Nabii ismail ndiyo yupi tena huyo? Shida yenu waislamu kila figure head kwenye torati ni nabii. Huyu alikuja na ujumbe gani?
Kule chini inasema pia paran labda ilikua sehemu ya Saudi Arabia,swali ni kwamba waisraeli walivyotoka Misri walipita Saudi Arabia ili kwenda Israel?
Uislamu hauna historia ya unabii,mlichofanya ni kujimilikisha historia za unabii na maeneo ya kiyahudi. Kisha mna wakana wayahudi kwamba matukio yao sio sahihi 😂.
Wayahudi hawajawahi kuwa na Mungu anaitwa Allah, manabii wao hawajawahi kuwa manabii wa Allah. Wanamjua mtu wa kwanza kuumbwa kwenye dini yao ni Adams,wa pili ni mkewe Hawa.
Quran imekopi lakini ikasahau kuhusu mke wa Adam, ndiyo maana mpaka leo waislamu hamjui mke wa Adam alikuwa anaitwa nani, Quran haijasema.
Chanzo cha dhambi ni Adam kila tunda na mkewe walilokatazwa na Mungu wao . Quran imebadilisha story,eti Allah aliwaambia malaika wamsujudie Adam shetani akagoma!!!
Wanafunzi wa Yesu wanasema Yesu alikufa na kufufuka, Quran inasema vinginevyo. Qur'an hiyo hiyo inamwambia Mohamed kama ana mashaka kuhusiana na utume wake basi akawaulize walioshushiwa maandiko kabla yake!!!!
Maandiko ambayo Quran imeyabadili na kuyachakachua. Pole sana.
Kumbe hata biblia huijui ?? hata Nabii ismail humjui ??
ALLAH KATIKA BIBLIA
Kiambishi tamati
"IM" katika neno
"ELOHIM" ni wingi wa heshima katika Kiebrania.
(Kumbuka kwamba katika Kiarabu na Kiebrania kuna aina mbili za wingi.
Moja ni ya idadi na nyingine ni ya heshima kama inavyotumika katika matangazo ya kifalme.
Kwa kuwa wingi wa heshima ni wa nadra katika lugha za Wazungu, wamechanganya aina hizi za wingi na kufikiria kuwa zinamaanisha wingi katika "utatu wa Mungu", na hivyo wakapata msingi wa kuhalalisha fundisho lao la Utatu Mtakatifu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu).
Kwa hivyo,
ELOHIM = ELOH + IM. Sasa nataka ufanye zoezi. Unaona maneno haya:
YA-HUWA ELOH-IM?
Weka kidole cha mkono wa kushoto juu ya herufi mbili za mwanzo "YA" zenye maana ya "Ewe!" na kidole kingine juu ya "IM" ambayo ni wingi wa heshima.
Unachobakiwa nacho sasa ni
Huwa Eloh au
Huwa Elah.
El kwa Kiebrania maana yake ni Mungu, na
Elah au
Eloh pia ni jina hilo hilo – Mungu. Kwa hivyo, "Huwa el Elah" au
HUWA 'L LAH, ambayo ni sawa kabisa na kauli ya Qur'an –
Huwal-lahu (maana yake:
YEYE NI ALLAH) katika aya ya:
QUL HUWA ALLAHU AHADU
SEMA:
YEYE NI ALLAH
YEYE NI MMOJA
(Qur'an Tukufu 112:1)
Zoezi hili linaonyesha wazi kwamba
El,
Elah, na
Elohim siyo maneno matatu tofauti.
Yote yanawakilisha neno moja la Kiarabu –
ALLAH. Hii siyo fikra yangu binafsi. Tafadhali angalia hapa chini.
Ni nakala ya picha halisi kutoka katika Biblia ya Kiingereza, iliyohaririwa na
Rev. C. I. Scofield, D.D., pamoja na maelezo yake ya Biblia.
Huyu Daktari wa Theolojia anaheshimiwa sana miongoni mwa wanazuoni wa Biblia katika ulimwengu wa Kikristo. Katika tafsiri yake hii ya “TOLEO JIPYA NA LILILOKAMILISHWA,” alisaidiwa na kundi la wanazuoni wengine wanane wenye shahada ya D.D.:
- Rev. Henry G. Weston, D.D., LL.D., Rais wa Crozer Theological Seminary
- Rev. W. G. Moorehead, D.D., Rais wa Xenia (U.I.) Theological Seminary
- Rev. James M. Gray, D.D., Rais wa Moody Bible Institute
- Rev. Elmore Harris, D.D., Rais wa Toronto Bible Institute
- Rev. William I. Erdman, D.D., Mwandishi wa “The Gospel of John,” n.k.
- Rev. Arthur T. Pierson, D.D., Mwandishi, Mhariri, Mwalimu, n.k.
- Rev. William L. Pettingill, D.D., Mwandishi, Mhariri, Mwalimu
- Arno C. Gaebelein, Mwandishi wa “Harmony of Prophetic Word,” n.k.
Sijawataja hawa wakubwa ili nikuogopeshe. Wote walikuwa na maoni ya pamoja ya kumuunga mkono
Rev. Scofield katika toleo lake hili la "New and Improved."
Tafadhali angalia katika maoni yao namba 1 chini kushoto, wanakubaliana kwamba –
"Elohim, (wakati mwingine El au Elah maana yake Mungu)" na pia imeandikwa kama
"Alah" (mstari wa tatu, neno la tatu). Je, inawezekana wataalamu wote wanane wa D.D. walikuwa vipofu na wakaandika neno
"Alah" badala ya
"God" ?
Je, walikuwa mbali kiasi gani na neno la Kiarabu linaloandikwa –
ALLAH – kwa Kiingereza? Nakuuliza ewe msomaji mpendwa. Hii ni kazi ya Allah, lakini Shetani (nitalazimika kuandika kwa herufi kubwa “S,” anastahili), hakukawia kurudi kwa haraka kupitia mawakala wake.
Aliweza kuwafukuza kazi wale D.D. wote waliowajibika kwa “kosa” hilo, na kuwaweka wengine tisa wenye shahada kubwa zaidi kuliko waliotangulia. Utawakuta katika toleo jipya la
"The New Scofield Reference Bible" Huwezi tena kuipata Biblia yenye neno
"Alah" ndani yake. Shetani ameihakikisha hilo.
KUFUTWA KWA HARAKA
"Sasa Unaiona" – "Sasa Huioni" ni mbinu ya zamani sana katika Magharibi.
Linganisha yaliyotajwa hapo juu uone jinsi kundi jipya la wamisionari walivyofuta kwa ujanja na werevu neno "Alah" kutoka kwenye "Toleo Lililoidhinishwa la Mfalme James" katika tafsiri ya Scofield ya Biblia