkataba wa kukodisha bandari hautusaidii kulipa hilo deni??
 
Alipokua akitapanya ziliitwa pesa za Mama kwenye kulipa tunajumuishwa duh aiseee
 
Back
Top Bottom