Angalia tu mazingira yalivyo, naamini Lissu sio mjinga kiasi hiko kuweka hili jambo hadharani,
Kumtaja mjumbe wa kamati kuu aliyempa siri za Abdul kuwa amefariki, akaja akasema maisha yake yako hatarini dhidi ya nani hasa? Tulijua ni mfumo ndio adui yake, akaenda kuchukua fomu za kugombania Uenyekiti makao makuu ya chama chake huku kavaa bullet proof vest, kama aliamini yupo salama kwenye makao makuu ya chama kwanini hakuvua hiyo bullet proof vest akaicha kwenye gari
kisha akaingia ofisini kuchukua fomu? Maana yake hata hapo makao makuu sio salama kwake na msumari wa mwisho amemalizia kwa kusema hana uhusiano mzuri na Mwenyekiti wake, wewe unajifunza nini?