Bro hujui maisha yangu kabisa. Na wala sina haja ya kufanya comparison. Na huwa sina dharau, nimelelewa kuheshimu kazi na watu.
Hata hilo la kumwendeleza inaonyesha kabisa jamaa alikuwa anaona huyo mwanamke hawezi kufanya maamuzi yoyote ya maana. Leo hii hata watoto wetu huwa tunawasikiliza wanachokitaka.
Na vipi kuhusu swala la kuchepuka mbona hajaliongelea, aliendelea na yule mwanamke au aliacha? Na ameongea katika namna ya kwamba ilikuwa lazima kwa yule mwanamke amsamehe.
Bro, kuna sintofahamu nyingi sana kuhusu hadithi ya ndugu yetu. The way anavyoelezea msaada aliuotoa kwa mama mkwe, it was like he was counting everything. Najua wewe hujafika hapo kwa msaada wako mwenyewe, vipi unajisikia ukikorofishana na mtu halafu aanze kuelezea misaada aliyokupatia nyuma.
Mimi naona kosa la huyo mwanamke ni ignorance, exposure, na umaskini. Na ndio maana hata watoto kashindwa kulea vizuri.
Mkuu I rest my case, ngoja nifanye mambo mengine. Ila na wewe next time ongea kwa heshima bro, mimi mwenyewe mtoto wa mjini, matusi nayajua, nimechagua tu kutotukana.