Kila napoangalia naona kazi ya kutukuka ya Rais Samia, Tunataka nini tena Watanzania ili turidhike?

Kila napoangalia naona kazi ya kutukuka ya Rais Samia, Tunataka nini tena Watanzania ili turidhike?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Kama ukiacha akili yako iwe huru, ukaondoa mawazo ya uchama kichwani, ukatazama uongozi wa Rais Samia kwa mawazo huru yasiyofungwa na chochote Wala kupofushwa na chuki binafsi kwa Rais Samia, utakubaliana nami kuwa Rais mama Samia kafanikiwa kufanya kazi njema na ya kutukuka katika kila secta na kila eneo linalogusa maisha ya watanzania wanyonge.

Utagundua kuwa Rais Samia kafanikiwa kugusa maisha ya watanzania moja kwa moja, kajenga uchumi unaomgusa mtanzania,utagundua kuwa Mama Samia anaelekeza mamilioni kwa mabillioni ya pesa za kitanzania katika miradi inayogusa na kumnufaisha mtanzania mnyonge katika maisha yake ya kila siku

Mfano ukienda katika kilimo secta iliyobeba kundi kubwa la watanzania unakuta Rais Samia kaelekeza mabillioni ya pesa takribani billioni Mia moja hamsini kama Ruzuku , Hatua hii ya makusudi , kimkakati , kishujaa na kijasiri imepelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni,. Mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa elfu 70 tu, hii imewasha Taa ya Matumaini katika mioyo ya mamilioni ya watanzania wanyonge ambao wanategemea kilimo kuendeshea maisha yao,kwani hatua hii itafanya wakulima kuongeza uzalishaji na hivyo kuinuka kiuchumi na kupunguza umaskini wa Kaya.

Ukija katika Elimu unakuta mh Rais Samia kachukua uamuzi wa kufuta Ada na kufanya Elimu kuwa bure Hadi kidato Cha sita, hatua hii imewafuta machozi na jasho na kuwatua mzigo wazazi wengi waliokuwa wanahangaika kutafuta Ada kwa ajili ya kusomesha watoto wao,lakini pia hatua hii ya mama yetu mpendwa mama Samia imewasha na kuamsha Matumaini kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni nafasi ya Kuendelea na masomo yao bila kikwazo chochote kile,

Lakini pia mama yetu shupavu na Mama wa shoka amehakikisha ujenzi wa shule mpya nchini kwote na ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu nane nchini,Hali iliyopelekea na kutoa nafasi kwa wanafunzi wote wanaofaulu kupata Nafasi ya kwenda shule kwa wakati bila kukaa nyumbani Kama ilivyokuwa zamani ambapo wanafunzi wengine walikuwa wanakwenda muhula wa pili na hivyo kuwa nyuma kimasomo ukilinganisha na wenzao waliotangulia tangia mwezi January.

Ukija katika Afya,Unakuta mama wa shoka kipenzi Cha watanzania Tumaini la wanyonge na chaguo la watanzania Mama Samia ameimarisha Sana secta ya Afya kwa kuhakikisha ujenzi wa zahanati na vituo vya Afya mbalimbali nchini,mfano majuzi hapa takribani vituo vya Afya 234 vimejengwa nchini kwote,lakini pia ameimarisha upatikanaji wa vifaa Tiba , madawa na hata wataalamu wa Afya nchini kwote Kama ambavyo tumeshuhudia utoaji wa ajira za Afya miezi michache iliyopita ambapo zilitoka pamoja na zile za ualimu,

Hatua hii imesaidia na kusogeza huduma Karibu kabisa ya mtanzania na kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma. Lakini pia huduma za kibingwa zinapatikana na hivyo kupunguza zile safari za kupeleka wagonjwa nje ya nchi ambapo watanzania masikini wasio na uwezo wa kupeleka wagonjwa wao nje ya nchi waliishia kuwapoteza na kubaki na majonzi na uchungu mioyoni mwao ya kupoteza wapendwa wao kwa kukosa tu fedha, Sasa Hali Ni ya Matumaini Sana kwetu watanzania kutokana na juhudi za Rais Samia kuimarisha secta ya Afya

Ndugu zangu kila eneo utakalo kwenda iwe Ni suala la demokrasia au usambazaji wa maji, au umeme unakuta Rais Samia kafanya kazi kubwa Sana ya kugusa maisha ya watanzania, Ni ngumu kumaliza yote aliyoyafanya Rais Samia maana hapa patajaa kabisaa

Watanzania tukubali kuwa taifa Letu halitaongozwa na Malaika kwa kuwa hatuna Malaika miongoni Mwetu, Na katika Ubinadamu wake Rais Samia Anastahili pongezi kubwa Sana kutoka kwetu watanzania, Anastahili kuungwa mkono na kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii, Anastahili kuombewa na kila mtanzania ili mwenyezi Mungu amjalie Afya njema na nguvu za kututumikia watanzania.

