SI KWELI Kila mwanakikundi wa Ngoma kutoka Bagamoyo aliyeenda Marekani kuzindua Royal Tour alipewa Tsh. Milioni 3 kwa siku

SI KWELI Kila mwanakikundi wa Ngoma kutoka Bagamoyo aliyeenda Marekani kuzindua Royal Tour alipewa Tsh. Milioni 3 kwa siku

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa na madai ya kwamba wasanii walioambatana na Rais Samia Suluhu katika safari ya Royal Tour walikuwa wakilipwa Tsh. Milioni 3 ya kitanzania kama pesa yao ya kujikumu kwa siku nzima kwa siku zote walizokuwepo nchini Marekani.

1657981614258.png
 
Tunachokijua
Aprili 19, 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alizindua filamu maarufu ya The Royal Tour nchini Marekani, alianza kurekodi filamu hiyo Agosti 29, 2021 kwa lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vivutio vya utalii.

Miongoni mwa vikundi vilivyoambatana na ujumbe wa Tanzania kwenye uzinduzi wa filamu hiyo ni Kile cha Ngoma za Asili kutoka Bagamoyo, ambacho kinadaiwa kulipwa kila siku kiasi cha Tsh. Milioni 3 kwa siku zote kilichokuwa Marekani.

JamiiForums imefuatilia madai hayo na kugundua kwamba sio ya kweli. Wasanii wa ngoma za asili walilipwa kiasi ambacho hakikufikia hata Tsh. milioni 1 japokuwa hakuweka bayana kiasi halisi walichokuwa wakipatiwa na hawakulipwa kwa siku.

Wasanii wa ngoma wamelalamika kuwa kiasi cha kujikimu walichopewa hakikukidhi mahitaji yao na ilibidi waongezewe kiasi kingine wakiwa katikati ya safari.

Wasanii wa ngoma ni moja ya kundi la kisanii linalotumiwa sana katika shughuli za kiserikali lakini maslahi yao huwa hayatiliwi maanani kabisa na kupewa uzito unaostahili.

Hata hivyo JamiiForums haina uthibitisho juu ya kiasi halisi kilichotumika kulipa wasanii hawa na shughuli nzima ya uzinduaji wa filamu hii ya Royal Tour.
Back
Top Bottom