Kila nikikumbuka ajira za ualimu nazo zina interview Sasa hivi nachanganyikiwa basi wangezingatia na miaka ya kuhitimu chuo

Kila nikikumbuka ajira za ualimu nazo zina interview Sasa hivi nachanganyikiwa basi wangezingatia na miaka ya kuhitimu chuo

Interview ni nzuri mazee maana uwezo wako ndio unakubeba tofauti na ule mfumo wa mwanzo ambao ulikuwa unategemea mabosi wa Tamisemi wameamka vipi maana unaweza Kuta wanakubaliana kwamba mwaka huu tuchukue waliomaliza 2018 na 2019 tu wengine nyote mnaachwa sasa huo ni ujinga .
 
tukiweka ushabiki pembeni ,,, hili swala ni kama serikali inajaribu kuwa ambiwa walimu kuwa walimu waliomaliza na kukaa miaka 5 6 mpaka 7 mtaani ,, watafute shughuli nyingine kwenye fani ya uwalimu hawaitajiki tenaaa ,, lakini sasa ndiyo hivyo tena serikali inashindwa lugha ya moja kwa moja ya kuitumia,, serikali inatamani kuajili vijana wa 2020 kuja juu basi ila sasa ndiyo hivyo huwezi kuwaambia watu wasiombe utanyanyua mjadala mzito sanaa

Unajua mfano mtu aliyemaliza let say 2017 ,, leo hii unaenda kumuuliza swali la course may introduction to psychology ,,, course hii huyu mtu aliisoma 2014 au 2015 sasa leo unaenda kumlazimisha akumbuke mambo aliyosoma miaka 7 nyuma na kuangalia kama kweli yupo compitent katika hilo eneo bila kujali other factors like time ,, na mambo mengine mengi,,, is like wame - assume huyu mtu toka alipomaliza yupo costant yani hajishughulishi na jambo jingine lolote isiokuwa shule tu ukwel interview ishakosa realibility...
Mwarobaini ingekuwa ni IQ test!! Hata kama umemaliza chuo leo kama IQ iko chini iko chini tu!! Kwa mfano unampa mtu kusoma habari fulani wakati huo huo anasikiliza taarifa ya habari kisha unamwuliza maswali kutoka habari aliyokuwa anasoma na maswali kutoka kwenye taarifa ya habari!! Mwenye IQ kubwa hata kama alimaliza chuo miaka 10 iliyopita atajitokeza tu!!
 
Wewe unaona wanatendewa haki??
Hakuna kelele kwa sababu toka mwanzo walikuwa wanapambana kwenye usaili kwa hiyo walishakubali matokeo!! Kama ni kulia wamelia hadi wamenyamaza!! Lakini watu wa Elimu na Afya walikuwa wanapangiwa vituo tu!!
 
Swala la umri nalo walipe kipaumbele aisee..kuna jamaa kamaliza chuo 2009 na sasa anaumri wa miaka 43 kabakiza miaka 2 Dirisha la usajili lifungwe kwenye swala la kuajiriwa serikalini.Ajira za hv karibuni nazo amejaribu kuomba tena na anasema mpaka dirisha la usajili lifungwe ndo atainua mikono juu....Huyu unaenda kumshindanisha... sisemi kushindanisha ni jambo mbaya hapana unamshindanisha na aliyemaliza chuo mwaka jana mi nadhani CV yake huyu ndo ingempitisha kwa sababu hata akiajiriwa kabakiza miaka 17 tu ya kustaafu nalo hili waliangalie sana.
nafasi ni chache serikali yenyewe haielewi imuchuke nani imuache nani,

Huu ndio Muda wa matambiko sasa 😁
 
Watu mnazungumzia kukaa mtaan miaka 5?

Nimehitimu chuo 2015,, mpaka muda naandika hapa nipo najishughulisha n biashara ya miwa.

Interview hata nikiitwa sitaenda maana sikumbuki chochote .

Ila naamin nikiajiriwa nitahitaji week mbili tu kuwa vizuri na hakuna atakayenikaribia kwenye uchapaji kazi Kwa sababu nafaham ilivyo kazi kupata kazi.
Wanazingatia lakini kwanza ufaulu
 
Back
Top Bottom