Kila nikijaribu kutaka kufanya Maendeleo kwa wazazi wangu ninashindwa

Kila nikijaribu kutaka kufanya Maendeleo kwa wazazi wangu ninashindwa

Haya mambo yanaumiza sana.

Nina deni kubwa sana nyumbani, Sijui hata nalimaliza vpi.

Mshukuru Mungu sana kama umezaliwa kwenye familia Middle class kiasi kwamba hulazimiki kulipa Madeni ya Wazazi wako
 
Haya mambo yanaumiza sana.

Nina deni kubwa sana nyumbani, Sijui hata nalimaliza vpi.

Mshukuru Mungu sana kama umezaliwa kwenye familia Middle class kiasi kwamba hulazimiki kulipa Madeni ya Wazazi wako
Yani we acha tu kuna namna unajaribu kusema watajijua ila ukikaa ukawaza kwa umakini utagundua kuwa ni ujinga sana kutoa hiyo kauli

Kuna siku kwenye utahitaji kupeleka mchumba au wanao nyumban kwenu na zaidi kuna mabalaa yanayokeaga kwa sisi wanadamu Kwahyo nyumbani ni pahali panapohitaji kuwekwa sawa ata kwa kiasi tu
 
Sijajenga ila wazazi wangu wana nyumba yao ila ni kama pagale tu coz haija kamilika sehemu kubwa na ule mtaa wanao ishi wamezungukwa na watu wenye pesa karibu wote………..Huwezi amini!!!! Kwetu ndio imekuwa mfano wa kaya masikini kwa pale mtaani

Shida yangu kubwa ni kubadili mazingira ya pale japo kwa kiasi kidogo tu ili nipunguze ile picha ya kudharaulika pale mtaani ila ndio hivyo tena mabalaa yamekuwa mengi sana
pole mkuu, the same to me. na ukicheki mm mwenyewe kwangu mambo hayako poa . na hii ndio hali ya watanzania tulio wengi
 
Kwenye uchumi hakuna kitu kinaitwa huruma watch out

Ningekushauri fanya vitu basic tu
Maji
Umeme
La muhimu zaidi wazazi wapate chakula bora basi
 
tatizo linaanzia kichwani kwako,una elimu ya chuo kikuu hujui kupangila mambo bado unaamini huenda umerogwa.
Ushauri
Rudi darasani tafuta chuo kinachofundisha kuelewa sio kukariri kisha njoo kitaa tukupe elimu ya mtaa halafu tutakufundisha namna ya kufanya jambo kubwa kwa kuanza kufanya kidogo halafu utatoboa.
Strong code#😎12990📌
 
Kinacho kuponza ni kutoa taarifa juu ya marekebisho ya makazi kwa wazazi wako, fanya iwe siri yako jichange alafu ibuka tu bila ya taarifa utafanikiwa kufanya maboresho
Na hapo ndio mzizi wa tatizo, anaweza kutoa taarifa kwa nia njema kabisa ila binadam kwa kupenda sifa si ajabu wazazi wanazitoa hizo taarifa na huo ndio mwanzo wa mkwamo wa anachotaka kukifanya.
 
The same problem kwa tuliotoka familia duni,

The circle doesn't end, komaa na mmoja (mwenye akili) wenu atoke then Mwingine, that's the only way forward
 
Ninatoka familia duni sana ambayo kipato chao,mlo wao na ata makazi yao ni duni sana

Nina wakubwa zangu Ila na wao wote wana familia zao na wao pia hali zao zipo chini sana kiuchumi, kwahiyo pale nyumban nimebaki mimi na wadogo zangu wengine ambao na wao bado wanasoma

Mimi ndio mtu wa kwanza kufika elimu ya Chuo Kikuu kwa home na ata kiukoo kwa ujumla japo kiuchumi bado sipo vizuri sana

Ila sasa kila nikiwapigia simu wazaz wangu kuwa mwezi unaokuja nitakwenda kuwakarabatia nyumba yao na ata kuwawekea umeme na pamoja na maji. Zile pesa zote nilizo changa zinaishia kwenye mambo mengne tena ni ya ovyo sana

Ninajiona kama nina jukumu kubwa sana la kubadili hali ya pale home coz nikiwaangalia ndugu zangu sifikirii kama ata wana mawazo hayo,ila sasa hali ninayo kumbana nayo ndio Kama hiyo

Msaada pleasee,kuna nguvu za giza zinaniandama au ni maroho ya umaskini?
Hebu jaribu kujenga ukweni tuone? Jokes.....

Kabla ya kuanza kujenga fanya maombi na kukabidhi mpango wako kwa Mungu
 
Back
Top Bottom