Watanzania tunataka Nini Tena ambacho Rais Samia hajafanya? Nini ambacho Hakipo katika mipango ya Rais Samia ambacho tunaona kina umuhimu kwetu? Nini na wapi ambako hajagusa kiutendaji? Mimi naona kagusa na kufanyia kazi kila eneo linalo gusa maisha ya mtanzania mnyonge, kila eneo kaweka mkono wake wa upendo na huruma kwa mtanzania mnyonge na kila eneo kalitazama kwa macho ya utayari

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Hayo mapambio ni nusu ya yale ya mwendazake!!hayo semeni ambao mnafaidika na utawala uliopo madarakani,ila kwa walio nje na mfumo huo ,maisha wanayoishi kwa sasa,ni kama kipindi cha baada ya vita vya kagera.
Sipo serikalini Wala siyo muajiriwa wa serikali zaidi ya ukulima wangu, lakini juhudi za mh Rais zimegusa maisha yetu wakulima ndio maana tunaendelea kumuunga mkono mh Rais
 
Umelipwa shilingi ngapi kwa kuandika hii makala mkuu?!
Sijalipwa chochote na huwa silipwi chochote kutoka kwa mtu yoyote kuandika hapa zaidi ya Uzalendo wangu na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia
 
Watanzania wanataka mambo haya:
1. Katiba mpya.
2. Umeme wa uhakika na nafuu.
3. Gharama za chini za bidhaa na huduma.
4. Maisha yasiyokuwa na tozo
Hayo yote yameguswa na mh Rais wetu mpendwa mama Samia,mfano majuzi tu hapa Tumeona kikosi kazi kimewasilisha maoni yake juu ya suala Hilo la katiba mpya, kwa hiyo Tuwe na Subira kila kitu kitakuwa sawa na kiu ya kila mtanzania itamalizwa
 
Mfalme amevaa suti imemkaa vizuri sana
 
IMG-20221030-WA0007.jpg

Unajua kuna vitu unaandika Hadi Raisi mwenyewe anakushangaa kwa sababu Hata yeyé binafsi anatambua Nchi imeshamshinda.
 
Kuna watu wapumbavu kweli, lila unapoangalia hauoni umeme ni shida? Hauoni maji ni shida? Hauoni udhaifu, rushwa matumizi mabaya ya rasilimali? Hauoni bei ya bidhaa kupanda? Tozo na gharama za maisha kupanda? Lakini bado mtu anaongea utumbo!
 
Sasa ndugu mgao wa umeme na maji ndio kumgusa mwananchi sio?

bidhaa kupanda bei kila uchwao ndio kumgusa mwananchi sio?

kuleta mitozo ilihali hali za maisha ya wananchi ni mbovu ndio kumgusa sio?

Hatusemi kuwa hawajafanya chochote lakin sio kwa hayo mapambio unayoandika humu mkuu ilihali hali halisi haiendani na unachokisifia
 
Sasa ndugu mgao wa umeme na maji ndio kumgusa mwananchi sio?

bidhaa kupanda bei kila uchwao ndio kumgusa mwananchi sio?

kuleta mitozo ilihali hali za maisha ya wananchi ni mbovu ndio kumgusa sio?

Hatusemi kuwa hawajafanya chochote lakin sio kwa hayo mapambio unayoandika humu mkuu ilihali hali halisi haiendani na unachokisifia
Mgao wa umeme umesababishwa na Hali ya ukame inayoendelea hivi Sasa iliyopelekea kupungua kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hata hivyo juhudi za serikali kupitia TANESCO zinaendelea ikiwepo kutumia mitambo ya gesi kuzalisha umeme ili kupunguza makali,

Lakini pia watanzania Tuendelee kupeana Elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu na vyanzo vyetu vya maji, tusilime kandokando ya vyanzo vya maji Wala kuchoma misitu yetu hovyo
 
Back
Top Bottom